Tuseme ukweli: Huwezi kuwa na Uhuru kama wewe ni mtegemezi. Watanzania sasa tuko Huru zaidi kwani sasa tunajitegemea

Tuseme ukweli: Huwezi kuwa na Uhuru kama wewe ni mtegemezi. Watanzania sasa tuko Huru zaidi kwani sasa tunajitegemea

Tumeweka udhibiti wa kisheria wa upashanaji wa habari unaozingatia professionalism ya taaluma ya habari. Tumepiga marufuku kwa makajanja wa taaluma hii. Haiwezekani wananchi wetu wawe wanalishwa taarifa za habari za uongo, za matusi, zisizokuwa balanced, za uchochezi, zinazodhalilisha utu na heshima ya wenzako nk. Uhuru wako unaishia pale pua yangu inapoanzia: hii ndiyo principle ya uhuru po pote duniani. Kuna limit ya uhuru wa mtu kwa mtu, na limit hiyo ni pale pua ya mwenzako inapoanzia.
Naunga mkono hoja

P
 
Katika kipindi hiki ambacho enzi za Anna Makinda, Tundu Lissu alikiita 'silly season' tutasikia uwongo na upotoshaji mwingi.

Tunaambiwa eti Tanzania kwa sasa hakuna Uhuru. Yaani sasa hivi Watanzania hatuko huru.

Ukweli ni kwamba mtu au nchi haiwezi kuwa huru kama mtu au nchi hiyo ni mtegemezi. Kwa mfano mtoto kama mahitaji yake mengi anategemea kuyapata kwa wazazi wake basi na uhuru wake unategemea matakwa ya hao wazazi wake. Hawezi kwenda disco kama wazazi wake hawapendi. Hawezi kurudi nyumbani saa sita usiku bila ruhusa ya wazazi wake. Na kadhalika.

Hivyo hivyo kwa nchi. Kama mahitaji ya nchi hasa yale ya msingi yanategemewa kupatikana kutoka nchi nyingine, tulikuwa tunaziita nchi hisani basi uhuru wa nchi hiyo utategemea matakwa ya hizo nchi hisani.

Ukweli ni kuwa nchi yetu kwa sasa si nchi tegemezi tena. Nchi yetu sasa inajitegemea kwa mahitaji yake yote. Hatutegemei nchi hisani. Hatutembezi bakuli la kuomba omba msaada kwa nchi yo yote. Na huko tulikokuwa tunaenda kuombaomba rais wetu kwa kipindi cha miaka mitano hajaenda hata kuwasalimia.

Nchi yetu inajitegemea kwani ni tajiri. Hivyo uhuru wetu wa kuamua mambo yetu umepaa sana. Hatuogopi nchi ye yote katika maamuzi yetu maana tunajitegemea. Wawekezaji kutoka nchi zingine ambao hatutapata angalao 50:50 win-win situation hawana nafasi hapa. Tumewatungia sheria ya natural resources. Wanune wasinune shauri yao.

Ushoga tumewaambia wazi kwamba hapa kwetu hatuutaki. Tumeutungia sheria. Wanune wasinune shauri yao. Wamkataze Makonda kukanyaga nchini kwao shauri yao.

Tumeweka udhibiti wa kisheria wa upashanaji wa habari unaozingatia professionalim ya taaluma ya habari. Tumepiga marufuku kwa makajanja wa taaluma hii. Haiwezekani wananchi wetu wawe wanalishwa taarifa za habari za uongo, za matusi, zisizokuwa balanced, za uchochezi, zinazodhalilisha utu na heshima ya wenzako nk. Uhuru wako unaishia pale pua yangu inapoanzia: hii ndiyo principle ya uhuru po pote duniani. Kuna limit ya uhuru wa mtu kwa mtu, na limit hiyo ni pale pua ya mwenzako inapoanzia.

Tutofautishe kukopa kwenye mabenki ya ndani au ya kimataifa. Mikopo siyo hisani. Mikopo ya mabenki ni biashara ya haya mabenki na yako hapo kwa ajili ya biashara hiyo: kukopesha kwa interest. Huwezi kukopa kama wewe ni fukara kwani hutaweza kurejesha huo mkopo. Wanaokopa benki ni matajiri. Amerika ndiyo inaongoza duniani kuwa na madeni makubwa ya mikopo ya mabenki. Na ukikopa hiyo hela uliyokopa inakuwa ni pesa yako ya ndani. Ni tahira tu atakayekuambia eti pesa yenyewe unayoringia ni ya mkopo. Si na yeye akakope kama anaweza, masikini hakopesheki.

