Tusichoke kukumbushana kwani kukumbushana kuna faida: Hatujachelewa kuiweka sawa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika

Tusichoke kukumbushana kwani kukumbushana kuna faida: Hatujachelewa kuiweka sawa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika

Ha ha ha, eti tusichoke kukumbushana

Kumbe ushajua huna jipya (ushazoeleka-maandiko yako ni udini, malamishi, upotoshaji, na nk)
 
Umejikita kuufifisha, na kupotosha mchango wa Mwalimu Nyerere kisa dini yake na kuwapaisha uwapendao wewe
 
Mohamed Said, baada ya uhuru wana TANU wengi walimezwa na sera za ubepari, tamaa ya kujilimbikizia mali, ubinafsi, hili jambo Nyerere ambae alikuwa mjamaa hakupendezwa nalo, akawashughulikia kwa kuwaweka jela, vizuizini, kuwafukuza TANU na kufilisi mali zao, wengi wa mabepari wakatoroka nchi , mfano Oscar Kambona, Abdurahman Babu, Kasim Hanga, Sheikh Othman Sharif, haingekuwa busara kuwaingiza kwenye historia wakati hawakuwa mfano mzuri kwa taifa, ndio maana historia imewakwepa,
 
Ha ha ha, eti tusichoke kukumbushana

Kumbe ushajua huna jipya (ushazoeleka-maandiko yako ni udini, malamishi, upotoshaji, na nk)
Automata,
Udini si kweli ila tuseme hujapendezewa kwa mimi kuieleza historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Kuwa sina jipya hakika hakuna jipya kwako lakini kila siku napata wasomaji wapya ambao ndiyo wao hii leo ndiyo wanasikia kuwa kulikuwa na mtu anaitwa Iddi Faiz Mafungo na wanasoma historia ya mchango wake katika TANU.

Kuzoeleka huku nakujua sana na ndiko kunakokufanya wewe ushindwe kuacha kunisoma.

Tabu sana kunipuuza kwa kuwa huwezi kuacha kusoma niandikayo popote pale.

Kipo kinachokuvuta.

Nimesomesha wengi historia ya Tanganyika ambayo ilifutika kabisa na wameelimika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umejikita kuufifisha, na kupotosha mchango wa Mwalimu Nyerere kisa dini yake na kuwapaisha uwapendao wewe
Automata,
Sijafifilisha mchango wa Mwalimu Nyerere.

Nilichofanya nimeirudisha historia ya TANU nyuma hadi mwaka wa 1929 kwa ushahidi wa mswada wa Kleist Sykes nikaeleza vipi yeye na wenzake akina Ibrahim Hamisi, Mzee bin Sudi, Raikes Kusi kuwataja wachache waliunda African Association.

Kisha nikaeleza jinsi 1933 Kleist na wenzake wakaunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Umuhimu wa taasisi hizi mbili ni kuwa viongozi wake wengi walikuwa Waislam na wanachama wa mwanzo wa TANU na baadhi ya viongozi wake walitokana na taasisi hizi.

Wako ambao hawakupendezewa na ukweli huu lakini ndiyo historia inavyosema.

Ukikwepa ukweli huu hapo utamfuta Kleist na wanae, utamfuta Iddi Faiz na nduguye Iddi Tosiri, utamfuta Sheikh Hassan bin Ameir.

Ukiwatoa hawa hiyo tena si historia ya TANU ni kitu kingine kabisa.

Sikuandika haya kwa kuwapenda ila hii ndiyo historia ya TANU.

Ikiwa wewe unayo nyingine isiyokuwa hii tuandikie tuisome.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mohamed Said, baada ya uhuru wana TANU wengi walimezwa na sera za ubepari, tamaa ya kujilimbikizia mali, ubinafsi, hili jambo Nyerere ambae alikuwa mjamaa hakupendezwa nalo, akawashughulikia kwa kuwaweka jela, vizuizini, kuwafukuza TANU na kufilisi mali zao, wengi wa mabepari wakatoroka nchi , mfano Oscar Kambona, Abdurahman Babu, Kasim Hanga, Sheikh Othman Sharif, haingekuwa busara kuwaingiza kwenye historia wakati hawakuwa mfano mzuri kwa taifa, ndio maana historia imewakwepa,
Laki...
Sikujua kuwa Kassim Hanga, Othman Shariff na Abdulrahman Babu walikuwa mabebari.

