Tushirikishane hapa kero au tabia zinazokera za wenza wetu na changamoto zake

Tushirikishane hapa kero au tabia zinazokera za wenza wetu na changamoto zake

Mchanya

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
1,062
Reaction score
1,713
Ulishawahi kuwa na mwenza (mpenzi/rafiki/mwanandoa) mwenye tabia yenye kukera lakini hata jinsi ya kumuambia unajiuliza mara mbilimbili utamuambiaje na ataipokeaje? Ana tabia ambayo, kwa kujua bila kujua inakera sio tu kwangu mimi binafsi bali hata watu wengine.

Kwasababu ya upendo na kuwafanya wenza wetu wawe watu bora zaidi, ni lazima na wajibu wetu tuwaambie wenza wetu hata kama watakasirika maana tukichelea kuwambia, aibu watakayoipata ni aibu yetu pia.

Mifano michache ni pamoja na kikwapa (harufu kali ya asili ya mwili) au kuingiza vidole puani, masikioni na kisha kuendelea kutumia mikono kama kawaida, kula, kusalimia n,k
Unamuambiaje mtu mwenye tabia kama hizo?.
Hebu nawe ongeza na kwako hapa
 
Mi nina rafiki zangu niliwakuta mkoani basi nikawaelekeza walikua kama watatu.wawili wamebadirika lakin kuna mmoja huyu sugu na ni mtu mzima tu mpka basi akivaa gauni siku 5 mfulizo..jamani nimechamba mie nimumelekeza na anaweka vidole puani nimefundisha lakin wapi..sasa sijui nitumie njia gani....Mmmh wanaume kazi mnayo..nae baby wa mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom