Tusichoke kukumbushana kwani kukumbushana kuna faida: Hatujachelewa kuiweka sawa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
HATUJACHELEWA KUIWEKA SAWA HISTORIA YA TANU NA UHURU WA TANGANYIKA

Hiyo picha hapo chini ni 1955/56 Dodoma Railway Station kushoto ni Iddi Faiz Mafungo, Sheikh Mohamed Ramiya, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu.

Ningefarajika sana kaka picha hii ingewekwa Makao Makuu ya CCM Dodoma kwa ukumbusho wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ukimtoa Mwalimu Nyerere katika picha hiyo kuna yeyote anaeweza kueleza mchango wa wazalendo hawa wengine katika kupigania uhuru wa Tanganyika?

Iddi Faizi Mafungo alikuwa Mwekahazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na pia Mwekahazina wa TANU.

Yeye ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kukusanya fedha za safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere UNO 1955.

Iddi Faizi na Sheikh Mohamed Ramia ni ndugu na ndiye aliyempeleka Mwalimu Bagamoyo kwa Sheikh Ramia akiongozana na Iddi Tosiri.

Wote hawa watatu ni ndugu wote hawa Wamanyema wazee wao wakitokea Belgian Congo katika miaka ya 1800 na walikuwa na chama chao cha Wamanyema - Batetera Union.

Ukitokea msiba walikuwa na ngoma wanapiga na ukisikika mlio wa ngoma ile wanajua kuna msiba.

Walipoamua kuunda TANU na kujenga taifa la Tanganyika yote haya yakaisha.

Historia ya Iddi Faizi jinsi alivyoandamwa na Special Branch wakati wa safari ya Mwalimu UNO siku anakusanya fedha za TANU ni senema ambayo anaeweza kuiongoza ni Steven Spielberg au Oliver Stone.

Haendi mtu msalani.

Sheikh Ramiya alisoma Maulid wakati wa kipindupindu Bagamoyo polisi wakenda nyumbani kwake kumleta kituo cha polisi kumhoji.

Habari zikaenea Khalifa wa Tarika Quadiriyya kakamatwa.

Haukupita muda Bagamoyo nzima na pembezoni na hii ikasababisha kituo cha polisi kuzungukwa na murid kila upande wamekuja kumtoa kiongozi wao.

Wachache katika askari wa pale kituoni waliojua kwa nini ghafla Bagamoyo nzima ikawa kama vile imehamia kituo cha polisi.

Murid wengine wametoka mashamba wamekuja Bagamoyo mjini kwa baiskeli wengi wao ni wakwezi na askari walitishika kuwaona wana visu kiunoni.

Saadan Abdul Kandoro amekufa hawezi kulipa ankara za umeme wala maji ya nyumba yake Magomeni Mikumi.

Yeye ndiye aliyeunda TANU Kanda ya Ziwa na ni mmoja kati ya waasisi 17 wa TANU 1954.
Haruna Taratibu ndiye aliyeasisi TANU Central Province 1955 pamoja na Omari Suleiman.

Inahitaji kuandika kitabu kizima kuieleza historia ya wazalendo hawa.

PICHA:
Aliyesimama mbele ya sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni Abdallah Saiwaad Mhariri Bingwa wa miswada ya vitabu.
IDD FAIZ MAFUNGO.JPG
ABDALLAH SAIWAAD.jpeg
 
Asante mkuu nimeongeza kitu leo. Tena buree kabisa🙏
 
Wahenga kumbe bado mpo....!!
Jaribuni kuiweka sawa historian yetu jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
Kamkuki,
Historia hii huijui kwa umri.

Kama ni umri wakati naandika kitabu cha Abdul Sykes 1980s walikuwapo watu wazima wengi ndani ya CCM lakini hawaijui.

Historia hii mimi nimeijua kwa kuelezwa na wazee wangu ambao ndiyo waliunda TAA na TANU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HATUJACHELEWA KUIWEKA SAWA HISTORIA YA TANU NA UHURU WA TANGANYIKA

Hiyo picha hapo chini ni 1955/56 Dodoma Railway Station kushoto ni Iddi Faiz Mafungo, Sheikh Mohamed Ramiya, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu.

Ningefarajika sana kaka picha hii ingewekwa Makao Makuu ya CCM Dodoma kwa ukumbusho wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ukimtoa Mwalimu Nyerere katika picha hiyo kuna yeyote anaeweza kueleza mchango wa wazalendo hawa wengine katika kupigania uhuru wa Tanganyika?

Iddi Faizi Mafungo alikuwa Mwekahazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na pia Mwekahazina wa TANU.

Yeye ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kukusanya fedha za safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere UNO 1955.

Iddi Faizi na Sheikh Mohamed Ramia ni ndugu na ndiye aliyempeleka Mwalimu Bagamoyo kwa Sheikh Ramia akiongozana na Iddi Tosiri.

