Tusijidanganye kutatua tatizo la uchumi na ajira bila kuhakikisha walau 70% ya bidhaa tunazozitumia tunazalisha wenyewe

Wala kwa sasa hakuna haja ya kuwatafuta Wachina watufunze ili hali kuna mengi bado tunaweza kujifunza wenyewe.

Na tuna Watu waliosoma uhandisi wa mitambo mbalimbali, hivi iweje hata hawana uwezo wa kushauri Watu kutengeneza mashine ndogo ndogo tu za nyumbani?

Kuna comment nimetoa mfano wa bidhaa kama soksi, mikanda ya kiunoni, nguo za ndani n.k....hivi hatuwezi kuwaongezea ujuzi wale kina Mama wanaofuma Masweta wakafuma na soksi zitakazofikia walau 70% ya ubora kama zile zinazotoka nje?.

Bidhaa yoyote ikipokelewa kwa wingi na jamii basi kidogokidogo na Watengenezaji wataimarika na kuongeza ubunifu wao, sambamba na kupunguza gharama zao za uzalishaji wa bidhaa hizo.

Haya yaende sambamba na kutengeneza kizazi kinachothamini bidhaa za ndani.
 
Kamwe usitarajie Mtu anayetegemea ugali wake kwenye jambo fulani kama ataruhusu ufahamu jinsi anavyofanya jambo hilo.....maana anajua kesho utamwambia aondoke ufanye mwenyewe.
 
Sasa kama bidhaa za humu ndani ya nchi ni ghali kuliko za kuagiza wewe utachagua kipi?
Mfano cement . Unaonaje ikaja ya South Africa 10000 mfuko utanunua ya Simba 18000?

Mfano Sukari ...Unaonaje Uganda wakaleta ya 1500 utanunua TPC 2800?

Tusidanganyane tunahitaji kujipanga kama nchi kabla hujazuia bidhaa za nje tofauti na hapo lazima pawepo mfumko wa bei
 
Lini mtatengeneza Sheria ya kulinda viwanda vya ndani kama spika wa Bunge mwenyewe ndio yule mjinga kabisa
 
Hapo juu nimeongelea pia hili suala la gharama za uzalishaji....Bidhaa ikikubalika kwa wingi kwa vyovyote itachangia kupunguza gharama za uzalishaji...hao Wachina gharama zipo chini kwa sababu wanauza kwa wingi.

Hapa ni ile hadithi ya Yai na Kuku kipi kitangulie, tuwe na bidhaa bora kwanza au tutengeneze kinachowezekana hivyo hivyo tuende tukiboresha siku baada ya siku kutokana na soko?. ...au tukae tu fwaaa. Ndio maana pia nikasema na utashi wa kisiasa unahitajika kwenye hili...pamoja mapungufu kadhaa lakini Mwendazake alikuwa na mtazamo mzuri sana kwenye hili la bidhaa za ndani.

Tuchukue mfano wa hii ligi yetu hapa Bongo...hivi unadhani Wabongo tungeisusa kabisa Ligi yetu na kubaki kushabikia tu EPL leo ungeona AZAM wakiweka mabilioni yao?, sanasana nao wangehangaika tu kupata namna ya kuonesha EPL wapige pesa wanazopiga dstv...lakini kwa kuwa tulikubaliana na Ligi yetu hivyohivyo na mapungufu yake tangu awali ndio maana leo tumefikia hapa.

Kwa maneno mengine Wachina wangeona fursa kweye soka basi wangepambana kuhakikisha tunafuatilia ligi yao....alafu kwenye hotuba wangetusifia sana kuwa wanatupenda....hivi nani asiyependa zezeta linalotumia asilimia 90 ya mapato yeke kununua bidhaa na huduma zake?....Wachina wanapata ajira, wanaboresha maisha yao kupitia migongo yenu.

Tukiweka nia kama taifa tutafika maana hili si lelemama.
 
Kumbe furniture za mninga tunatengeneza, sasa unachowabeza Watanzania ni nini?

Acha mambo ya kupenda kujitukana Utanzania wako, uwezo tunao, tembea kifua mbele
 
Kumbe furniture za mninga tunatengeneza, sasa unachowabeza Watanzania ni nini?

Acha mambo ya kupenda kujitukana Utanzania wako, uwezo tunao, tembea kifua mbele
Ni sawa lakini huu uwezo unahitaji kukuzwa kwa soko.

Tukinunua kwa wingi bidhaa za Wabunifu wetu tutawakuza....wanasema tuwaungishe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…