Ukweli sisi tunajitegemea. Mapato ya TRA pekee yake yameweza kupanda toka wasitani wa Tsh 800 billion mwaka 2015 kwa mwezi hadi Tsh 1.5 trillion mwaka 2019 na matarajio ni kuwa Tsh 2 trillion kwa mwezi ifikapo 2021. Mapato yasiyotokana na kodi nayo yamepanda hadi kufikia Tsh trillion zisizopungua moja kila mwezi. Matumizi yasiyo ya lazima tumeyapunguza hadi kufika 0%. Hivyo hatutegemei hisani kutoka kwa ye yote. Tuko huru kabisa. Tunatunga sheria tunazozitaka wenyewe bila kuingiliwa na nchi au mtu ye yote.
Jalala walilokuokata siyo mchezo, maana uvundo ulioandika afadhali ya Prof aliyeokotwa jalala la UDSM!
 
Pole kwa kazi ngumu ya kumpigia mbuzi gitaa.
Mnatumia nguvu nyingi sana.

CCM imepoteza Uhalali wa kuongoza Taifa.
kuna ukweli fulani. baada ya ujenzi wa flyovers, mabwawa, SGR na ukuta merelani CCM ingepaswa isiwe na haja tena ya kupiga kampeni mwaka huu. Lakini hali ni tofauti kabisa, wamepigia mbuzi gitaa. Watu hawapendi CCM hata kama ungewachambisha na maji ya karafuu na iliki.

Ndio maana matumizi ya Tume hayaepukiki.
 
Hiyo simu unayotumia kuandika upupu imetengenezwa bongo. ARV unazotumia,viatu ulivyovaa,magari,soko la mazao yetu eg korosho, hizo treni za umeme zinaundwa kigoma, hata hizo ndege tunatengeneza pale Mtwara, ukiweza kumiliki technology wewe ndio uko huru,beberu akikuwekea vikwazo mwaka tu utajiona uko jehanamu, utakula hizo korosho mpaka uvimbiwe huna kazi nazo.
Hao wanaotengeneza magari, treni, ndege na simu wanazitengeneza kwa ajili ya kuuza na wanunuzi wazuri ni sisi kwani tunawalipa cash money. Hawazitengenezi kwa ajili ya kuzila. Wanatutegemea sisi tuzinunue. Hivyo wao ndiyo wategemezi. Halafu hizo malighafi ya kuzitengeneza hizo bidhaa zao wanategemea kuzipata kwetu. Hapo nyuma walikuwa wanazichukua bure na kutuletea tu misaada kiduchu twenye masharti kibao. Leo wanalazimika kuzipata kwa win-win formula ambayo sisi tunapata zaidi ya 80% ya thamani ya mali hiyo.

Hivyo hao mabeberu tumewageuza kuwa wategemezi. Yaani wanatutegemea sisi. JPM kaonesha mfano. Nchi nyingine za Afrika na Asia ziko mbioni kufuata nyayo. Mabeberu wataipata enzi hii. Wametuletea kibaraka wao kutaka kutuvuruga. Hawataweza hata kidogo. Kibaraka huyo tutamfundisha adabu tarehe 28 Oct 2020. Stay tuned my frend!
 
Jalala walilokuokata siyo mchezo, maana uvundo ulioandika afadhali ya Prof aliyeokotwa jalala la UDSM!
This thread was not meant for those with small brains (anacephally) like you. So you better just keep quiet.
 
Wafanyakazi ( walimu, wajeda ,watumishi mbali mbali), waliofukuzwa kazi, mama ntilie, boda boda, wamachinga, waliokosa ajira na wanyonge wote hao wanawachora tu. Ila yaliyopo moyoni ni kwenye sanduku la kura , pale meza itakopogeuzwa juu chini.

Tuendelee kupiga kampeni ,. Mwaka huu mtapigwa chini kimya kimya.
 
Hao wanaotengeneza magari, treni, ndege na simu wanazitengeneza kwa ajili ya kuuza na wanunuzi wazuri ni sisi kwani tunawalipa cash money. Hawazitengenezi kwa ajili ya kuzila. Wanatutegemea sisi tuzinunue. Hivyo wao ndiyo wategemezi. Halafu hizo malighafi ya kuzitengeneza hizo bidhaa zao wanategemea kuzipata kwetu. Hapo nyuma walikuwa wanazichukua bure na kutuletea tu misaada kiduchu twenye masharti kibao. Leo wanalazimika kuzipata kwa win-win formula ambayo sisi tunapata zaidi ya 80% ya thamani ya mali hiyo.

