Tuseme ukweli! Jaribio la treni ya SGR lilishindwa kufikia lengo

Tuseme ukweli! Jaribio la treni ya SGR lilishindwa kufikia lengo

Lengo la majaribio inawezekana ilikuwa ni kuhakikisha tu kama treni itafika Morogoro, kama hivyo ndivyo basi wamefanikiwa.

Hayo mambo ya mwendo labda wanaweza kuyarekebisha mbele ya safari, kama itawezekana kufanya hivyo kwa kutumia vichwa vya mabehewa vilivyopo.

Lakini binafsi nina mashaka na vile vichwa vya treni, sidhani kama vina ubora stahiki ili kufikia malengo ya muda wa safari uliowekwa.

Nahisi vitakuwa vya bei rahisi, tofauti na vile tunavyoona vikiendesha treni za mwendokasi kwenye nchi nyingine kama China.

If this is the case, naishauri serikali ijipange kwa kununua vichwa vyenye ubora stahiki, hata kwa kuanza na kimoja, ili kuhakikisha lengo kusudiwa la mwendokasi linafikiwa.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Hivi vichwa vya treni ni kama vinavyotumika SA..tu vya kizamani sana SA wanavitumia kama mbadala wa daladala mijini kupumguza msongamano wa magari..lakini kwa masafa marefu havifai havina spidi
 
Hivi ni kitu gani kilisimamiwa na Serikali, halafu kikawa na ufanisi?

Simu walishindwa. Bia walishindwa. Viwanda vya aina mbalimbali walishindwa. Usafiri wa anga walishindwa, na ili ATCL iendelee waliamu kuifukuza Fastjet ili ATCL isiwe na mshindani.

Kama wameshindwa kila kitu, ndiyo waweze kuiendesha reli? Reli ni muhimu sana, lakini chini ya Serikali hii ya kwetu, mradi huu mkubwa wa reli nao utaishia ilikoishia miradi mingine.
Shida ni kwamba wameshindwa kununua treni za kisasa kenge hawa..sidhani kama hii ni vision aliyokuwa nayo marehemu magufuli.
 
Kuna watu wao kujidai ni wataalamu kila mahali kumbe wamejawa na chuki na husda na visasi. Hivi kwa akili ya kawaida ulitegemea ufanye majaribio kwenye reli mpya halafu utembee na speed kali?. Na huko kukatika kwa umeme si ndio majaribio yenyewe ya kupina ni vipi treni itabehave ikiwa umeme umekatika au huelewi neno majaribio.
 
3. Waje kufanya jaribio lingine baada ya kupata utatuzi wa mapungufu yote.
Akili kichwani mtu wangu. Mabasi yapo ya maana sana siku hizi!
Majaribio hata wafanye mara 100 hawatoboi! Upigaji ni mwingi sana kwenye SGR project.

NB:
1. Walificha lakini zile ni hybrid trains - diesel na umeme. Spidi haiwezi kuwa kubwa!
2. Kushindwa kufikia maximum speed kwenye majaribio ni ishara kwamba mengi hayapo sawa kwenye SGR!
 
Huyu jamaa sijui kama ana ufundi wowote ule huwezi sema treni iwekwe tu kwenye reli ianze kwenda mwendo mkubwa kiasi hicho ila ujue reli ni mpya treni ni mpya ina takiwa kwenda mwendo wa kawaida huku mafundi wakifuarilia kila hatua injini mabehewa umeme nk halafu safari 2 ,3,4 ndo itakuwa mwendo mdundo
Mleta mada anadhani treni ni baiskeli, hivi kweli unaweza kuambiwa endesha hili gari ujaribu kama breki zinashika vizuri, wewe ukaanza na speed ya 80
 
Siku ya jana, tarehe 26/2/2024, shirika la reli hapa Tanzania (TRC) lilifanya jaribio la kwanza la treni ya kisasa, umeme na mwendokasi (SGR), na miongoni ya malengo (matarajio ya watu?) ya msingi yalikuwa ni haya;

1. Mwendokasi (muda wa kusafiri uwe mchache huku umbali uwe mrefu).

2. Nishati ya Umeme (uhakika wa umeme wakati wote)

Bila kumumunya maneno, malengo yote mawili hayakufikiwa. Treni haikuwa na kasi ya kutosha, safari ikatumia muda mrefu zaidi kutoka Dar mpaka Moro. Lakini mara mbili umeme ulikatika katikati ya safari, treni ikapunguza mwendo na huduma ya umeme ndani ya mabehewa ikapotea.

