Kuna tofauti kubwa kati ya alichoandika Msigwa na alichoongea Ndugai, ukiangalia kwa nje wote walionekana kutumia uhuru wao wa kutoa maoni.
Lakini kwa ndani zaidi, alichokiandika Msigwa kwa nafasi yake kama mpinzani hatakiwi kuwashauri CCM nani wa kumchagua.
Kwa sababu huyo atakayechaguliwa kuwa spika akianza kuwabeba CCM wenzake bungeni kwa maslahi yao, Msigwa kama mpinzani atakosa namna ya kumponda kwa kuwa atakuwa "alishajitega" kwa kumuunga mkono.
Lema aliona mbele zaidi kwa alichofanya.
CCM ni madikteta walimnyima Ndugai haki yake ya kuhoji jambo la msingi lenye maslahi kwa taifa, kukopa kwa taifa masikini kama letu lenye rasilimali zakutosha sio sifa, ni kuzidi kujidumaza akili.