Tuseme ukweli! Jaribio la treni ya SGR lilishindwa kufikia lengo

Hawa ndio chadema bana ,kila kitu wanajua
 
Treni la mbio, kwenye trial hawajaribu mbio zenyewe?? Note: walifanya trial mwanzo madereva walikua washatest test vitu
 
Sidhani kama kuna haja ya kuhangaika na vichwa vya treni za kisasa zaidi ambavyo vinaendana na model ya mabehewa, na labda bei, gharama za uendeshaji na maintainance ni kubwa sana.
Muhimu kuzingatia ni ubora wa vichwa na mabehewa kutimiza malengo ya hizo safari hata kwa huo muda wa saa moja na nusu, siyo mbaya.​
 
Naona ununuzi wa vichwa vya Treni haukuzingatia ushauri wa kitaalamu , bali umefuata utashi au ushauri wa wanasiasa
 
Kwani hili ni jaribio la kwanza?
 
Nimeona pia huko twitter (X) wanazungumzia mazingira yetu, wanadai nature ya mazingira yetu inaifanya treni isiende kwa spidi inayotakiwa, wanadai uwepo wa vitu kama mifugo kwenye njia za treni unasababisha kupunguza mwendo, hii nayo nimeona kwa namna fulani inaleta maana.

Ingebidi basi hiyo njia ya treni iwekewe uzio ili kuwazuia watu na mifugo wasiingie kwenye njia, ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kujitokeza kama treni ya umeme itakuwa na mwendo mkali, sijui nchi ya jirani kama Kenya wao wamefanyaje kwao nadhani nao wanatumia treni ya umeme ...

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
sasa mtu huna ujuzi wa safari za treni za umeme unapata wapi ujasiri wa kukosoa?
 
Ndiyo maana hawakuliwasha mapema walijua wamepiga cha juu lpkama ile feri ya Bagamoyo inayofanana na nyambizi
 
Wasijitetee
Reli nzima imepigwa fensi pande zote mbili, mifugo gani wanaizungumzia
 
Si muendelee na Biashara yenu ya mabasi...kwa nini mnatunyanyasa hivi!!!
 
Lengo la jaribio lilikuwa ni lipi? Ni vema tukajua scope ya majaribio, na mengine yanayokuja kabla ya kulaumu
TRC wao wenyewe walisema malengo ya majaribio yalikuwa ni haya:
1. Kuashiria kukamilika kwa miundo mbinu yote (Reli, vichwa vya treni, mabehewa) ya SGR kipande cha Dar-Moro.

2. Kuwaonyesha watanzania namna TRC ilivyojipanga vyema kuanza kutoa huduma za usafirishaji kwa kutumia treni ya SGR.

3. Kujionea, kufurahia na kuutangaza mradi wa SGR kama sehemu ya mapinduzi ya kisasa (kasi, usalama na uhakika) katika usafirishaji wa watu na mizigo.

Sasa mategemeo ya watanzania yakawa tofauti na kile walichokipata katika majaribio.
 
I say it is too soon, lets say tuone with time kama watafikia matarajio ya watanzania
 
Mkuu jaribio la jana halikuwa jaribio la kiufundi bali lilikuwa ni jaribio la matumizi kwa wateja. Hayo ya kuogopa mwendo mkali au upya wa reli hayana mantiki. Lengo la ujenzi wa SGR ni kwenda kasi zaidi, sasa unapoita wateja waje kwenye majaribio ya SGR halafu treni itembee mwendo mdogo maana yake hujui unachokifanya.
 
I say it is too soon, lets say tuone with time kama watafikia matarajio ya watanzania
It is a right time to say now ili waende wakarekebishe haraka. Maana baada ya jaribio bovu jana, TRC na chawa wa serikali walikuwa busy kusifikia na kushangilia kila kitu wakati kiuhalisia ilikuwa ni huge failure.
 
Tuwape muda
Tuwape muda upi tena?
TRC wameshasema mradi uko tayari, majaribio yamefanikiwa kwa 100%+, na watanzania wamefurahia mwendo mdogo mdogo na kuelewa sababu za kukatika umeme safarini haziepukiki, zina athari fulani lakini zina nia njema!
 
Majaribio ni muhimu kabla ya kuanza matumizi rasmi ya mitambo na miundo mbinu.
Kwa akili ya kawaida, majaribio huanza pole pole, kwa tahadhari ili kuona kama kuna sehemu zinazohitaji marekebisho, huku kasi na mzigo ukiongezwa kwa viwango hadi kufikia kile kilichokusudiwa.
Kilichotakiwa ni kufanya majaribio kimya kimya hadi siku ya ufunguzi rasmi ndipo matangazo yafanyike. Lakini kwa sababu ya siasa za kutafuta sifa, utaalamu hufunikwa na ujinga.
Siasa zinafanya jamii na taifa kuwa na fikra na mijadala ya kijuha.
 

Hiv kile kichwa na zile behewa ndio tren; Ila TZ bhana wanapotezaga hela sana kwenye vitu takataka.that train. Ni UCHAFU kwa sis tunaojua tren za Umeme. Nimeanza kupanda na kujua tren za umeme way back

MKURUGENZI wa TRC na SSH na Gavana wote wanatakiwa kwenda Gerezani kwa matumiz mabaya ya kodi full stop
 

Hivi ni kitu gani kilisimamiwa na Serikali, halafu kikawa na ufanisi?

Simu walishindwa. Bia walishindwa. Viwanda vya aina mbalimbali walishindwa. Usafiri wa anga walishindwa, na ili ATCL iendelee waliamu kuifukuza Fastjet ili ATCL isiwe na mshindani.

Kama wameshindwa kila kitu, ndiyo waweze kuiendesha reli? Reli ni muhimu sana, lakini chini ya Serikali hii ya kwetu, mradi huu mkubwa wa reli nao utaishia ilikoishia miradi mingine.
 
Hakuna mradi mkubwa unafanyika duniani na kuanza shughuli 100% bila kuwa na matatizo yanayo rekebishika. Wapeni TRC muda wafanye kazi yao kikamilifu. Haya ni majaribio na lazima yaende kwa stages.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…