Simba itafute Mtaalam wa Saikolojia ili awasaidie wachezaji wake. Walivyocheza na Mbabane Swallows, Nkana na hata walivyocheza na Soura wachezaji walikuwa na hamasa kubwa ya kujituma uwanjani. Tofauti na walivyocheza na AS Vita au Al-Ahly walikosa hali ya kujituma, Wanakabia macho, wakinyang'anywa mpira wala hawajisumbui kuutafuta, wakifungwa wanacheka na kutabasamu tu wala hawaumizwi na vichapo, mabeki hawarukii mipira ya kona au Cross utazani wamepewa posho na Timu pinzani. Timu hata ikizidiwa uwezo basi waonyeshe hali ya kupambana. Vichapo vya Hamsa vinavunja moyo kwa kweli