Rashid Fed Chaula
Member
- Jun 17, 2024
- 7
- 5
Kukwama na kusuasua kwa maendeleo ya Tanzania yanaweza yakawa yameshikiliwa na mambo machache ambayo kama yakibadilishwa yanaweza kuchochea mabadiliko ya kimaendeleo ya kasi sana.Nchi ni mali ya watu wote kila kiongozi na raia atambue wajibu wake na kutekeleza kikamilifu. Maamuzi magumu yafanyike katika maeneo yafuatayo ili kuyafanya yabadili hatima ya nchi kwa kipindi husika.
1-Mihimili mitatu ya dola Serikali, bunge na mahakama ifanye kazi kwa uhuru pasipo kuingiliana. Dola inayo mihimili mitatu ambayo ina mamlaka ya kujiongoza na kufanya maamuzi yake yenyewe. Kuingiliana kwa maamuzi kati ya mhimili mmoja na mwingine ni kukiuka kwa katiba ya nchi. Serikali itunge sera zake katika nchi na kuwezesha utawala bora, bunge kutunga sheria mbalimbali za nchi na mahakama kutafsiri sheria za nchi na kusimamia katiba. Licha ya mihimili hii kufanya kazi kwa ushirikiano katika nchi lakini kila mhimili unayonafasi ya kusimama wenyewe kama wenyewe katika maamuzi kwaajili ya maslahi ya taifa.
2-TAKUKURU iwe huru katika utendaji kazi wake. Taasisi muhimu ya kuzuia na kupambana na rushwa ikitekeleza majukumu yake pasipo kuwa na kizuizi kutoka mhimili wowote inaweza saidia kuwepo na unyoofu katika huduma zote. TAKUKURU haipaswi kuegemea upande wowote katika maamuzi yake. Uhuru wa taasisi hii utachochea haki katika utoaji wa huduma na kudhibiti vikali rushwa katika maeneo yote nchini.
3-Kujihudhuru haraka kwa kiongozi mara tu anaposhukiwa kujihusisha na rushwa au ufisadi.
Rushwa ni adui wa haki,ufisadi ni ubadhilifu wa pesa za umma kwa maslahi binafsi. Ikiwa kiongozi yeyote wa ngazi yoyote atahusishwa na rushwa na ufisadi hapaswi kuendelea kuwa kiongozi. Lazima aachie ngazi husika na achukuliwe hatua kali za kisheria. Hii itapelekea nidhamu kwa viongozi wote madarakani. Pia, miradi mbalimbali nchini itatekelezwa kwa viwango sitahiki kulingana na bajeti iliyotengwa.
4- Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali afanye kazi bila kuingiliwa na ripoti yake ifanyiwe kazi kwa kuchukua hata stahiki. Yeye ni mamlaka ya kikatiba ambayo inaweza kuchunguza mgao wa mapato na masuala yanayohusiana na uchumi wa nchi. Huyu ndiye mkaguzi mkuu ambaye kazi yake ni kwenda katika uchumi, ufanisi na wa matumizi ya rasilimali za nchi. Kwa hiyo kama yupo kikatiba anayo mamlaka ya kutoa ripoti pasipo kipingamizi chochote kile. Hii itachochea bajeti za miradi mbalimbali kutumika kama zilivyokusudiwa na kwa viwango madhubuti.
5-Tume ya uchaguzi iwe huru kabisa.
Mfumo wa upatikanaji wa viongozi wa tume ya uchaguzi usitegemee chama au mhimili mmoja wa dola. Kusiwe na kiongozi yeyote katika tume ya uchaguzi anayeteuliwa na chama tawala. Ninapendekeza mihimili yote mitatu ishiriki katika upatikanaji wa viongozi wa tume ya uchaguzi
Mara tu baada ya kupatikana asiwe na chama chochote. Uchaguzi ukiwa huru na wa haki utawezesha upatikanaji wa viongozi waliochaguo la watu. Sera bora za kiongozi wakati wa kampeni ndizo zitakazompa nafasi katika uongozi.
6-Rasilimali za nchi zitumike kulineemesha taifa kuondokana na umaskini.
Rasilimali za nchi zikitumika vema zinauwezo wa kuibadilisha nchi yetu kutoka katika umaskini na kuwa taifa tajiri. Rasilimali kama madini, milima , gesi, misitu, mbuga za wanyama vikiundiwa sera nzuri na kupata wa taalamu watakaopanga vizuri namna ya kunufaika navyo itakuza pato la taifa na kutuwezesha kulipa madeni ya taifa. Kuna mataifa mengi duniani hayana rasilimali kama Tanzania ila ni mataifa tajiri zaidi kuliko Tanzania.Kama taifa tuwekeze katika kupata wataalamu wa ndani watakaosaidia nchi kujitegemea. Nilitamani sana Tanzania iwekeze katika viwanda ili taifa litoe bidhaa na sio rasilimali.
Mfano mdogo; Tanzanite ni madini pekee yanayopatikana Tanzania tu dunia nzima. Serikali ikachunguza bidhaa zinazotengenezwa na madini ya Tanzanite. Ikajenga viwandavya kutengeneza bidhaa hizo kwa ubora wa kimataifa. Ikaamua hatutatoa madini ila bidhaa za madini husika. Pia kama kuna mwekezaji basi aje awekeze katika viwanda vya ndani ili kuzalisha bidhaa na sio kutoa madini nchini na kupeleka taifa jingine. Hatutabaki tulipo lazima tutainuka kiuchumi.
Mwisho, Tuanze kufanyia kazi maeneo madogo madogo. Tuyarekebishe pasipo kuyaonea haya. Viongozi washirikiane na wananchi katika kuboresha mifumo mbalimbali. Uongozi uzingatie demokrasia kwakuwa demokrasia ni serikali ya watu kwaajili ya watu. Maendeleo ya nchi ni yetu sote kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Upvote
6