Tusidanganye, Rest in Peace (RIP) haipatikani bure; lazima uishi maisha mema kwanza

Tusidanganye, Rest in Peace (RIP) haipatikani bure; lazima uishi maisha mema kwanza

Yohana 8
1 [Walikwenda kila mtu nyumbani kwake; naye Yesu akaenda mpaka mlima wa Mizeituni.

2 Hata asubuhi kulipokucha akaingia tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; naye akaketi, akawa akiwafundisha.

3 Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati.

4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini.

5 Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje?

6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi.

7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.

8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi.

9 Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati.

10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?

11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]

12 Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.

13 Basi Mafarisayo wakamwambia, Wewe unajishuhudia mwenyewe; ushuhuda wako si kweli.

14 Yesu akajibu, akawaambia, Mimi ningawa ninajishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ndio kweli; kwa sababu najua nilikotoka na niendako; lakini ninyi hamjui nilikotoka wala niendako.

15 Ninyi mwahukumu kwa kufuata mambo ya mwili; mimi simhukumu mtu.

16 Nami nijapohukumu, hukumu yangu ni kweli; kwa kuwa mimi si peke yangu, bali ni mimi na yeye aliyenipeleka.

17 Tena katika torati yenu imeandikwa kwamba, Ushuhuda wa watu wawili ni kweli.

18 Mimi ndimi ninayejishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenipeleka ananishuhudia.

19 Basi wakamwambia, Yuko wapi Baba yako? Yesu akajibu, Mimi hamnijui, wala Baba yangu hammjui; kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba yangu.

20 Maneno hayo aliyasema alipokuwa akifundisha hekaluni, katika chumba cha hazina; wala hakuna mtu aliyemkamata, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado.

21 Basi akawaambia tena, Mimi naondoka, nanyi mtanitafuta; nanyi mtakufa katika dhambi yenu; mimi niendako ninyi hamwezi kuja.

22 Basi Wayahudi wakasema, Je! Atajiua! Kwa kuwa asema, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja?

23 Akawaambia, Ninyi ni wa chini, mimi ni wa juu; ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu.

24 Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu.

25 Basi wakamwambia, U nani wewe? Yesu akawaambia, Hasa neno lilo hilo ninalowaambia.

26 Ninayo mengi ya kusema na kuhukumu juu yenu; lakini yeye aliyenipeleka ni kweli, nami niliyoyasikia kwake, ndiyo ninenayo katika ulimwengu.

27 Wala hawakutambua ya kuwa anawatajia Baba.

28 Basi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye; na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba alivyonifundisha ndivyo ninenavyo.

29 Naye aliyenipeleka yu pamoja nami, hakuniacha peke yangu; kwa sababu nafanya sikuzote yale yampendezayo.

30 Naye alipokuwa akisema hayo, wengi walimwamini.

31 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;

32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.

33 Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru?

34 Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.

35 Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote.

36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.

37 Najua ya kuwa ninyi ni uzao wa Ibrahimu lakini mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halimo ndani yenu.

38 Niliyoyaona kwa Baba ndiyo niyanenayo; nanyi vivyo hivyo mliyoyasikia kwa baba yenu ndiyo myatendayo.

39 Wakajibu, wakamwambia, Baba yetu ndiye Ibrahimu! Yesu akawaambia, Kama mngekuwa watoto wa Ibrahimu, mngezitenda kazi zake Ibrahimu.

40 Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya hivyo.

41 Ninyi mnazitenda kazi za baba yenu. Ndipo walipomwambia, Sisi hatukuzaliwa kwa zinaa; sisi tunaye Baba mmoja, yaani, Mungu.

42 Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu, mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, nami nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma.

43 Mbona hamyafahamu hayo niyasemayo? Ni kwa sababu ninyi hamwezi kulisikia neno langu.

44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.

45 Nami, kwa sababu nasema iliyo kweli, hamnisadiki.

46 Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki?

47 Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.

48 Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Je! Sisi hatusemi vema ya kwamba wewe u Msamaria, nawe una pepo?

49 Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini mimi namheshimu Baba yangu, na ninyi mwanivunjia heshima yangu.

50 Wala mimi siutafuti utukufu wangu; yuko mwenye kutafuta na kuhukumu.

51 Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele.

52 Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng'amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.

53 Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?

54 Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu.

55 Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nalishika.

56 Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.

57 Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu?

58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.

