Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Automata,Ha ha ha, eti tusichoke kukumbushana
Kumbe ushajua huna jipya (ushazoeleka-maandiko yako ni udini, malamishi, upotoshaji, na nk)
Automata,Umejikita kuufifisha, na kupotosha mchango wa Mwalimu Nyerere kisa dini yake na kuwapaisha uwapendao wewe
Laki...Mohamed Said, baada ya uhuru wana TANU wengi walimezwa na sera za ubepari, tamaa ya kujilimbikizia mali, ubinafsi, hili jambo Nyerere ambae alikuwa mjamaa hakupendezwa nalo, akawashughulikia kwa kuwaweka jela, vizuizini, kuwafukuza TANU na kufilisi mali zao, wengi wa mabepari wakatoroka nchi , mfano Oscar Kambona, Abdurahman Babu, Kasim Hanga, Sheikh Othman Sharif, haingekuwa busara kuwaingiza kwenye historia wakati hawakuwa mfano mzuri kwa taifa, ndio maana historia imewakwepa,
We ni mdini tu!, maandiko yako yote ni kuwapamba na kuwakweza waislamu na uislamu wakati huo huo ukipotosha, kukosoa na kuwadogosha viongozi wakristo/ama ukristo, iwe ni kwenye TANU, CCM, Harakati za Uhuru, Muungano, na nk.Udini si kweli ila tuseme hujapendezewa kwa mimi kuieleza historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Unadhani ni sababu gani Oscar Kambona alisafiri kutoka Uingereza kwenda Guinea kuonana na Kassim Hanga? Walipanga nini? kwa msaada wa nani? kuna watu walitumika na mabepari kumuhujumu nyerere,Laki...
Sikujua kuwa Kassim Hanga, Othman Shariff na Abdulrahman Babu walikuwa mabebari.
Leo unanisomesha historia mpya.
Sent using Jamii Forums mobile app
Unadhani ni sababu gani Oscar Kambona alisafiri kutoka Uingereza kwenda Guinea kuonana na Kassim Hanga? Walipanga nini? kwa msaada wa nani? kuna watu walitumika na mabepari kumuhujumu nyerere,Laki...
Sikujua kuwa Kassim Hanga, Othman Shariff na Abdulrahman Babu walikuwa mabebari.
Leo unanisomesha historia mpya.
Sent using Jamii Forums mobile app
inawezekana akina Abdurahman Babu, Kassim Hanga, hawakuwa mabepari, lakini walikuwa na nia ovu ya kumpindua Karume, Huku bara akina Titi Mohamed, Kambona na washirika wengine wakataka kumpindua Nyerere, hapo unapata picha wapigania uhuru wengi walioleta uhuru , waligeukana baada ya uhuru,Laki...
Sikujua kuwa Kassim Hanga, Othman Shariff na Abdulrahman Babu walikuwa mabebari.
Leo unanisomesha historia mpya.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ninachokiona kwenu ni nyinyi kutaabika na historia hii ya kweli kwa akili zenu kukataa kuamini ukweli wa mambo mkatamani kubakia na ile historia iliyowafuta wazalendo waliuounda TANU na waliopigania uhuru wa Tanganyika.Sl
Sent using Jamii Forums mobile app
Laki...
Wote wanataka kutambulika hii fikra kuwa kulikuwa na watu walitaka kutambulika wewe umeitoa wapi?
Watake kutambulika kwa kufanya nini?
Huenda wewe hujui yaliyopitika baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961.
Sijapata kusikia au kusoma popote kuwa katika waasisi wa TANU wako waliotaka kutambulika.
Mimi nililiona tatizo la historia ya TANU mwaka wa 1981 katika kitabu cha Chuo Cha CCM Kivukoni.
Historia ile waliyoandika haikuwa historia ya TANU niijuavyo mimi ndipo nikaandika hii historia mnayoisoma hivi sasa hapa barzani.
Ninachokiona kwenu ni nyinyi kutaabika na historia hii ya kweli kwa akili zenu kukataa kuamini ukweli wa mambo mkatamani kubakia na ile historia iliyowafuta wazalendo waliuounda TANU na waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Automata,We ni mdini tu!, maandiko yako yote ni kuwapamba na kuwakweza waislamu na uislamu wakati huo huo ukipotosha, kukosoa na kuwadogosha viongozi wakristo/ama ukristo, iwe ni kwenye TANU, CCM, Harakati za Uhuru, Muungano, na nk.
