Tusichoke kukumbushana kwani kukumbushana kuna faida: Hatujachelewa kuiweka sawa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika

Tusichoke kukumbushana kwani kukumbushana kuna faida: Hatujachelewa kuiweka sawa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika

Boma,
Kitabu hiki hakijapuuzwa.

Kilipotoka mwaka wa 1998 kilifanyiwa "book review," na mabingwa wa African History - John Illife, Jonathon Glassman na James Brennan na hizi review zikachapwa katika CambridgeJournal of African History.

Halikadhalika The East African (Nairobi) waliotoa "series" tatu.

Hadi sasa kitabu kimepigwa chapa mara tatu na kimetafsiriwa kwa Kiswahili 2002 na tunakwenda chapa ya nne.

Sababu kubwa ya mafanikio haya ni kuwa kitabu kimebadili historia nzima ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Kitabu hiki nimekizungumza University of Iowa na Northwestern University Evanston, Chicago kwengine kwingi.

Kwa hakika hata mimi sikutegemea mengi ambayo nimeyashuhudia baada ya kuandika kitabu hiki.

Hayo ya "bias," wala sijui unakusudia nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bado impact yake ni ndogo katika jamii yetu ya kitanzania,leo hii asilimia kubwa ya watanzania hawajui hayo yaliyoko kwenye hicho kitabu!Pia jitahada zako humu JF zinafifishwa na udini uliokujaa kwa maana unaonekana wazi unaitangaza dini yako katika historia ya nchi yetu!Watu wa dini yako unawapaka rangi sana humu!Ukiachana na kutowataja wakristu ambao historia imesahau walioshiriki katika ukombozi,hata huyu Nyerere anayetajwa kwenye historia unajaribu kushusha heshima yake na kwamba hastahili hizo sifa anazopewa!Kwa sababu hizo,uungwaji wako mkono unasuasua na lengo lako haliwezi kutimia kwa maana watu wakishaona jina lako tu wanajua ni yaleyale ya udini na kumu-undermine Nyerere!
Kizazi kinachokuja bado hakitaijua historia vizuri,itakuwa kama jana na leo!
Ningeshauri uweze kupambana kwanza na hisia binafsi ili uweze kuandika historia bila msukumo wa kidini,hii inaweza kuleta matokeo chanya sana Mzee Said!
 
Mohamed Said kwa hiyo unaijua historia ya TANU ya watu wa kariakoo tu, siyo Tanganyika yote, huku Songea wana TANU walikuwa wanawajua Nyerere na Kambona na viongozi wa vyama vya ushirika tu maana ndio waliokuwa wanakuja kuwahamasisha watu, historia ya TANU ni pana sana haiishii kariakoo na magomeni tu, kuandika historia ya wazee wa kariakoo peke yake, hauwatendei haki wapigania uhuru wengine wa mikoani
 
Bome...
Siwezi mimi kukisemea kitabu changu kwa namna unavyohoji mafanikio au kufeli kwake.

Ninachoweza kukueleza ni kuwa kitabu kimenunulika sana kiasi tunakwenda toleo la nne.

Hili la kwanza.

Pili ni kuwa napokea kila siku mialiko kuzungumza historia hii.

Nimezungumza University of Johannesburg, Zanzibar University, University of Ibadan, Kenyatta University, University of Dar es Salaam, Muslim University of Morogoro, Mzumbe University, University of Iowa, Northwestern University na Zentrum Moderner Orient, Berlin.

Oxford University Press Nairobi wakanitia katika mradi wa kuandika vitabu vya historia shule za msingi na wamechapa kitabu changu, "The Torch on Kilimanjaro," na nimeshiriki kwenye kitabu "African Anthology," nikiwa mmoja wa waandishi kutoka nchi kadhaa za Afrika.

Halikadhalika nimetiwa katika mradi wa Harvard na Oxford University Press New York - Dictionary of African Biography (DAB)na niliombwa kumwandika Kleist Sykes (1894 - 1949).

Oxford University Press New York wametoa volume sita ya kazi hii mwaka 2011.

Hapa IF nimefanya mjadala uliodumu miezi sita bila ya kusimama kuhusu kitabu cha Abdul Sykes.

Hili lilikuwa halijapata kutokea.

Yapo mengi si kweli kuwa napuuzwa.

