Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kuitana "mama yangu", "baba yangu", "mdogo wangu", "kaka yangu", "dada yangu", "shangazi yangu", "shemeji yangu" na vyeo vingine kama hivyo katika shughuli za siasa na umma ni utamaduni mpya uliovuka mipaka, kushika kasi na sasa unaanza kukomaa.
Zamani vyeo vya kifamilia ambavyo nilikuwa nimevizoea ni "mzee" ikasogea mbele kidogo ikawa "kaka" kwa wingi, sijui wanasiasa wamegundua nini sasa hivi idadi kubwa kama sio karibia wote wanaitana kwa vyeo vya kifamilia katika shughuli zote za umma.
Rudini kwenye mtindo wenu wa zamani tu wa kuitana ndugu, komredi na kamanda. Utamaduni mpya sasa unapelekea viongozi wadogo kuanza kujimilikisha viongozi wa umma wakubwa kama mama au baba zao jambo ambalo sio sahihi.
Japo inaweza kuonekana ni kama uungwana fulani bado sio sahihi kabisa viongozi kuanza kuitana na kuchukuliana kwa mfumo huo wa kifamilia kwa sababu itapeleka kuwa vigumu kuwajibishana, itazidisha tabia ya kuchukulia uongozi kwa mazoea na pia itapelekea kupeana nafasi na fadhili(favours) isivyostahili.