Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Hicho unachosema ndio ukweli, lakini ukweli mwingine ukisemwa sio ukweli kwako!Dogo hasira za uchaguzi 2020 zinahusiana vipi na ukweli huu?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hicho unachosema ndio ukweli, lakini ukweli mwingine ukisemwa sio ukweli kwako!Dogo hasira za uchaguzi 2020 zinahusiana vipi na ukweli huu?
Unajua serikali ya enzi za Mwalimu ilivyokua au una ota mkuu.?Yaani hawa wanaChadema waliogwuza bunge ndio iwe msaada kwa watanzania?
Acheni kudanganya umma bana. Mbona akina Njelu kasaka na wenzao waliweza kuikosao na kuisimamia serikali wakati wa chama kimoja.
Ishu ya msingi ni kuwa na wazalendo na wenye uchungu na taifa letu.
Mnadai kuna demokrasia ili hali pesa za umma zinaliwa.
Pumba tupuUnajua serikali ya enzi za Mwalimu ilivyokua au una ota mkuu.?
Nchi hii ilipata uhuru Dola Moja ikiwa inakaribiana sana na sh.ya Tanganyika.
Nchi ilikua na uchumi sawa na India , China , Indonesia ,Korea n.k. Bunge la Chama kimoja likalemaa Vyama vya ushirika vikafa, nyumba za serikali zikauzwa , Wahindi wakatiwa Mashamba ya Katani nchi nzima , Wahindi wakauziwa VIWANDA vyote wakahamishia Kenya na India, Wahindi wakakabidhiwa nyumba za NHC Kwa pango kama la Chumba kimoja Sinza. Chama kimoja na Bunge lake linalolindana na Mawaziri likaua TTCL , ATC wakati huo, TRC wakati huo, VIWANDA vya sementi vikafa wakati ambao ujanzi umeshamiri bara Zima la Afrika, Kiwanda Cha Matairi kikafa wakati ambao wananchi wengi wanamiliki magari binafsi na serikali inaagiza makumi Elfu ya magari. Chama kimoja na serikali yake wakaua Benki ya NBC mpaka Mwalimu akahoji lini Benki hiyo imapata hasara.! Wakamkoromea Mwalimu ili walindane na kujikea hisa kwanye makampuni?
Wakuza Kilimanjaro Hotel Kwa Bei ya Kiwanja chini ya Bunge la Chama kimoja !
Wakalindana kati ya Bunge na serikali.
Mama Samia ni Mwadilifu asiyewaza sana kujilimbikizia Mali za umma. Mwacheni aimarishe Demokrasia ili wananchi wakiona CCM haifai waikatae wachague Chama kingine. Watu wataogopa kuiba Kwa wazi Mali za umma. Hebu fikiri Chadema ikifanikiwa kuingia madarakani watakavyowabana waliokwapua Mali za umma au kuwatoa kabisa kwenye reli ya siasa wezi kama alivojaribu Magufuli akazidiwa na CCM wenyewe.
Kosa alilofanya Magufuli lilipangwa kijanja sana Kwa kumdanganya kuwa adui zake ni wapinzani kumbe adui mkubwa wa nchi hii wapo ndani ya CCM.
Pakiwa na Demokrasia vyama vitajipambanua kati ya Wanaopinga ufisadi na wanaojenga mifumo ya kifisadi.
Leo hii Kuna kundi lilipaswa liwa lina Chama chao Cha siasa ,hasa kundi linalounga mkono harakati za kubana matumizi ya serikali na kujenga uchumi wa watu wa chini katika misingi ya usawa. Kundi linguine ni lile la walamba asali ambao wapo ndani ya CCM na Vyama vingine pia. Hawa walitakiwa waamua Moja kuwa upande wa kulia au Kushoto.
Chini ya Bunge la Chama kimoja serikali inakua ya kinafiki na wanafiki wanakuwa wengi kuanzia wananchi mpaka watawala. Watu wanalindana Kwa maslahi binafsi.
Demokrasia ikikomaa uadilifu unakua mkubwa na Mali za umma zinaheshimiwa. Kwa Sasa watu wanajipanga kuiba Mali za umma kuanzia kule kwenye vikao vya madiwani Halmashauri mpaka Bungeni . Wabunge wanahongwa na matajiri wanazibwa midomo na serikali na kujipemdekeza ili Mwenyekiti awaone na kuwateua watoto wao na wake zao.
Kiufupi Bunge la Chama kimoja linafaa tu Kwa Serikali ya Kidikteta Kwa sababu dikteta atanatumia Bunge kama muhuri TU wa kupitisha mipango yake iwe mizuri au mibaya
Awamu ya Tano ilileta tafsiri mbaya sana ya neno 'uzalendo' inabidi BAKITA waingilie kati. Yaani mliaminishwa kuwa Uzalendo ni kukubaliana na kuunga mkono fikra zote za raisiYaani hawa wanaChadema waliogwuza bunge ndio iwe msaada kwa Watanzania?
Acheni kudanganya umma bana. Mbona akina Njelu kasaka na wenzao waliweza kuikosao na kuisimamia serikali wakati wa chama kimoja.
Ishu ya msingi ni kuwa na wazalendo na wenye uchungu na taifa letu.
Mnadai kuna demokrasia ili hali pesa za umma zinaliwa.