Tuseme tu ukweli, ujenzi unahitaji kujinyima sana

Sitasahau wakati najenga msingi, niliporudi site jioni, nikakuta wamemwaga zege kwenye nguzo na imekaa upande, nikasema mbona nguzo hii sijaielewa, fundi uchwara akaniambia ikikauka tutatindua kidogo tu inakaa squire. Nikasema hapana, nikamtafuta fundi mmoja alikuwa anajenga site nyingine jirani kabisa na kwangu, tukakubaliana tubomoe inawezekana chini hakusuka kitako na kumwaka zege la uji, kufukua tukakuta jamaa kakunja nondo akaizamisha kwenye udongo dadeki!! Nikampigia fundi akaja kuona uozo wake, nilimfyatua na mkanda begani akainama nikalala naye chini alikula kipigo cha mbwa Koko hatasahau.
 
Alikua kashakuibia mzee😀😀
 
Nilipata Stress baada ya kupiga mahesabu ya kupaua nyumba yangu iliyotosha 9M. Badala yake ikafika 14M. Nilichanganyikiwa.
Stress gan ulipata au ulipata fundi alikupa bei sna za kupaua nyumba yako karibu tukuasaidie kkupa mafundi bola na wazuri na wenyew weled na kazi zao na mbao utapata kwa bei nafuu sna wasilian nasi 0782 425190.
 
Stress gan ulipata au ulipata fundi alikupa bei sna za kupaua nyumba yako karibu tukuasaidie kkupa mafundi bola na wazuri na wenyew weled na kazi zao na mbao utapata kwa bei nafuu sna wasilian nasi 0782 425190.
Asante next time. Fundi alinipa design kaniambia sijui British vs French. Mwisho wa siku kwangu niliona gharama ziliongezeka kinyume na matarajio.
 
Fundi kaniambia et kuta atainua wa million tatu!!!!

Vyumba vipo vi5
Nkaona ujinga hu ngoj nili pozi njichange
Wakat naendelea kawaza kuna mwingine kaomba kazi atajenga kwa laki9
Nae bado nnamfikilia hapa

Kuna fundi kaniambia wanajenga kwa 200 tofali moja

So unahesabu tofali unazidisha mara 200 unamlipa mnaachana
 
mwamba akili yako imenifaa hapa nilipo.

good knowledge
 
Ilibaki kazi ya kufanya finishing kuweka gypsum Chumba na sebule Tu

Fundi akaja akaniambia inahtajika 500k akimaanisha kazi itakua na

awamu mbili

Awamu ya 1 ni kuja kupga boundary na kufunga Gypsum Boards

Awamu ya 2
ni kuja kufanya skimming,na Rangi wanakua wamemaliza.

Nikakaaa nikatafakari weee baada ya miezi kadhaa nikawaita wapige kazi

hapo moyo unahisi kabisa nimepgwa (ila sikua na namna) wakamaliza kweli nikakabidhiwa

kazi AISEEE ile pesa ni sawa na maajabu waliyoyafanya,Japo iliuma ila nili ridhika na kazi yao.

NEXT TIME


Mchezo wangu ule ule ila saivi nikasema hapana siwezi tumia 500k kwa chumba na sebule tu

nikatafuta mafundi nijuapo nikapata wakupga Kazi yote Full kwa 150k nikampa kazi,Kazi ikaanza

kwakweli kilichonikuta na kazi nilivyokuja kukabidhiwa eti ndio tayari imeisha walahi niliishia kuwapa 100k

Tangu hiyo siku nimekoma tumia Mafundi wa bei za kitonga Nimekoma,Nikiwa na mafundi wa 5 nikiwa interview

mwenye ataniambia BEI KUBWAAA ndio nitampa kipaumbele kujua kwann yeye ni bei kubwa,staki mafundi cheap cheap mimi...sitaki aseeeee.
 
Fundi kaniambia et kuta atainua wa million tatu!!!!

Vyumba vipo vi5
Nkaona ujinga hu ngoj nili pozi njichange
Wakat naendelea kawaza kuna mwingine kaomba kazi atajenga kwa laki9
Nae bado nnamfikilia hapa
Mtumie huyo alietaka 3M mkuu

Najua kakuanzia 3m kwasababu anajua mtashushana bei so mshushe shushe

KUMBUKA hatokua peke yake atakua na wasaidizi ambao atawalipa pia si kwamba

hela atayochukua ataikunja yote mfukoni, lakini pia Fundi hawezi ropoka hela mingi hivyo

kama hajiamini,kabla hujamchukua Mwambie siku akipata kazi akupgie uende huko site kwake

ukamkague uone anavyopga kazi... Mimi mafundi wangu huwa nawapata kwenye ma site ya watu

nikiwa napita mahali nikaona nyumba inasimamishwa nikaielewa Huwa naenda pale nachukua namba za fundi mkuu

katika kila ninachojenga mafundi zangu wote sitafutiwi huwa nawatafuta mwenyewe na wote nawakutaga kwenye site

za watu wakipga kazi wakiwa huko huko ndio nachukua Namba zao za simu,Epuka kutumia mafundi wakupointiwa

mtu asikwambie Flani ni fundi mzuri hata kama akisifiwa na watu 20 isiwe kigezo chakumtumia "yashanikuta mwenzako"

Kila mtu ana vigezo vyake anapotafuta fundi mzuri,kwangu mimi fundi tu asie na Vifaaa vya maana vya kazi yake kwangu huyo "sio fundi bora" Fundi lazima awe na zana/vitendea kazi.

Nilipataga fundii wa wiring wakupointiwa yule jamaa yaliyonisibu sikuamini kama ni yule fundi anaesifiwa na kila mtu sikuelewa sifa zake zinatoka wapi.
 

Ahsante kunikumbusha mkuu
 
changamoto niliyoipata wakati najenga nyumba yangu ndogo mafundi waliniibia mno kwani nilikuwa si muelewa wa vitu, yaani fundi alikuwa kila maora aniambie kimeisha hiki mara kile kumbe anakwapua pembeni yaani acha tu mpaka nimeamliza yaani nimekoma sana
 
nataka kujenga flemu tatu za kawaida je matofali mangapi yanatakiwa na cement mifuko mingapi?
 
Daaah!!! Umejenga hoja zako vizuri sana, tunashukuru kwa ABCs zako nzuri.
 
nataka kujenga flemu tatu za kawaida je matofali mangapi yanatakiwa na cement mifuko mingapi?
Mtafute Fundi ndio atakupa majibu kulingana na Ukubwa wa Chumba/Vyumba vyako.

Upana uwe ngapi Urefu kwenda Juu uwe Futi ngapi kisha ndio atakwambia idadi ya matofali yanayohtajika kulingana na mahitaji ya frem zako.

Kila frem ina ukubwa tofauti kwahyo huwezi pata jibu la moja kwa moja ni matofali mangapi au cement mifuko mingapi.
 
asante mkuu ngoja nifanye hivyo
 
Ujenzi unahitaji usimamizi was halo ya juu,mafundi walijenga ukuta viziri kwenye kufunga mbao za linta tofali zitaingia kwa ndani badala ya kurekebisha hizo kozi kwa kuzijenga viziri Cha ajabu walimwaga linta hi yohivyo,marekebisho kwa baadae yanakuwa makubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…