Wote hawa watatu ni ndugu wote hawa Wamanyema wazee wao wakitokea Belgian Congo katika miaka ya 1800 na walikuwa na chama chao cha Wamanyema Batetera Union.

Ukitokea msiba walikuwa na ngoma wanapiga na ukisikika mlio wa ngoma ile wanajua kuna msiba.

Walipoamua kuunda TANU na kujenga taifa la Tanganyika yote haya yakaisha.

Historia ya Iddi Faizi jinsi alivyoandamwa na Special Branch wakati wa safari ya Mwalimu UNO siku anakusanya fedha za TANU ni senema ambayo anaeweza kuiongoza ni Steven Spielberg au Oliver Stone.

Haendi mtu msalani.

Sheikh Ramiya alisoma Maulid wakati wa kipindupindu Bagamoyo polisi wakenda nyumbani kwake kumleta kituo cha polisi kumhoji.

Habari zikaenea Khalifa wa Tarika Quadiriyya kakamatwa.

Haukupita muda Bagamoyo nzima na pembezoni na hii ikasababisha kituo cha polisi kuzungukwa na murid kila upande wamekuja kumtoa kiongozi wao.

Wachache katika askari wa pale kituoni waliojua kwa nini ghafla Bagamoyo nzima ikawa kama vile imehamia kituo cha polisi.

Murid wengine wametoka mashamba wamekuja Bagamoyo mjini kwa baiskeli wengi wao ni wakwezi na askari walitishika kuwaona wana visu kiunoni.

Saadan Abdul Kandoro amekufa hawezi kulipa ankara za umeme wala maji ya nyumba yake Magomeni Mikumi. Yeye ndiye aliyeunda TANU Kanda ya Ziwa na ni mmoja kati ya waasisi 17 wa TANU 1954.

Haruna Taratibu ndiye aliyeasisi TANU Central Province 1955 pamoja na Omari Suleiman.

Inahitaji kuandika kitabu kizima kuieleza historia ya wazalendo hawa.

PICHA:
Aliyesimama mbele ya sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni Abdallah Saiwaad Mhariri Bingwa wa miswada ya vitabu.
View attachment 1369543View attachment 1369550
Soma, Diwani ya Saadan Abdul kandoro, humo utakuta wameandikiana mashairi kati yake na Shk Amri Abeid.
Huyo ni baba'ke Kamanda Mohamed Chico au nduguye?

Umenikumbusha Da Saida "Sewadi" wa mtaa wa Chui na Mzee Sewadi wa mtaa wa Mafia,Kariakoo, muuza barafu za mapande, tangu sisi wadogo tukienda dukani kwake anatupa chega chenga mbili tatu za barafu na warning juu "zinaumiza kifua hizo, nisiwaone tena hapa". Allah awarehemu wazee wetu.
 
Maalim,
Huyu Abdallah na Chico ni baba mkubwa na mdogo.

Baba zao ni ndugu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kesho mkienda mnapewa tna hakika tulikuwa tunaishi kwa upendo Mkubwa...
Huyo ni baba'ke Kamanda Mohamed Chico au nduguye?

Umenikumbusha Da Saida "Sewadi" wa mtaa wa Chui na Mzee Sewadi wa mtaa wa Mafia,Kariakoo, muuza barafu za mapande, tangu sisi wadogo tukienda dukani kwake anatupa chega chenga mbili tatu za barafu na warning juu "zinaumiza kifua hizo, nisiwaone tena hapa". Allah awarehemu wazee wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANU ilikuwa na wanachama wengi mno walioipigania wengine walikua mikoani, wilayani wengi sana kuwataja wote haiwezekani, ndio maana wanazuoni wa chuo cha kivukoni wakamzungumzia nyerere tu kuwakilisha harakati za TANU, wote wakitaka watambulike ingeleta vurumai
 
Sl

Sent using Jamii Forums mobile app
Laki...
Wote wanataka kutambulika hii fikra kuwa kulikuwa na watu walitaka kutambulika wewe umeitoa wapi?

Watake kutambulika kwa kufanya nini?

Huenda wewe hujui yaliyopitika baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961.

Sijapata kusikia au kusoma popote kuwa katika waasisi wa TANU wako waliotaka kutambulika.

Mimi nililiona tatizo la historia ya TANU mwaka wa 1981 katika kitabu cha Chuo Cha CCM Kivukoni.

Historia ile waliyoandika haikuwa historia ya TANU niijuavyo mimi ndipo nikaandika hii historia mnayoisoma hivi sasa hapa barzani.

Ninachokiona kwenu ni nyinyi kutaabika na historia hii ya kweli kwa akili zenu kukataa kuamini ukweli wa mambo mkatamani kubakia na ile historia iliyowafuta wazalendo waliuounda TANU na waliopigania uhuru wa Tanganyika.
 
Back
Top Bottom