Leo unanisomesha historia mpya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Udini si kweli ila tuseme hujapendezewa kwa mimi kuieleza historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
We ni mdini tu!, maandiko yako yote ni kuwapamba na kuwakweza waislamu na uislamu wakati huo huo ukipotosha, kukosoa na kuwadogosha viongozi wakristo/ama ukristo, iwe ni kwenye TANU, CCM, Harakati za Uhuru, Muungano, na nk.

(Maandiko yako yote scope na objective ni waislamu na uislamu)......'jomba' usidhani we ndo msomi/mwandishi pekeyako kwamba 'michezo' unayofanya haifahamiki
 
Laki...
Sikujua kuwa Kassim Hanga, Othman Shariff na Abdulrahman Babu walikuwa mabebari.

Leo unanisomesha historia mpya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unadhani ni sababu gani Oscar Kambona alisafiri kutoka Uingereza kwenda Guinea kuonana na Kassim Hanga? Walipanga nini? kwa msaada wa nani? kuna watu walitumika na mabepari kumuhujumu nyerere,
 
inawezekana akina Abdurahman Babu, Kassim Hanga, hawakuwa mabepari, lakini walikuwa na nia ovu ya kumpindua Karume, Huku bara akina Titi Mohamed, Kambona na washirika wengine wakataka kumpindua Nyerere, hapo unapata picha wapigania uhuru wengi walioleta uhuru , waligeukana baada ya uhuru,
 
Sl

Sent using Jamii Forums mobile app
Laki...
Wote wanataka kutambulika hii fikra kuwa kulikuwa na watu walitaka kutambulika wewe umeitoa wapi?

Watake kutambulika kwa kufanya nini?

Huenda wewe hujui yaliyopitika baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961.

Sijapata kusikia au kusoma popote kuwa katika waasisi wa TANU wako waliotaka kutambulika.

Mimi nililiona tatizo la historia ya TANU mwaka wa 1981 katika kitabu cha Chuo Cha CCM Kivukoni.

Historia ile waliyoandika haikuwa historia ya TANU niijuavyo mimi ndipo nikaandika hii historia mnayoisoma hivi sasa hapa barzani.

Ninachokiona kwenu ni nyinyi kutaabika na historia hii ya kweli kwa akili zenu kukataa kuamini ukweli wa mambo mkatamani kubakia na ile historia iliyowafuta wazalendo waliuounda TANU na waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Mzee Said.
Sidhani kama hoja hapa ni Mtu kutaabika, ila tatizo la mandiko yako ni kukosekana namna ya kuunganisha doti.

Nilishacomment huko nyuma na narudia tena...umekuwa unamlenga na kumtaja Mwalimu kama Mtu aliyezuka tu na kubebwa na unaowaita 'Wazee wako'.

Kuna Mdau amesema hapo juu kuhusu mchango wa wengi kufanikisha TANU na harakati zake, lakini sijui ni kwa nini umekuwa unasisitiza kutambuliwa kwa baadhi yao tu, tena wale unaowachagua.

Hata Mwalimu mwenyewe ameongea sana kuhusu Wazee wa Dar Es Salaam kwa umoja wao, lakini huishi kwataja Wazee baadhi wasiozidi kama ishirini au hamsini hivi.

Unataka tuamini ya kwamba harakati za kupigania uhuru wa nchi hii zilianza na kukamilishwa kwenye eneo moja tu ilihali nchi hii ni kubwa , na karibia kila jimbo kulikuwa na harakati/mawasiliano na kazi zilifanyika.

Na si kwamba unayosema ni urongo ama la, baadhi yana ukweli kwa 100% ila una hariri sana kwa kukwepa yale usiyo na maslahi nayo.

Hata hivyo nafurahi unavyoleta maandiko hapa kwani kupitia maoni tunajifunza zaidi.
 
Waliokuwepo Dar walipata nafasi au bahati kwani Dar ilikuwa ni kama kitovu, na ni bahati kwamba Mwalimu naye alilazimika kuwepo Dar kufanya shughuli zake.

Ila ukweli ni kwamba kuna maeneo mengi tu ya nchi kazi iliendelea.

Naambatisha kipande kidogo kutoka Pare Mountains.
Independence Movement[edit]
The Pare Union formed in 1946 was one of Tanzania's first ethnic-based nationalist movements to begin activism against the colonial system. Among many grievances, was the exploitation through the production of export crops particularly Sisal and Coffee. Like many other ethnic-based political groups in Tanganyika, The Pare Union then became part of the Tanganyika African Association (TAA) which later became the Tanganyika African National Union (TANU) in 1954. This avoided groups like the Pare Union forming into full political parties that were ethnic in orientation.