Fanya utafiti wako kwa utulivu upate kunifahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bome...
Siwezi mimi kukisemea kitabu changu kwa namna unavyohoji mafanikio au kufeli kwake.

Ninachoweza kukueleza ni kuwa kitabu kimenunulika sana kiasi tunakwenda toleo la nne.

Hili la kwanza.

Pili ni kuwa napokea kila siku mialiko kuzungumza historia hii.

Nimezungumza University of Johannesburg, Zanzibar University, University of Ibadan, Kenyatta University, University of Dar es Salaam, Muslim University of Morogoro, Mzumbe University, University of Iowa, Northwestern University na Zentrum Moderner Orient, Berlin.

Oxford University Press Nairobi wakanitia katika mradi wa kuandika vitabu vya historia shule za msingi na wamechapa kitabu changu, "The Torch on Kilimanjaro,na nimeshiriki kwenye kitabu "African Anthology," nikiwa mmoja wa waandishi kutoka nchi kadhaa za Afrika.

Halikadhalika nimetiwa katika mradi wa Harvard na Oxford University Press New York - Dictionary of African Biography (DAB)na niliombwa kumwandika Kleist Sykes (1894 - 1949).

Oxford University Press New York wametoa volume sita ya kazi hii mwaka 2011.

Hapa IF nimefanya mjadala uliodumu miezi sita bila ya kusimama kuhusu kitabu cha Abdul Sykes.

Hili lilikuwa halijapata kutokea.

Yapo mengi si kweli kuwa napuuzwa.

Fanya utafiti wako kwa utulivu upate kunifahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaamini maandiko yako yamewafikia asilimia ngapi ya watanzani?Tukichukua vijana 100,umri kati ya miaka 20-40 randomly,unadhani ni wangapi wanaweza kuelezea historia ya uhuru wa nchi yetu?Hapa namaanisha kwa mujibu wa unavyoelezea historia!
 
Mohamed Said kwa hiyo unaijua historia ya TANU ya watu wa kariakoo tu, siyo Tanganyika yote, huku Songea wana TANU walikuwa wanawajua Nyerere na Kambona na viongozi wa vyama vya ushirika tu maana ndio waliokuwa wanakuja kuwahamasisha watu, historia ya TANU ni pana sana haiishii kariakoo na magomeni tu, kuandika historia ya wazee wa kariakoo peke yake, hauwatendei haki wapigania uhuru wengine wa mikoani
Kweli kabisa,nimemweleza kasoro hiyo ya kuwa biased!Nadhani anajua zaidi ya hicho anachoandika ila anaamua tu kuelezea uoande mmoja kwa manufaa anayotaka yeye!
 
Unaamini maandiko yako yamewafikia asilimia ngapi ya watanzani?Tukichukua vijana 100,umri kati ya miaka 20-40 randomly,unadhani ni wangapi wanaweza kuelezea historia ya uhuru wa nchi yetu?Hapa namaanisha kwa mujibu wa unavyoelezea historia!
Bome...
Wangapi wamekisoma kitabu mimi sina namna ya kufahamu.

Hapa nimekueleza vipi kitabu changu kilivyopokelewa ndani na nje ya miaka ya Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa,nimemweleza kasoro hiyo ya kuwa biased!Nadhani anajua zaidi ya hicho anachoandika ila anaamua tu kuelezea uoande mmoja kwa manufaa anayotaka yeye!
Bome...
Inaelekea hujakisoma kitabu.

Nimeeleza TANU iliyoundwa Southern Province na Suleiman Masudi Mnonji, Salum Mpunga, Yusuf Chembera, Sheikh Mohamed Yusuf Badi, Shariffa bint Mzee kwa kuwataja wachache.

Nimeeleza historia ya TANU Central Province TANU ilivyoasisiwa na Omari Suleiman na Haruna Taratibu na wazalendo wengine.

Tanga - Hamisi Heri, Mohamed Kajembe, Sheikh Rashid Sembe na wengine.

Northern Province-Yusuf Olotu, Bi. Halima Selengia, Mama bint Maalim...

Sasa ikiwa unaona kuna pande mbili katika kuunda TANU nitafurahi ikiwa utaeleza historia ya huo upande mwingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni nyongeza:

Iddi Faizi Mafungo alikuwa Mwekahazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na pia Mwekahazina wa TANU.

Yeye ndiye aliyekabidhiwa kukusanya fedha za safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere UNO.

