Tusifanye swala la El nino kuwa la kisiasa, tusiwabeze TMA

iMind

Platinum Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
3,224
Reaction score
5,514
Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na mijadala mingi kuhusu tahadhari ya mvua za El Niño iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA). Baadhi ya wananchi wameanza kuibeza TMA na hata Serikali kwa sababu mvua zilizotabiriwa kuanza mwanzoni mwa Oktoba hazijanyesha katika maeneo mengi nchini. Wengine wamekwenda mbali zaidi na kuligeuza suala hili kuwa la kisiasa. Ni muhimu tukatambua kwamba utabiri wa hali ya hewa ni suala la kisayansi, si la kisiasa. TMA haizalishi mvua, bali hutumia taarifa na mifumo ya kisayansi kutabiri mwenendo wa hali ya hewa ili kutuwezesha kuchukua tahadhari mapema.

Tunapaswa kuelewa kwamba utabiri si ahadi kwamba mvua zitanyesha siku fulani kwa uhakika wa asilimia 100. Hali ya hewa inaathiriwa na mifumo mingi ya kiasili ambayo inaweza kubadilika. Aidha, TMA ilieleza kuwa mvua zingeanza katika baadhi ya maeneo mwishoni mwa Septemba na mwanzoni mwa Oktoba, kisha kusambaa taratibu katika maeneo mengine, huku ongezeko kubwa likitarajiwa mwezi Novemba. Kwa hiyo, kuchelewa kwa mvua katika baadhi ya maeneo hakumaanishi moja kwa moja kwamba utabiri wote umekosewa. Bila shaka, wananchi wana haki ya kuhoji na kupata ufafanuzi kutoka TMA, lakini kuhoji kwa hoja ni tofauti na kubeza taaluma na wataalamu wetu.

Ni bora kuchukua tahadhari na mvua zisije kuliko kupuuza tahadhari halafu maafa yatokee. Gharama ya kujiandaa mapema inaweza kuwa ndogo sana ikilinganishwa na madhara ya mafuriko, uharibifu wa miundombinu na upotevu wa mali na maisha ya watu. Tuendelee kuihimiza TMA kutoa taarifa za mara kwa mara, kueleza mabadiliko ya utabiri na kuelimisha wananchi. Wakati huohuo, Serikali na wananchi waendelee na maandalizi badala ya kulegeza tahadhari. Tusiruhusu tofauti zetu za kisiasa zitufanye tudharau sayansi, tupuuze wataalamu wetu au tuweke maisha ya wananchi hatarini
 
"Elimu ,Elimu Elimu " Lowassa alisema .

Hii nchi ina wajinga wengi sana mkuu
 
Mkuu ulichosema sahihi ila ,hili swala limekuja kuonekana katika upande wakisiasa baada ya kutizama namna serikali inaendesha mambo ,tujiulize miaka ya Magufuli kuna utabiri ulikuwa ukiwekwa unatizamwa kwa mlango wakisiasa , shida sio kwamba elimu hawana ila kila jambo sasa limekaa kutuliza mambo Flan ,bila wanachi kujenga imani na serikali yao hakuna jambo tunaweza litizama kwa mlango wa maslahi ya taifa .
#Professor shivj alisem mwaka huu serikali yetu haina uwajibikaji#
#Professor shivj tenha huyu hyu akasema serikali yetu inafanya mambo kimaficho # inakosa kuaminika na ndo chanzo cha haya yote tusitafute mchawi na tunajua ninan.
 
Naona kabisa hii El nino itakuwa fursa kwa content creator yaan bongo tuna masihara san
 
TMA wako Sahihi Kwa utabiri wao. Ila Mungu ana nafasi yake muhimu Kwa maisha. El nino haikutabiriwa kutuletea baraka, Bali maafa. Goti lilipigwa na linaendelea kupigwa.
 
Back
Top Bottom