Kwa wale wasiofahamu kuhusu Sayansi ya majaribu (practical trial/ testing ama Pilot survey) ni kuwa, ili malengo yanayotegemewa kuwepo katika uhalisia yaweze kuonekana kwelikweli inabidi majaribu yafikie malengo na kupitiliza walau robo zaidi ya lengo (yaani yafikie 125%). Kwa mfano kama Treni ya SGR inategemewa kutoka Dar-Moro kwa dakika 75 tu basi wakati wa majaribio walau itumie dakika zisizozidi dakika 57.

USHAURI.
TRC inabidi ifanye mambo haya matatu kwa sasa;

1. Itoe taarifa kamili ya kitaalamu kuonyesha taswira nzima ya hilo jaribio, wapi walifikia lengo na wapi walishindwa kufikia lengo.

2. Wakae chini kujipanga upya namna ya kuweza kukabiliana na mapungufu hayo.

3. Waje kufanya jaribio lingine baada ya kupata utatuzi wa mapungufu yote.


"Kwa mfano kama Treni ya SGR inategemewa kutoka Dar-Moro kwa dakika 75 tu basi wakati wa majaribio walau itumie dakika zisizozidi dakika 57"

Hata kama huwapendi ccm basi usionyeshe wazi wazi
 
Wakuu kwani lengo la kufanya Jaribio ni nini?, kwa sababu navyofahamu mimi lengo kuu la Jaribio ni kupima ufanisi kwa sababu mfanya Jaribio hana uhakika na ufanisi uliokusudiwa na kama Jaribio limeonyesha kuwa hakuna ufanisi tarajiwa basi Jaribio limefaulu kwa asilimia mia, na hivyo limewapa fursa wafanya Jaribio kurudi Kwenye planning phase ili kung'amua ni kwanini ufanisi haukufikiwa na kufanya marekebisho hitajika. Hivyo mimi sioni tatizo lolote Lile na ninawapa kongole wafanya Jaribio kwa kufanya Jaribio kabla ya safari kuanza na Tena nawapa moyo wa kuendelea kufanya majaribio kadhaa hata kwa muongo mmoja mpaka ufanisi upatikane.
 
Shida ni kwamba wameshindwa kununua treni za kisasa kenge hawa..sidhani kama hii ni vision aliyokuwa nayo marehemu magufuli.
walibadilisha supplier na kuongeza sifuri mbele ili wapige hela kisha wakanunua refurb na bi mkora alikazia kuwa mtumba huo ni kama mpya tu. For the first time naskia serikali inanunua mtumba na kujisifia😂
 
Nimeona pia huko twitter (X) wanazungumzia mazingira yetu, wanadai nature ya mazingira yetu inaifanya treni isiende kwa spidi inayotakiwa, wanadai uwepo wa vitu kama mifugo kwenye njia za treni unasababisha kupunguza mwendo, hii nayo nimeona kwa namna fulani inaleta maana.

Ingebidi basi hiyo njia ya treni iwekewe uzio ili kuwazuia watu na mifugo wasiingie kwenye njia, ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kujitokeza kama treni ya umeme itakuwa na mwendo mkali, sijui nchi ya jirani kama Kenya wao wamefanyaje kwao nadhani nao wanatumia treni ya umeme ...

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Nyang'au wao hawana treni ya umeme, ya kwao inatumia dizeli........hii ya kwetu ndo ya kwanza East Africa, jambo hili litakuwa linawauma sana nyang'au kwa jinsi wanavyopenda kujilinganisha na Tanzania.
 
Nyang'au wao hawana treni ya umeme, ya kwao inatumia dizeli........hii ya kwetu ndo ya kwanza East Africa, jambo hili litakuwa linawauma sana nyang'au kwa jinsi wanavyopenda kujilinganisha na Tanzania.
SI wanayo tiari
 
Back
Top Bottom