Ulikuwa unayajua haya?
 
Kweli kabisa,nimemweleza kasoro hiyo ya kuwa biased!Nadhani anajua zaidi ya hicho anachoandika ila anaamua tu kuelezea uoande mmoja kwa manufaa anayotaka yeye!
uko sahihi! nimempa mchango wa vyama vya ushirika kwenye harakati za kupigania uhuru, mpaka viongozi wa vyama vya ushirika wakapewa vyeo serikalini na kwenye baraza la mawaziri la tanganyika, lakini mohamed said anajifanya hajui mchango wake, kwa sababu sio miongoni mwa wapendwa wake anaowataka, anachofanya ni kuchagua wachache anaowataka yeye, hicho kitabu chake hakielezi historia yote ya TANU, bali ni historia ya wapendwa wake wachache ndani ya TANU.
 
Kabisa mkuu,nimeoma unavyomchallange lakini anakwepa!Mara aseme wengine nao waandike!Kama anataka historia iwe sawa,basi suala la kuchagua wapendwa wake ni lazima aliweke kando!Yaani mpaka watu waliojitolea kumpa Nyerere vitafunwa na mboga mboga ilimradi tu ni wa upande wake,basi kawaelezea kwa kina sana!
 
Laki...
Umesema kweli niliyoandika mimi ni historia ya TANU kuanzia wazee wangu walipounda African Association 1929 Kleist Sykes akiwa Katibu muasisi.

Alipofariki 1949 mwanae Abdul Sykes akawa katibu mwaka wa 1950 na Dr. Vedasto Kyaruzi akawa Rais.

Katika miongo hii miwili kutokea 1929 hadi 1950 kuna mengi muhimu yametendeka ambayo hamkuwa mnayajua mathalan mchango wa Hassan Suleiman na Ali Juma Ponda kama viongozi wa TAA Dodoma.

Halikadhalika hamkuwa mnajua mchango wa TAA Political Subcommittee iliyoundwa 1950 katika kupeleka mapendekezo ya katiba kwa Gavana Edward Twining.

Wala hamkuwa mnajua kuwa kamati hii ndani yake mmoja wa wajumbe alikuwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na "mjumbe," mwengine alikuwa Earle Seaton.

Unajua uhusiano wa watu hawa wawili na Abdul Sykes?

Unajua uhusiano wa TAA Political Subcommittee na hotuba aliyesoma Mwalimu Nyerere UNO 1955?

Ikiwa unayo historia ya TANU ambayo ni tofauti na hii inayoanza na vyama vya ushirika tuandikie tuisome.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabisa mkuu,nimeoma unavyomchallange lakini anakwepa!Mara aseme wengine nao waandike!Kama anataka historia iwe sawa,basi suala la kuchagua wapendwa wake ni lazima aliweke kando!Yaani mpaka watu waliojitolea kumpa Nyerere vitafunwa na mboga mboga ilimradi tu ni wa upande wake,basi kawaelezea kwa kina sana!
Bome...
Mimi sina tatizo na historia yoyote l ile ambayo iko kinyume na historia ya TANU kama niijuavyo.

Hii ndiyo husema muiandike historia yenu ili sote tufaidike.

Bahati mbaya hili la kuandika hamlipendi.

"Wapendwa," wangu hayo yote niliyoeleza hakika wamefanya lakini ikiwa hamuamini hakuna shida wako wanaoamini yote nisemayo.

Tuje kwenye "challenge," ya kitabu chenyewe.

Hiki kitabu sasa kina miaka 22 toka kichapwe anakuja mtu kukihoji leo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilishacomment huko nyuma na narudia tena...umekuwa unamlenga na kumtaja Mwalimu kama Mtu aliyezuka tu na kubebwa na unaowaita 'Wazee wako'.
Very nice, huyu mdini aliyekubuhu (Mohamed Said) amekua akim-potray Mwalimu Nyerere kuwa ni wakuja, hakustaarabika na hivyo ustaarabu alifundishwa na hao wazee wake, na nk.
 
Unataka tuamini ya kwamba harakati za kupigania uhuru wa nchi hii zilianza na kukamilishwa kwenye eneo moja tu ilihali nchi hii ni kubwa , na karibia kila jimbo kulikuwa na harakati/mawasiliano na kazi zilifanyika.
Si hilo tu, pia anapambana kuaminisha kuwa harakati za uhuru zilianzishwa na kukamilishwa na waislamu (yaani ukizungumza uhuru basi taja/tukuza uislamu)...Very stupid!
 
