Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Kwa sasa kumekuwa na vita kali ya maneno, dhihaka, majigambo, vitisho na kebehi mbalimbali baina ya makundi mawili ndani ya CCM, kundi moja likiunga mkono utawala uliopita wa Magufuli (huku likikosoa vikali utawala wa sasa wa Samia) dhidi ya kundi linalounga mkono utawala wa sasa wa Samia (huku likichafua vikali utawala uliopita wa Magufuli). Na msamiati wa ulioshika kasi ni Uhuni na wahuni.
Makundi yote hayo mawili yanakubadiliana jambo moja kwa hakika, kuwa CCM ni chama chenye wanachama na viongozi waandamizi wahuni na wanaofanya mambo kihuni kihuni.
Maswali fikirishi ni kuwa, ilikuwaje wahuni wakaingia ndani ya CCM na kupewa vyeo kihuni, wakafanya uhuni wao mpaka kuhakikisha CCM inaendelea kukaa madarakani muda wote kihuni kihuni?
Kama Nape, January na Kinana ni wahuni ndani ya CCM, vipi kuhusu ule 'uhuni' wao wa bao la mkono wanaodaiwa walioufanya 2015 mpaka Magufuli akaingia madarakani?
Kama Polepole na Bashiru ni wahuni ndani ya CCM, vipi kuhusu ule 'uhuni' wao waliofanya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu wa 2020 uliopelekea Magufuli kuendelea kukaa madarakani?
Yaani leo CCM inataka kusema wahuni hawatakiwi ndani ya CCM lakini matunda ya uhuni wao wataendelea kuyatumia, kujivunia na kuyaenzi!
Unawezaje kuitenganisha falsafa ya CCM kuendelea kukaa madarakani na wahuni wake waliowezesha hayo?