Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,170
- 6,757
Viongozi wetu najua mna nia njema kabisa ya kutaka kukuza lugha yetu ya taifa, Kiswahili.
Pamoja na kuwa na nia njema ya kukuza lugha ya Kiswahili tuwe wakweli kuwa majaji na mahakimu kutumia kiingereza kama lugha ya kurekodi kumbukumbu za mwenendo wa kesi sio sababu ya kunyima raia haki zao.
Mnataka kutuambia viongozi wetu hamjui kabisa kuwa, rushwa, vyombo vya ulinzi na usalama vilivyokosa maadili na watumishi wasiowaadilifu ndio chanzo cha kukosa haki kwa wananchi?
Mfano tunajua kabisa haki jinai huwa inaanzia polisi ambao ni wachunguzi,jalada linaenda kwa DPP ili aendeshe mashitaka na kisha mahakama kutoa haki. Je, ni kwa nini magereza yamejaa karibu 50% ya wafungwa na mahabusu ambao wamebambikiwa kesi?
Ndugu viongozi wetu mmekaa na kujiuliza kwa nini kuna watu wengi wapo uraiani lakini walifanya makosa waliyostahili kufungwa? Japokuwa sio vizuri kuwataja ila wapo wengi.
Hivyo basi ni wazi kuwa hukumu kutolewa kiswahili au kiingereza sio sababu ya kutoa haki kama mnavyotafuta sababu.
Mutu kama hajaonewa kama anayohaki yake iwe kwenye lugha ya kiswahili au kiingereza ataipata hiyo haki yake tu.Hata kama ni gharama kupata wakili ili aweze kutafsiri na kuandaa nyaraka za kesi, ukweli ni kuwa lugha haiwezi kumpatia mutu haki yake.
Namaliza kusema kuwa haki za wananchi wengi zinapotezwa na polisi wanaoshindwa kupeleza kwa ukweli na kuithibitishia mahakama bila shaka kama mtu ni mkosaji. Pia mahakimu wala rushwa na wasiosimamia misingi ya kazi yao,ambao kazi yao ni kuonea watu kwa kuwafunga huku hawajafanya makosa,kisa tu wawafuraishe polisi.
Tutaandika hukumu kwa kiswahili lakini haki za Wananchi zitaendelea kupotea kama viongozi hamtaki kung'oa mzizi wa tatizo.