Very nice, huyu mdini aliyekubuhu (Mohamed Said) amekua akim-potray Mwalimu Nyerere kuwa ni wakuja, hakustaarabika na hivyo ustaarabu alifundishwa na hao wazee wake, na nk.
Automata,
Laiti mimi ningeandika kitabu cha Abdul Sykes kwa nia ya kumkanyaga Mwalimu Nyerere ningekiua kitabu changu.

Hayo yote uliyosema hayapo katika kitabu changu.

Kilichokuwapo na hili ndilo lililovutia wasomaji wengi katika kitabu ni kule kueleza kwa undani kabisa historia ya harakati za uhuru Nyerere akiwa bado hajafika Dar es Salaam na kufahamiana na Abdul Sykes.

Nini umuhimu wa Abdul Sykes?

Kwanza baba yake ndiye alikuwa kiongozi katika kuasisi African Association mwaka wa 1929 akiwa Katibu.

Pili ni mapinduzi aliyofanya yeye na Hamza Mwapachu 1950 ya kuwatoa madarakani uongozi wa wazee wakati huo Rais akiwa Thomas Saudtz Plantan ambae yeye ni baba yake Katibu akiwa Clement Mohamed Mtamila.

Tatu ni yeye na Dr. Vedasto Kyaruzi wakiwa sasa ni viongozi wa TAA wa kuchaguliwa kuunda TAA Political Subcommittee na Abdul kumtia Mwanasheria Earle Seaton ndani ya TAA kama mshauri kuhusu masuala ya nchi zilizokuwa chini ya udhamini wa Umoja wa Mataifa.

Abdul ili kuitia nguvu TAA akamtia Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Said Chaurembo ndani ya hiyo TAA Political Subcommittee kama wajumbe.

Jukumu kubwa la kamati hii ilikuwa kutengeneza mazingira ya kuunda chama cha siasa na Abdul akaanza mazungumzo na Chief Kidaha Makwaia wa Usukuma akimtaka ajiunge na TAA ili wamchague kuwa Rais na mwaka unaofuata waunde TANU na Chief Kidaha aongoze harakati za kupigania uhuru.

Mipango hii haikufanikiwa na ndipo mwaka wa 1952 Nyerere akaja Dar es Salaam na Kasella Bantu akampeleka nyumbani kwa Secretary na Act. President wa TAA Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Attachments

  • HAMZA MWAPACHU.jpg
    HAMZA MWAPACHU.jpg
    5.8 KB · Views: 2
  • THOMAS PLANTAN.jpg
    THOMAS PLANTAN.jpg
    16.4 KB · Views: 2
  • SHEIKH SAID CHAUREMBO.jpg
    SHEIKH SAID CHAUREMBO.jpg
    43.5 KB · Views: 2
  • SHEIKH HASSAN BIM AMEIR PORTRAIT.jpg
    SHEIKH HASSAN BIM AMEIR PORTRAIT.jpg
    17.8 KB · Views: 2
Si hilo tu, pia anapambana kuaminisha kuwa harakati za uhuru zilianzishwa na kukamilishwa na waislamu (yaani ukizungumza uhuru basi taja/tukuza uislamu)...Very stupid!
Automata,
Hakuna sababu ya matusi huu ni mjadala tu mimi nitakueleza niyajuayo nawe kama unalo la kuchangia lilete lakini usinitukane.

Hili la harakati za uhuru kuwa zilianzishwa na Waislam sijalisema mimi.

Ukisoma mswada wa maisha ya Kleist Sykes alioandika kabla hajafa mwaka wa 1949 anaeleza kuwa waasisi wa African Association wengi walikuwa Waislam kwa sababu Wamishionari walikuwa wakiwakataza waumini wao kujihusisha na siasa (Iliffe 1973).

Yako mengi lakini kwa kuwa nakuona umeghadhibika na umeenza matusi bora nisimame hapa.

Ukweli ni kuwa Nyerere hakwenda nyumbani kwa Abdul kumtaka waunde chama cha siasa.

Nyerere ameikuta TANU ipo katika fikra ya Abdul kwa miaka mingi fikra ambazo Abdul alizipata kutoka kwa baba yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom