Tusaidieni kupata kadi za NIDA ndani ya muda mfupi

Tusaidieni kupata kadi za NIDA ndani ya muda mfupi

ERICKY_TZ255

Member
Joined
Aug 27, 2024
Posts
49
Reaction score
42
Yani kati ya kitu kimoja kikubwa Tanzania imeshindwa kutoa huduma yake kwa angalau hata asilimia 30% ni huduma ya NIDA yani huduma hii imekuwa tatizo kubwa sana kwasababu inaweza pelekea mtu kukosa kuendelea na masomo sababu ya kukosa namba ya NIDA itakayomsaidia mtu aliyemaliza Kidato cha Sita.

Tunaombeni sana sisi Wananchi mtuwezeshee kupata huduma hiyo ndani ya muda mchache mfanye hata tulipie ili turahisishe hili swala. Asanteni.

UKIONA POST HII JARIBU KU-SHARE IFIKE NGAZI ZA JUU ILI TUPATE SULUHISHO MAPEMA 🙏🏻🙏🏻🤝
 
Inashangaza kwa kweli.
Ikiwa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) inaweza kutoa kadi ya mpiga kura ndani ya saa chache; inashindikana vipi kwa NIDA kufanya hivyo?
 
NIDA walipaswa kuwa wabunifu wapite kwenye mashule kusajiliwa wanafunzi wa kidato cha nne wanaomaliza shule.

Hao ni raia wapya wanaoingia mtaani katika nyanja za juu za kielimu na soko la ajira
 
Inashangaza kwa kweli.
Ikiwa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) inaweza kutoa kadi ya mpiga kura ndani ya saa chache; inashindikana vipi kwa NIDA kufanya hivyo?
Kadi ya NIDA sio sawa na kitambulisho cha kupigia kura.
 
Utofauti wake ni nini??.
Ukipata kitambulisho cha NIDA unapata access nyingi hivyo lazima vitolewe kwa umakini sio haraka haraka kama kitambulisho cha kupigia kura ingawa ucheleweshaji wao unaweza kuwa ni uzembe pia. Muhimu umakini uwepo tu kuhakikisha ni wa-Tanzania pekee ndio wanaopata vitambulisho hivyo.
 
Mimi tangu nilivyopiga picha 2018 mpaka leo cjapata hata namba ya nida yenyewe,mwisho nimeamua kukubali tu yaishe
 
Mimi tangu nilivyopiga picha 2018 mpaka leo cjapata hata namba ya nida yenyewe,mwisho nimeamua kukubali tu yaishe
Upo Mkoa gani ndugu yangu??.🙄 Na nasikia hairuhusiwi kufanya maombi zaidi ya mara moja.😂🤣
 
Ila ukipata namba ya NIDA ndo unakuwa Mtanzania halisi kila kitu NIDA itafika mda hata Kupata Access hambazo hazihusiani na NIDA itabidi uwe na NIDA
 
NIDA walipaswa kuwa wabunifu wapite kwenye mashule kusajiliwa wanafunzi wa kidato cha nne wanaomaliza shule.

Hao ni raia wapya wanaoingia mtaani katika nyanja za juu za kielimu na soko la ajira
Hii iko Sawa.
 
Attachments

  • FB_IMG_17250929941752127.jpg
    FB_IMG_17250929941752127.jpg
    721.1 KB · Views: 5
Back
Top Bottom