Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
HATUJACHELEWA KUIWEKA SAWA HISTORIA YA TANU NA UHURU WA TANGANYIKA
Hiyo picha hapo chini ni 1955/56 Dodoma Railway Station kushoto ni Iddi Faiz Mafungo, Sheikh Mohamed Ramiya, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu.
Ningefarajika sana kaka picha hii ingewekwa Makao Makuu ya CCM Dodoma kwa ukumbusho wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Ukimtoa Mwalimu Nyerere katika picha hiyo kuna yeyote anaeweza kueleza mchango wa wazalendo hawa wengine katika kupigania uhuru wa Tanganyika?
Iddi Faizi Mafungo alikuwa Mwekahazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na pia Mwekahazina wa TANU.
Yeye ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kukusanya fedha za safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere UNO 1955.
Iddi Faizi na Sheikh Mohamed Ramia ni ndugu na ndiye aliyempeleka Mwalimu Bagamoyo kwa Sheikh Ramia akiongozana na Iddi Tosiri.
Wote hawa watatu ni ndugu wote hawa Wamanyema wazee wao wakitokea Belgian Congo katika miaka ya 1800 na walikuwa na chama chao cha Wamanyema - Batetera Union.
Ukitokea msiba walikuwa na ngoma wanapiga na ukisikika mlio wa ngoma ile wanajua kuna msiba.
Walipoamua kuunda TANU na kujenga taifa la Tanganyika yote haya yakaisha.
Historia ya Iddi Faizi jinsi alivyoandamwa na Special Branch wakati wa safari ya Mwalimu UNO siku anakusanya fedha za TANU ni senema ambayo anaeweza kuiongoza ni Steven Spielberg au Oliver Stone.
Haendi mtu msalani.
Sheikh Ramiya alisoma Maulid wakati wa kipindupindu Bagamoyo polisi wakenda nyumbani kwake kumleta kituo cha polisi kumhoji.
Habari zikaenea Khalifa wa Tarika Quadiriyya kakamatwa.
Haukupita muda Bagamoyo nzima na pembezoni na hii ikasababisha kituo cha polisi kuzungukwa na murid kila upande wamekuja kumtoa kiongozi wao.
Wachache katika askari wa pale kituoni waliojua kwa nini ghafla Bagamoyo nzima ikawa kama vile imehamia kituo cha polisi.
Murid wengine wametoka mashamba wamekuja Bagamoyo mjini kwa baiskeli wengi wao ni wakwezi na askari walitishika kuwaona wana visu kiunoni.
Saadan Abdul Kandoro amekufa hawezi kulipa ankara za umeme wala maji ya nyumba yake Magomeni Mikumi.
Yeye ndiye aliyeunda TANU Kanda ya Ziwa na ni mmoja kati ya waasisi 17 wa TANU 1954.
Haruna Taratibu ndiye aliyeasisi TANU Central Province 1955 pamoja na Omari Suleiman.
Inahitaji kuandika kitabu kizima kuieleza historia ya wazalendo hawa.
PICHA:
Aliyesimama mbele ya sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni Abdallah Saiwaad Mhariri Bingwa wa miswada ya vitabu.