59 Basi wakaokota mawe ili wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni.
😔
 
Mtu mwenyewe anajichanganya, mara tumwabudu Yesu, mara Yesu ni Mungu, mara bila Yesu hatuwezi fika kwa Mungu ilimradi tafrani
Sikupenda kutoa elimu hii ya ndani sana kwa leo, lakini sina budi kufanya hivyo. Naomba nianze kueleza kwa kina kwanini tunasema Yesu ni Mungu. Vitabu vitakatifu vimeeleza wazi kwamba Yesu ni Mungu. Na hizi ndio sababu kuu zinazothibitisha kwamba Yesu ni Mungu.

1. YESU ALIKUWEPO KABLA YA KUZALIWA
Ufuatao ni ushahidi wa kibiblia kwamba YESU KRISTO ni Mungu.
Yohana 8:58
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye IBRAHIMU ASIJAKUWAKO, MIMI NIKO.
NIKO ni jina la Mungu peke yake. Tunakutana na jina hilo pale Musa alipoongea na Mungu na kutumwa kuwakomboa wana wa Israeli kutoka Misri. Imeandikwa:
Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n’nani? Niwaambie nini? Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO (Kutoka 3:13-14).
Mwanadamu yuko kwa sababu Mungu alisababisha awepo. Gari liko kwa sababu injinia au mbunifu alisababisha liwepo. Nyumba ipo kwa sababu fundi alisababisha iwepo. Lakini Mungu YEYE YUKO TU!! Hayupo kwa kusababishwa na yeyote! Ndiyo maana akasema MIMI NIKO AMBAYE NIKO! Yesu ni NIKO. Kwa hiyo, Yeye ni Mungu.

2. YESU NA BABA NI WAMOJA
Yohana 10:30
Mimi na Baba tu umoja.
Waislamu wana msemo wao kwamba eti, Yesu na Mungu ni wamoja katika malengo, si katika asili yao. Basi huwa nawauliza swali kuhusu aya ifuatayo ya Isaya, nao wanazimika na kukosa jibu:
Isaya 9:6
Maana kwa ajili yetu MTOTO amezaliwa, Tumepewa MTOTO MWANAMUME; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, MUNGU MWENYE NGUVU, BABA WA MILELE, Mfalme wa amani.
Aya hii iko wazi kabisa. anayetajwa ni Yesu kwamba Yeye ni Mungu mwenye nguvu.
Yohana 14:9
Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? ALIYENIONA MIMI AMEMWONA BABA; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?
Maneno haya Yesu aliyasema baada ya kuulizwa swali lililo wazi kabisa, ambalo lilikuwa na lengo la kumjua MUNGU BABA! Imeandikwa: Filipo akamwambia, Bwana, UTUONYESHE BABA, yatutosha. Ndipo Yesu akajibu waziwazi: ALIYENIONA MIMI AMEMWONA BABA. Maana yake ni kuwa, “Mimi ndio Baba mwenyewe.”

3. YESU NI MWANZO NA MWISHO
Ufunuo 1:17 na Ufunuo 22:13
Mimi ni wa kwanza na wa mwisho
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
Ni Mungu TU ndiye mwenye uwezo wa kuwa wa kwanza na wa mwisho; Yesu ni Alfa na Omega. Kwa hiyo Yeye ni Mungu.

4. YESU NI NENO
Yohana 1:1
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye NENO ALIKUWA MUNGU.
Andiko hili Waislamu hawalipendi kabisa. ni kwa sababu liko wazi mno. Yesu ni Neno; na Neno ni Mungu; hivyo, Yesu ni Mungu!

5. THOMASO AKIRI KUWA YESU NI MUNGU, NA YESU HAKUKATAA KUITWA MUNGU
Yohana 20:28
Tomaso akajibu, akamwambia, BWANA WANGU NA MUNGU WANGU!
Tomaso aliposema hivi, Bwana Yesu hakukanusha na kusema, “Mimi sio Mungu.” Badala yake: Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki. (Yoh 20:29).
Kama Thomaso alikuwa muongo, kwanini Yesu hakukataa kuitwa Mungu. Imani zote zinakiri kuwa Yesu hakufanya dhambi na hakuwa na dhambi.