Hivyo hao mabeberu tumewageuza kuwa wategemezi. Yaani wanatutegemea sisi. JPM kaonesha mfano. Nchi nyingine za Afrika na Asia ziko mbioni kufuata nyayo. Mabeberu wataipata enzi hii. Wametuletea kibaraka wao kutaka kutuvuruga. Hawataweza hata kidogo. Kibaraka huyo tutamfundisha adabu tarehe 28 Oct 2020. Stay tuned my frend!
Unaongea bila mantiki huwezi shindana na mzungu dogo .kale ulale ukue
 
Unajitegemea kwenye nini wewe. Unajua maana ya busker finds kwenye idara ya afya? Embu nenda kwa Dmo wa wilaya ulipo muulize ndani ana fund budget ya dawa na vifaa Tiba hapa nchini?
Unadhan kujitegemea ni kupigwa push ups
Wewe unaongelea historia. Mambo ya sijui basket funding yalikuwa enzi hizo tulipokuwa wategemezi wa nchi hisani. Sasa hivi tumeongeza bajeti ya dawa kwenye vituo tiba vyetu zaidi ya mara kumi ukilinganisha na mwaka 2015. Na fedha hizi zinapelekwa kwa wakati kila mwezi. Hakuna tena uhaba wa dawa na vifaa tiba. Tumeboresha huduma za tiba hadi hatupeleki tena wagonjwa India kwa ajili ya heart operations, renal transplants, joint replacement, brain tumor operations, retinal surgery etc kwani huduma hizi sasa zinapatikana hapa hapa nchini kwetu. Sasa hivi nchi nyingi za nje hasa za Afrika zinaleta wagonjwa wao kwetu kwa ajili ya tiba hizo badala ya kuwapeleka India kwani gharama zetu ni nafuu kuliko za India. Tunaingiza fedha za kigeni kwa huduma hizo.
 
Wafanyakazi ( walimu, wajeda ,watumishi mbali mbali), waliofukuzwa kazi, mama ntilie, boda boda, wamachinga, waliokosa ajira na wanyonge wote hao wanawachora tu. Ila yaliyopo moyoni ni kwenye sanduku la kura , pale meza itakopogeuzwa juu chini.

Tuendelee kupiga kampeni ,. Mwaka huu mtapigwa chini kimya kimya.
Aliyepata kuwa tishio ni Lowassa tu. Hatatokea mwingine. Ona walivyoanza kuvurugana wenyewe: Lissu vs Membe. Baadhi ya wagombea ubunge waliokuwa wameshateuliwa na Tume, tayari wameshaanza kujitoa kwenye kampeni kwa sababu ya kutopata support na kunyanyaswa na viongozi wao wakuu. Sasa kipi tutegemee?
 
Hiyo simu unayotumia kuandika upupu imetengenezwa bongo.
Mwaka 2015, Vifaa vya kieletronik zaidi ya asilimia 70 vilivyokuwa vinatumika na vingine vikiwa madukani nchini Ujerumani vilikuwa vimetengezwa China na Korea Kusini.

Sasa tujiulize, nani amejaza upupu kichwani mpaka sasa!
 
Mwaka 2015, Vifaa vya kieletronik zaidi ya asilimia 70 nchini Ujerumani vilikuwa vimetengezwa China na Korea Kusini.

Sasa tujiulize, nani amejaza upupu kichwani mpaka sasa!
China ni bongo.tatizo mnadhani beberu ni mzungu tu hata mchina ni beberu
 
Hata sisi tunaweza kuwa beberu. Au hujui maana ya ubeberu?
Ubeberu una stage zake sio kwamba unaamua tu,unaoitia ubepari kwanza ,capitalism ndio uje kuwa imperialist.kwa akili za watanzania ni process ya miaka 599
 
Waulize Libya,beberu hawezi kubali umpite atakufanyia figisu zote utanyoosha mikono tu
Huwezi kutulinganisha sisi na hao waarabu wa Libya. Ulikuwa hujazaliwa tulipo waangamiza hao walibya katika vita ile ya nduli Iddi Amini Dada huko Uganda?

Sisi si wa mchezo. Na tayari hao mabeberu wako wameshaanza kunyoosha mikono. Hukumbuki jinsi wa akina Mkwawa huko Iringa na akina Kiyungi huko Tabora walivyowachachafya hao mabeberu wako enzi zile? Sasa tuna wakina Mkwawa na Kiyungi wapya wako madarakani. Wembe ni ule ule.
 
Ubeberu una stage zake sio kwamba unaamua tu,unaoitia ubepari kwanza ,capitalism ndio uje kuwa imperialist.kwa akili za watanzania ni process ya miaka 599
Hujui. Nitatafuta siku nikuelimishe maana ya neno ubeberu.
 
Back
Top Bottom