Moses Seenarine writes of the contribution of Pare women in the struggle: 'The Pare women's uprising in northwest Shambaai, Tanzania, occurred in early January 1945 and continued with demonstrations into 1946, involving thousands of women. It began in Usangi, one of the chiefdoms, when the district commissioner arrived for discussions with the local chief. A crowd of hundreds (if not thousands) of women appeared, demanding an explanation of mbiru, a system of graduated taxation. When the commissioner tried to leave without addressing the women, they became enraged and mobbed the assembled officials. Two days later, women surrounded the chief's house singing songs, and ultimately stoned officials and battled police.' The Mbiru protest by the Pare people refusing to pay colonial tax was eventually led by Paulo Kajiru of Mamba. The Pare eventually managed to defeat this tax system, and eventually went back to the flat rate of tax in 1947[9]. This is an important historical event in Tanzania.
 
We ni mdini tu!, maandiko yako yote ni kuwapamba na kuwakweza waislamu na uislamu wakati huo huo ukipotosha, kukosoa na kuwadogosha viongozi wakristo/ama ukristo, iwe ni kwenye TANU, CCM, Harakati za Uhuru, Muungano, na nk.

(Maandiko yako yote scope na objective ni waislamu na uislamu)......'jomba' usidhani we ndo msomi/mwandishi pekeyako kwamba 'michezo' unayofanya haifahamiki
Automata,
Hakika mimi nimeandika historia ya Waislam wa Tanganyika hili siwezi kulikataa hata kitabu changu cha kwanza anuani yake ni: ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika.''

Nadhani unaona ''title'' ya kitabu inajieleza yenyewe kuwa ni historia ambayo haijaelezwa.

Hili la kwanza.

La pili ni ipi hiyo historia ambayo haijaelezwa?

Sasa ndiyo unapata jibu kuwa ni harakati za Waislam dhidi ya ukoloni wa Waingereza.

Kwani kulikuwa na harakati za Waislam?

Sasa ukiingia ndani ya kitabu ndipo unaikuta historia yenyewe.

Kwa hakika kitu kinachowakera wengi ni kuwa historia hii ambayo kwangu mimi ni historia ya wazee wangu imegusa historia ya uhuru wa Tanganyika.

Hapa ndipo lilipo tatizo kwa wengi.

Wapo wasiopendezewa na watu hawa kuunganishwa na historia ya Mwalimu Nyerere.

Laiti historia hii ya wazee wangu isingegusa historia ya ukombozi wa Tanganyika pasingekuwa na tatizo lolote.

Bahati mbaya sana Mwalimu Nyerere hakupata kueleza historia hii.

Mathalan wewe unaweza kuandika historia ya kwenu lakini haitamgusa Mwalimu Julius Nyerere wala haitagusa historia ya African Association wala Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika wala haitagusa historia ya TANU.

Kwangu mimi hili haliwezekani.

Bahati mbaya kuwa historia hii wewe inaunguza moyo wako pakubwa lakini tufanyeje?

Ingekuwa sawa kwangu mimi kuacha kuandika historia hii?

Ningefanya hivi ningekuwa nimejifanyia khiyana mimi mwenyewe na wazee wangu.

Angalia picha hizo hapo chini wakati wa kupigania uhuru.

Picha ya kwanza ni safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere UNO mwezi February 1955 hao akina mama kulia ni Bi. Chiku Said Kisusa mke wa Shariff Attas, Bi. Titi Mohamed, na wa mwanza kushoto ni Bi. Tatu bint Mzee.

Picha ya pili ni Baraza la Wazee wa TANU August, 1954.

Picha ya tatu ni babu yangu Salum Abdallah akivishwa mgolole mmoja wa waasisi wa TANU Tabora 1955 na muasisi wa Tanganyika Railway Africa Union (TRAU) akiwa Rais na Kasanga Tumbo Katibu.

Katika picha hiyo Kassanga Tumbo wa kwanza kulia nyuma ya huyo anaemvisha babu yangu mgolole kama alama ya jemadari aanaeongoza vita dhidi ya wakoloni.

Hii ndiyo historia ya wazee wangu na walikuwa Waislam na haya yote wameyafanya lakini hayakuandikwa katika kitabu cha historia ya TANU kilichoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni.

Mbona hujawa na ujasiri wa kuuliza imekuwaje wazalendo hawa hawamo katika historia ya uhuru wala picha zao hazipambi kuta ofisi za CCM Lumumba na Dodoma?

Ili historia hii isifutike mimi nimeaiandika.

Wewe ulitakaje?

Mimi sina tatizo na kuitwa mdini wala jina hilo halininyimi usingizi.

