Wakuu Juni ndo hiyo inakaribia kukata tayari tumemaliza miezi sita ya mwanzo! Muda hautusubiri na umri unasonga. Huu ndio wakati muafaka wa kusimama na kujitathmini.
Jikague Haraka:
- Zile ahadi za Januari zipo hatua gani?
- Kuna tabia zozote zinazokurudisha nyuma?
- Ufanye nini tofauti ili kutusua miezi 6 iliyobaki?
Mambo ya Kufanya Sasa:Usitupe taulo. Kama mambo magumu, badili mbinu badala ya kubadili lengo. Fanyia kazi udhaifu wako, tafuta maarifa (mtandaoni au kwa washauri), na jipongeze kwa hatua ndogo unazopiga.