6. DAMU YA YESU INAMAMLAKA
Matendo 20:28
Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake MUNGU, ALILOLINUNUA KWA DAMU YAKE MWENYEWE.
Ni Mungu gani mwenye damu huyu? Jibu liko wazi. Huyu ni Yesu Kristo. Huyu ndiye aliyetoa uhai wake na kumwaga damu yake msalabani; na hapo ndipo alipoanzisha Kanisa.

7. KATIKA YESU, KILA KITU KILIUMBWA

Wakolosai 1:16
Kwa kuwa KATIKA YEYE VITU VYOTE VILIUMBWA, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.
Katika Yeye Yesu vitu vyote viliumbwa. Ina maana kuwa vitu vyote vilitokana na Yesu; maana Yesu ni Neno la Mungu. Na tunajua kuwa Muumba wa vitu vyote ni Mungu; hivyo, Yesu ni Muumba – Yeye ni Mungu!!

8. KATIKA YESU, UNAKAA UTIMILIFU WA MUNGU
Wakolosai 2:9
Maana KATIKA YEYE UNAKAA UTIMILIFU WOTE WA MUNGU, kwa jinsi ya kimwili.
Sisi sote ni watu wasio wakamilifu. Tunaanguka tena na tena kwenye dhambi. Kwa hiyo, hakuna mwanadamu wa kawaida ambaye anaweza kujigamba kwamba yeye ametimia kama alivyo Mungu. Lakini katika Yesu “utimilifu WOTE wa Mungu unakaa.” Kwa nini? Kwa sababu Yeye ndiye Mungu huyohuyo.

9. YESU NI MUNGU PAMOJA NASI “EMMANUEL”
1Timotheo 3:16
Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. MUNGU ALIDHIHIRISHWA KATIKA MWILI, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
Ni Mungu gani aliyedhihirishwa katika mwili? Jibu liko wazi. Ni Yesu Kristo peke yake.

10. YESU NI MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU
Tito 2:13
….tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa KRISTO YESU, MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU
Yesu Kristo ni Mungu Mkuu!!
 
Ukristo una contradictions nyingi sana nikikuwekea hapa huwezi kumaliza kuzitatua.

Ukitaka kuhubiri dini yako hubiri kwa upole, usihubiri kwa kutufokea tumuabudu huyo Yesu wako sisi wengine tunamuona ni mtu aliyekosa maadili tu.

Huwezi kuthibitisha kwamba kuna hukumu baada ya kifo.

Kama unabisha, thibitisha.
Naomba nithibitishe ifuatavyo:
Soma hili andiko mpaka mwisho:

Luka 16.22 “Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.

23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.

24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.

25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.

26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.

27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,

28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.

29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.

30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu

31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu”.
 
Naomba nithibitishe ifuatavyo:
Soma hili andiko mpaka mwisho:

Luka 16.22 “Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.

23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.

24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.

25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.

26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.

27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,

28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.

29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.

30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu

31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu”.
Sasa hapa umethibitisha nini?
 
Baada ya kusema tumuabudu Mungu wewe unasema tumuabudu Yesu, haya endelea kumuabudu Yesu kama utapata hiyo Rest in peace.
 
Baada ya kusema tumuabudu Mungu wewe unasema tumuabudu Yesu, haya endelea kumuabudu Yesu kama utapata hiyo Rest in peace.
Hata huyo Mungu hakuna anayeweza kuthibitisha yupo kweli, habari za kuwepo kwa Mungu ni hadithi za uongo za kutungwa na watu tu.

Ukibisha, thibitisha Mungu yupo.
 
Hicho kilicho andikwa hapo ndicho kinacho tokea baada ya kifo. Aliyetenda mema anaenda peponi na ambaye hakutenda mema anaenda kuzimu kwenye mateso.
Hujathibitisha lolote linatokea baada ya kifo.

Umeleta mahubiri ya kidini tu.

Tatizo hujui tofauti ya uthibitisho na mahubiri ya kidini.
 
Hata huyo Mungu hakuna anayeweza kuthibitisha yupo kweli, habari za kuwepo kwa Mungu ni hadithi za uongo za kutungwa na watu tu.

Ukibisha, thibitisha Mungu yupo.
Hivi kwa uonavyo wewe huu ulimwengu umekuja tu kwa bahati mbaya?
 
Hivi kwa uonavyo wewe huu ulimwengu umekuja tu kwa bahati mbaya?
Kwa nini swali lako limekuwa umekuja tu kwa bahati mbaya? Kwa nini bahati mbaya? Kwa nini unafikiri umekuja at all? Umekuja kutoka wapi? Kilichosababisha uje ni kipi?
 