Kama unaona huu ni uongo andika ukweli unaoujua wewe tuusome.

Mimi siko katika ''mchezo'' kama ulivyosema mimi nimeandika historia hii kwa nia ya kusahihisha historia iliyopotoshwa siko hapa kufanya michezo wala maskhara.

Jiulize hivi wazee wako wangekuwa na historia kama hii ungeache kuiandika?
 
Attachments

  • TATU BINT MZEE (1).JPG
    TATU BINT MZEE (1).JPG
    15.4 KB · Views: 2
  • BARAZA LA WAZEE WA TANU.jpg
    BARAZA LA WAZEE WA TANU.jpg
    36.4 KB · Views: 2
  • SALUM ABDALLAH NA MGOLOLE.jpg
    SALUM ABDALLAH NA MGOLOLE.jpg
    88.3 KB · Views: 2
Ninachokiona kwenu ni nyinyi kutaabika na historia hii ya kweli kwa akili zenu kukataa kuamini ukweli wa mambo mkatamani kubakia na ile historia iliyowafuta wazalendo waliuounda TANU na waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Mzee Said.
Sidhani kama hoja hapa ni Mtu kutaabika, ila tatizo la mandiko yako ni kukosekana namna ya kuunganisha doti.

Nilishacomment huko nyuma na narudia tena...umekuwa unamlenga na kumtaja Mwalimu kama Mtu aliyezuka tu na kubebwa na unaowaita 'Wazee wako'.

Kuna Mdau amesema hapo juu kuhusu mchango wa wengi kufanikisha TANU na harakati zake, lakini sijui ni kwa nini umekuwa unasisitiza kutambuliwa kwa baadhi yao tu, tena wale unaowachagua.

Hata Mwalimu mwenyewe ameongea sana kuhusu Wazee wa Dar Es Salaam kwa umoja wao, lakini huishi kwataja Wazee baadhi wasiozidi kama ishirini au hamsini hivi.

Unataka tuamini ya kwamba harakati za kupigania uhuru wa nchi hii zilianza na kukamilishwa kwenye eneo moja tu ilihali nchi hii ni kubwa , na karibia kila jimbo kulikuwa na harakati/mawasiliano na kazi zilifanyika.

Na si kwamba unayosema ni urongo ama la, baadhi yana ukweli kwa 100% ila una hariri sana kwa kukwepa yale usiyo na maslahi nayo.

Hata hivyo nafurahi unavyoleta maandiko hapa kwani kupitia maoni tunajifunza zaidi.
May Day,
Ikiwa kuna historia ya wazalendo waliokuwa huko majimboni na haifahamiki mwenye kuifahamu aiandike hakuna tabu.
Mimi nimeandika historia niijuayo na siwezi kudai kuwa imekamilika.

Wengine wajitokeze waandike.
Wala sijasisitiza kuwa wazee wangu watambuliwe.

Katika wazalendo niliowataja katika kitabu changu waliopewa medali ni wawili tu Abdul na Ally Sykes na sijui sababu yake kwani wengine waliokuwa pamojanao hawakupewa.

Historia nimeiandika na ndiyo hii tuko hapa tunaijadili.
 
Mimi nina swali moja kwako mzee Said,hivi katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika,waliohusika katika harakati hizo ukiachana na Nyerere ni waislamu pekee unaowatambua?Nauliza hivyo maana katika threads zako nyingi za historia ya uhuru wetu,zaidi ya Nyerere sijaona mkristu mwingine ukiamuandika!Ni kwamba huwafahamu wakristo wengine au hauna interest nao kwenye maandiko yako?Hii ndio sababu kubwa watu wengi wamekuwa wakikuona una angle nyingine zaidi ya kueleza historia!Na hii inashusha sana credibility ya nyuzi zako!
 
Bome...
Wakristo walikuwapo katika harakati za kupigania uhuru na kwenye kitabu cha Abdul Sykes nimewataja.

Walikuwapo akina Dome Okochi Budohi (Mkenya) kadi yake ya TANU ni no. 5, Dennis Phombeah(Mnyasa) kadi yake ya TANU no. 6 Steven Mhando na mdogo wake Peter Mhando, Robert Makange kwa kuwataja wachache.

Ila mchango wa Waislam kama wanachama wa TANU ni historia ya pekee na ndiyo sababu nilipoona haipo nikaamua kuiandika na naamini hata wewe unapoisoma inakusisimua.