(Maandiko yako yote scope na objective ni waislamu na uislamu)......'jomba' usidhani we ndo msomi/mwandishi pekeyako kwamba 'michezo' unayofanya haifahamiki
May Day,Ninachokiona kwenu ni nyinyi kutaabika na historia hii ya kweli kwa akili zenu kukataa kuamini ukweli wa mambo mkatamani kubakia na ile historia iliyowafuta wazalendo waliuounda TANU na waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Mzee Said.
Sidhani kama hoja hapa ni Mtu kutaabika, ila tatizo la mandiko yako ni kukosekana namna ya kuunganisha doti.
Nilishacomment huko nyuma na narudia tena...umekuwa unamlenga na kumtaja Mwalimu kama Mtu aliyezuka tu na kubebwa na unaowaita 'Wazee wako'.
Kuna Mdau amesema hapo juu kuhusu mchango wa wengi kufanikisha TANU na harakati zake, lakini sijui ni kwa nini umekuwa unasisitiza kutambuliwa kwa baadhi yao tu, tena wale unaowachagua.
Hata Mwalimu mwenyewe ameongea sana kuhusu Wazee wa Dar Es Salaam kwa umoja wao, lakini huishi kwataja Wazee baadhi wasiozidi kama ishirini au hamsini hivi.
Unataka tuamini ya kwamba harakati za kupigania uhuru wa nchi hii zilianza na kukamilishwa kwenye eneo moja tu ilihali nchi hii ni kubwa , na karibia kila jimbo kulikuwa na harakati/mawasiliano na kazi zilifanyika.
Na si kwamba unayosema ni urongo ama la, baadhi yana ukweli kwa 100% ila una hariri sana kwa kukwepa yale usiyo na maslahi nayo.
Hata hivyo nafurahi unavyoleta maandiko hapa kwani kupitia maoni tunajifunza zaidi.
Bome...Mimi nina swali moja kwako mzee Said,hivi katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika,waliohusika katika harakati hizo ukiachana na Nyerere ni waislamu pekee unaowatambua?Nauliza hivyo maana katika threads zako nyingi za historia ya uhuru wetu,zaidi ya Nyerere sijaona mkristu mwingine ukiamuandika!Ni kwamba huwafahamu wakristo wengine au hauna interest nao kwenye maandiko yako?Hii ndio sababu kubwa watu wengi wamekuwa wakikuona una angle nyingine zaidi ya kueleza historia!Na hii inashusha sana credibility ya nyuzi zako!
Hapo ndipo shida ilipo,maana inaonekana unapambania zaidi dini yako!Kwa namna hii ni vigumu sana kwa watu kuijua historia maana utapuuzwa kila mara!Usingekuwa biased nadhani ungepata support ya kutosha kwenye kuiweka historia yetu sawa!Bome...
Wakristo walikuwapo katika harakati za kupigania uhuru na kwenye kitabu cha Abdul Sykes nimewataja.
Walikuwapo akina Dome Okochi Budohi (Mkenya) kadi yake ya TANU ni no. 5, Dennis Phombeah(Mnyasa) kadi yake ya TANU no. 6 Steven Mhando na mdogo wake Peter Mhando, Robert Makange kwa kuwataja wachache.
Ila mchango wa Waislam kama wanachama wa TANU ni historia ya pekee na ndiyo sababu nilipoona haipo nikaamua kuiandika na naamini hata wewe unapoisoma inakusisimua.
Sent using Jamii Forums mobile app
Boma,Hapo ndipo shida ilipo,maana inaonekana unapambania zaidi dini yako!Kwa namna hii ni vigumu sana kwa watu kuijua historia maana utapuuzwa kila mara!Usingekuwa biased nadhani ungepata support ya kutosha kwenye kuiweka historia yetu sawa!
Laki...TANU ilizaliwa katika mazingira ya vyama vya ushirika, baadhi ya vyama vya ushirika vilvyokuwepo kabla ya TANU ni: {1) Kilimanjaro Co-operative Union Ltd -1933 {2} Ngoni Matengo Cooperative Union Ltd- 1936 {3} Rungwe African Cooperative Union Ltd ~ 1949 {4} Lake Province Native Growers Association. {5} Bukoba Cooperative Union Ltd- 1950 Kwa kuwepo vyama hivi , ujumbe wa TANU uliwafikia wananchi kwa urahisi, wanachama wa vyama vya ushirika , walijiunga na TANU, viongozi wa ushirika, walichaguliwa kuwa viongozi wa TANU TAIFA , Mfano: Nsilo Swai, George Kahama, Jeremia Kasambala, Paul Bomani, John Mhavile. N.B. Mohamed Said, mchango wa vyama vya ushirika kwenye TANU ni mkubwa kupita mchango wa mtu mmoja mmoja, bila vyama vya ushirika, TANU ingeishia kariakoo tu kwa wazaramo na wamanyema.