Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Tumeshuhudia uchaguzi uliojaa uchafu wa kila aina, kuanzia kanuni za hovyo kabisa za kusimamia uchaguzi, uandikishaji wa wapiga kura bandia, uenguaji wa wagombea, mpaka utengenezaji wa kura bandia, kamatakamata ya wanaozuia kura za wizi, mpaka mauaji ya wanaoonekana ni kikwazo dhidi ya uovu wa kupokonya maamuzi ya wananchi.
Lengo la haya yote, ni kuwanyima haki wananchi ya kuwachagua viongozi wanaowataka. Watawala wameamua wawape wananchi watu wa kuwatawala.
Hawa viongozi walioletwa na watawala ili wawatawale wananchi, utiifu wao ni kwa aliyewapa hizo nafasi, kamwe hawawezi kuwa na wananchi, kamwe hawawezi kuwatetea wananchi. Wananchi watambue kuwa wameletewa vibaraka wa watawala ambao jukumu lao kubwa ni kutekeleza matakwa ya waliowateua.
Huu ni ukoloni mpya wa watu weusi dhidi ya weusi wenzao. Akina Chabruma, Mkwawa, Isike, Mirambo, japo hawakuwa na elimu, lakini walipambana kwa mioyo yao yote kuukataa ukoloni. Leo pamoja na elimu zetu za kwenye makaratasi, tumeshindwa kupambana na ukoloni mbaya zaidi kuliko hata ule wa mzungu.
Hata katika unyonge mbaya kabisa, tunastahili kuupinga ukoloni huu mpya.
Yeyote anayezuia wananchi kuwachagua viongozi wanaowataka, ni adui yetu, ni adui wa Taifa, kupambana dhidi yake kwa namna yoyote inayowezekana ni halali.