Hapo ndipo shida ilipo,maana inaonekana unapambania zaidi dini yako!Kwa namna hii ni vigumu sana kwa watu kuijua historia maana utapuuzwa kila mara!Usingekuwa biased nadhani ungepata support ya kutosha kwenye kuiweka historia yetu sawa!
 
TANU ilizaliwa katika mazingira ya vyama vya ushirika, baadhi ya vyama vya ushirika vilvyokuwepo kabla ya TANU ni: {1) Kilimanjaro Co-operative Union Ltd -1933 {2} Ngoni Matengo Cooperative Union Ltd- 1936 {3} Rungwe African Cooperative Union Ltd ~ 1949 {4} Lake Province Native Growers Association. {5} Bukoba Cooperative Union Ltd- 1950 Kwa kuwepo vyama hivi , ujumbe wa TANU uliwafikia wananchi kwa urahisi, wanachama wa vyama vya ushirika , walijiunga na TANU, viongozi wa ushirika, walichaguliwa kuwa viongozi wa TANU TAIFA , Mfano: Nsilo Swai, George Kahama, Jeremia Kasambala, Paul Bomani, John Mhavile. N.B. Mohamed Said, mchango wa vyama vya ushirika kwenye TANU ni mkubwa kupita mchango wa mtu mmoja mmoja, bila vyama vya ushirika, TANU ingeishia kariakoo tu kwa wazaramo na wamanyema.
 
Boma,
Kitabu hiki hakijapuuzwa.

Kilipotoka mwaka wa 1998 kilifanyiwa "book review," na mabingwa wa African History - John Illife, Jonathon Glassman na James Brennan na hizi review zikachapwa katika CambridgeJournal of African History.

Halikadhalika The East African (Nairobi) waliotoa "series" tatu.

Hadi sasa kitabu kimepigwa chapa mara tatu na kimetafsiriwa kwa Kiswahili 2002 na tunakwenda chapa ya nne.

Sababu kubwa ya mafanikio haya ni kuwa kitabu kimebadili historia nzima ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Kitabu hiki nimekizungumza University of Iowa na Northwestern University Evanston, Chicago kwengine kwingi.

Kwa hakika hata mimi sikutegemea mengi ambayo nimeyashuhudia baada ya kuandika kitabu hiki.

Hayo ya "bias," wala sijui unakusudia nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANU ilizaliwa katika mazingira ya vyama vya ushirika, baadhi ya vyama vya ushirika vilvyokuwepo kabla ya TANU ni: {1) Kilimanjaro Co-operative Union Ltd -1933 {2} Ngoni Matengo Cooperative Union Ltd- 1936 {3} Rungwe African Cooperative Union Ltd ~ 1949 {4} Lake Province Native Growers Association. {5} Bukoba Cooperative Union Ltd- 1950 Kwa kuwepo vyama hivi , ujumbe wa TANU uliwafikia wananchi kwa urahisi, wanachama wa vyama vya ushirika , walijiunga na TANU, viongozi wa ushirika, walichaguliwa kuwa viongozi wa TANU TAIFA , Mfano: Nsilo Swai, George Kahama, Jeremia Kasambala, Paul Bomani, John Mhavile. N.B. Mohamed Said, mchango wa vyama vya ushirika kwenye TANU ni mkubwa kupita mchango wa mtu mmoja mmoja, bila vyama vya ushirika, TANU ingeishia kariakoo tu kwa wazaramo na wamanyema.
Laki...
Mimi siwezi kukupinga katika hili kuwa TANU ilijengwa na Ngoni Matengo.

Mimi nimeandika historia ninavyoijua kama nilivyopokea kwa wazee wangu wa Kariakoo na kama nilivyosoma katika Nyaraka za Sykes zinazoanza mwisho wa 1800 hadi kufika kuundwa kwa African Association 1929 na kuendelea kufikia 1954 ilipoundwa TANU.

Mimekuthibitishieni historia hii kwa ushahidi wa nyaraka na picha.

Ukiwa huko kwenu iliundwa TANU kutoka vyama vya ushirika mimi siwezi kukupinga kwa kuwa siijui historia hiyo.

Kwa kawaida ninapoletewa hoja mfano wa hii yako mimi hujibu kwa kusema kuwa huenda kuna wazalendo wengine huko majimboni walikuwa na fikra ya kuunda TANU nje ya hawa wazee wangu na uhitimisha kwa mwito kuwa tutie hima historia hii nayo ifanyiwe utafiti na kuandika.

Lakini ukweli wengi huwa hawaridhishwi na haya majibu yangu kwa sababu zilizo wazi.

TANU ya Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Hamza Mwapachu, Dossa Aziz, John Rupia Julius Nyerere imewashangaza sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom