I got you Ila Mwanamke ukimwambia ukweli mzee itakula kwako hata akiwa mkeo we endelea kumdanganya na anajua unamdanganya Ila atakaa nawe.
Yani huna hela halafu unamwambia Sina, kesho Sina, keshokutwa Sina, wallah utaona ule upendo unaanza kupungua. Surely I tell you. Yani heri hata ukakope umpe.
Suala la mwanaume kujithamini, kwanza lazima ujue sisi wanaume tunajithamini sana na ndio maana hatuwezi kukubali mwanamke ajihudumie au mwanamke wako ahangaike kutafuta pesa we ukae bure tu. Sababu kubwa ni kujithamini hatutaki kuletewa dharau.
Mwanamke anayekulisha au akinunua chakula wiki ya kwanza, ya pili, ya tatu ataanza kukusimanga tu aisee, jaribu kama una mke utaona. Jaribu tu utashangaa na simu yako anakuwa mzito kupokea na akirudi analalamika tu.
Hii ndio nature nadhani hata wao wanajilazimishaga tu Ila wanapenda pesa ya mwanaume aisee. Ndio maana pamoja mnafanya wote kazi Ila pesa yako ndio itatumika, pesa ya mwanamke inakuwa kama ya kuziba viraka tu na sijui wanapelekaga wapi.
Hata uoe mtoto wa tajiri atataka umuhonge mapesa aishi kama kwa babake tu, Hawa wanawake wape pesa tu mengine wajipange wao. Kama anakupenda kweli ajipange kweli lakini we mpe pesa na usiache kumpa pesa hata akizeeka.