Turekibishe ulaji wa kisiasa usio na tija katika katiba mpya.

Turekibishe ulaji wa kisiasa usio na tija katika katiba mpya.

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Siku tutakayopata fursa ya kuandika katiba mpya ya nchi tukumbuke.

1. Kufuta nafasi ya waziri mkuu.
Hakuna tija kuwa na waziri mkuu na makamu wa rais pamoja.

2. Kufuta nafasi za manaibu mawaziri.
Mawaziri wanatosha kumshauri rais na kufanya maamuzi ya kisera na kisiasa katika wizara zao, kazi nyingine zifanywe na watumishi wataalamu wasio wanasiasa katika wizara.

3. Kufuta ubunge wa viti maalumu

4. Kufuta nafasi za ukuu wa wilaya.
Hakuna tija kuwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya, mkurugenzi wa Halmashauri, DAS na mkuu wa wilaya pamoja.

5. Kuweka ukomo wa idadi ya mawaziri.
Mfano hakuna tija ya kuwa na wizara za vijana, jinsia na michezo.
 
Moja ya feature ya demokrasia ni kuwa na walaji wengi. Ukipunguza vyeo hao unaowaacha wataenda kukupinga.
 
Kupunguza masilahi ya wabunge. Tuondoe kiinua mgongo cha milioni 400 kila baada ya miaka mitano kwa kila mbunge. Pia malipo yao yapunguzwe mpaka kima cha waajiri wa kawaida yaani milioni 2-3..
 
Back
Top Bottom