Hujathibitisha Mungu yupo. Thibitisha.

Ulimwengu kuwapo na sisi kutojua umekuwapo vipi si uthibitisho kwamba umewekwa hapa na Mungu.

That is a logical non sequitur fallacy.

Unatakiwa kuthibitisha Mungu yupo na ndiye kaumba ulimwengu.
 
Hujathibitisha Mungu yupo. Thibitisha.

Ulimwengu kuwapo na sisi kutojua umekuwapo vipi si uthibitisho kwamba umewekwa hapa na Mungu.

That is a logical non sequitur fallacy.

Unatakiwa kuthibitisha Mungu yupo na ndiye kaumba ulimwengu.
Siwezi kukuthibitishia uwepo wa Mungu ila tunatambua uwepo wa Mungu kupitia ishara zake kama mwenyewe Mungu alivyosema kwamba tutamtambua yeye kupitia ishara zake na ishara za uwepo wake zipo nyingi sana. Suala la Mungu lipo kiimani zaidi, huwezi kumuona Mungu kwenye maisha haya duniani ila ameahidi kuna siku tutamuona live bila chenga na hii ni baada ya kufa utaenda kuona huko kama unayoamini ni sahihi au siyo.
 
Siwezi kukuthibitishia uwepo wa Mungu ila tunatambua uwepo wa Mungu kupitia ishara zake kama mwenyewe Mungu alivyosema kwamba tutamtambua yeye kupitia ishara zake na ishara za uwepo wake zipo nyingi sana. Suala la Mungu lipo kiimani zaidi, huwezi kumuona Mungu kwenye maisha haya duniani ila ameahidi kuna siku tutamuona live bila chenga na hii ni baada ya kufa utaenda kuona huko kama unayoamini ni sahihi au siyo.
Unajuaje hii ni ishara ya Mungu na si kitu tofauti tu ambacho wewe unafikiri ni ishara ya Mungu?

Unaweza kuitaja ishara moja ya Mungu tuichambue hapa na kuona kama kweli ni ishara ya Mungu na si hadithi za kuungwaungwa na watu tu?
 
Unajuaje hii ni ishara ya Mungu na si kitu tofauti tu ambacho wewe unafikiri ni ishara ya Mungu?

Unaweza kuitaja ishara moja ya Mungu tuichambue hapa na kuona kama kweli ni ishara ya Mungu na si hadithi za kuungwaungwa na watu tu?
Utofauti wa lugha
 
Acheni kiburi cha uzima, mwabuduni Yesu Kristo. Siku za mwisho zipo karibu. Hapa duniani tunapita. Miaka ya kuishi ya mwanadamu ni 60 hadi 80, baada ya hapo anakufa.

Baada ya kifo, ndio mwanzo wa hukumu unaanza hapo. Rest in Peace haipatikani bure; lazima mtu aingie gharama ya kuishi maisha ya kumpendeza Mungu aliyeziumba mbingu na nchi. Maisha yale aliyoyaishi Yesu Kristo. Huwezi kuacha dhambi bila kumfuata Yesu Kristo. Huwezi kuacha dhambi kwa kujiongoza mwenyewe.

Dini za Kiafrika zilikosa sifa ya maisha matakatifu, haziwezi kumpeleka mwanadamu kwenye Rest in Peace. Tubuni ingali bado ni wazima wa afya. Msijifanye welevu wakati hata siku za kuzaliwa kwenu mlikuwa hamzijui. Je, mlijua mtazaliwa lini? Tumwabudu Yesu Kristo.

Yesu ndio njia ya kweli na uzima. Ndiye atakayekufanya mawazo yako yawe mazuri na matakatifu, maneno yako yawe mazuri na matakatifu, na matendo yako yafae mbele za Mungu aliyeziumba mbingu na nchi. Ndiye pekee atakayekufanya uingie peponi, mahali penye amani. Mtu anayestahili Rest in Peace ni mtu yule aliyefanikiwa kufuata maisha ya Yesu Kristo pekee.

Mbali na hivyo, mtu huyo lazima aende kuzimu, kwenye giza na mateso, huku akisubiri hukumu yake ya mwisho. Tuache kiburi. Ukweli ndio huo. Kazi kwako; kupanga ni kuchagua.

