Tupunguze desturi ya kuongelea maisha ya watu

Tupunguze desturi ya kuongelea maisha ya watu

Umbea mbaya sana,kwanza mtu binafsi we mwenyewe una mambo mengi yanakuzonga, hivi utamwongelea mtu mwingine Ili upate nini,ufaidike na nini!!,huko nikupoteza wako tu,
 
Muda mwingi niko home kuna mafundi wanaendelea na ujenzi tangu july nimegundua kitu

Hawa jamaa ni wanaume lakini wanavyongelea maisha ya watu wananishangaza

Muda mwingine niko ndani hawajui kama niko ni mwendo wa umbeya. hadi mimi humo ndani najadiliwa

Kidogo watamix na story za mpira ila mazungumzo 85% ni maisha ya watu tena private life kabsa

Utaskia unamjua yule bwana ee naskia alikopa hela eee halafu yule ee hizi gari naskia ni mikopo ee
halafu yule ee anasumbuliwa na presha aah aah eeh iv yule ni kabila gan ahh kumbe aiseee mke wake ehh ahh ivi na yule ni mtoto wake eeh ahh na blah blah kama hizo .
According to plato;
Low mind: Discuss about people
Average mind: Discuss about event
Great mind: Discuss about idea
 
Na wao walikuwa wanasema tabia mbaya za watu.
Embu soma mada tena uone mfano wa kinachosemwa na mtoa mada..
Cha mwisho acha hizo mambo maana masengenyo ni dhambi maana umeweka ngao kabisa kutetea
 
Back
Top Bottom