Don't take everything serious bro, vingine vimeundwa kupunguza machungu tu maisha yaende na kupunguza psychological stress wakati wa msiba, kufariji wafiwa tu msiba uishe. Hutayaweza yote ya dunia ukitaka majibu yake...
 
Utofauti wa lugha unathibitisha vipi Mungu yupo?
Kama ulimwengu ungekuwa umetokea pasipo kujulikana basi amini nakwambia pasingekuwapo kitu kinachoitwa lugha kwa wanadamu tungekuwa kama wanyama tu, hebu angalia lugha za jamii tofauti tofauti za wanadamu zilivyo na mpangilio halafu tafakari vizuri ujiulize ni nani alizipangilia hizi lugha, na kwanini wewe kuna lugha unazijua na zingine huzijui.
 
Acheni kiburi cha uzima,
Kwani kuna aliyetaka kuzaliwa kwenye hii Dunia iliyojaa shida za kila aina?

Hakuna aliyetaka huo uzima.
mwabuduni Yesu Kristo.
Huyo Yesu akiabudiwa anafaidika nini?

Huyo Yesu asipo abudiwa atapata kwashakoo au?
Siku za mwisho zipo karibu. Hapa duniani tunapita. Miaka ya kuishi ya mwanadamu ni 60 hadi 80, baada ya hapo anakufa.
Hakuna siku za mwisho.

Siku ya mwisho ni siku yako ya kufa wewe peke yako.

Dunia haina mwisho. Ulizaliwa umeikuta, Utakufa utaiacha.
Baada ya kifo, ndio mwanzo wa hukumu unaanza hapo.
Ulishawahi kufa ukajua kwamba kuna hukumu siku ya mwisho?

Au unaleta imani na hofu zako uchwara ulizo pumbazwa na kuaminishwa na dini yako?
Rest in Peace haipatikani bure; lazima mtu aingie gharama ya kuishi maisha ya kumpendeza Mungu aliyeziumba mbingu na nchi.
Hakuna Mungu aliyeumba chochote kile.

Huyo Mungu mmemtunga vichwani mwenu tu, Na wala huwezi kuthibitisha uwepo wake.

Mungu hajawahi kuwepo, Mungu hayupo na hatakaa awepo
Maisha yale aliyoyaishi Yesu Kristo. Huwezi kuacha dhambi bila kumfuata Yesu Kristo. Huwezi kuacha dhambi kwa kujiongoza mwenyewe.
Kama tayari Yesu alishakufa kwa ajili ya dhambi zetu na kulipa yote, Kwa nini arudi tena kutuhukumu kwa dhambi ambazo tayari alishazifia na kulizipia?

Hivi huyo Yesu wako anajielewa kweli?
Dini za Kiafrika zilikosa sifa ya maisha matakatifu, haziwezi kumpeleka mwanadamu kwenye Rest in Peace.
Unathibitisha vipi dini za kiafrika zilikosa sifa ya maisha matakatifu na haziwezi kumpeleka mwanadamu kwenye uzima wa milele?

Au ndivyo ulivyo pumbazwa na dini yako uchwara ya kikristo?
Tubuni ingali bado ni wazima wa afya. Msijifanye welevu wakati hata siku za kuzaliwa kwenu mlikuwa hamzijui. Je, mlijua mtazaliwa lini? Tumwabudu Yesu Kristo.
Kwani kuna aliyeomba au aliyetaka kuzaliwa?
Yesu ndio njia ya kweli na uzima. Ndiye atakayekufanya mawazo yako yawe mazuri na matakatifu, maneno yako yawe mazuri na matakatifu, na matendo yako yafae mbele za Mungu aliyeziumba mbingu na nchi. Ndiye pekee atakayekufanya uingie peponi, mahali penye amani. Mtu anayestahili Rest in Peace ni mtu yule aliyefanikiwa kufuata maisha ya Yesu Kristo pekee.

Mbali na hivyo, mtu huyo lazima aende kuzimu, kwenye giza na mateso, huku akisubiri hukumu yake ya mwisho. Tuache kiburi. Ukweli ndio huo. Kazi kwako; kupanga ni kuchagua.
Yesu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.

Shetani hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.

Allah hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.

Mbingu haijawahi kuwepo, haipo na haitakaa iwepo.

Kuzimu hakujawahi kuwepo, hakupo na hakutakaa kuwepo.

If you fail to live on earth 🌎 the fantasy of heaven is an illusion.
 
Back
Top Bottom