Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Majina mazito mazito haya ni kielelezo kamili cha wapigania haki wenye kutukuka. Nini kisimame mbele ya watu kama hao kuzuia haki kutamalaki?

IMG_20220821_165743_714.jpg

Nini thamani ya maisha ya awaye yote kama ukosefu wa haki ndiyo unaozidi kuota mizizi?

Nini kimetupata watanzania sisi leo kutokuwa na kizazi cha waungwana firebrand kama hawa katika jamii yetu?

IMG_20220821_165805_200.jpg

Harakati huongozwa, haziwezi kuja (spontaneously) kama mvua.

Kadamnasi lisililokuwa na viongozi thabiti ni sawa na kundi la kondoo bila Mchungaji.

Mengine tuyaonayo ni yatokanayo tu.
 
chadema sio size yako wewe shoga la fifth presidential failure odinga and the follower of walamba asali wa lumumba.

Walamba asali na vibaraka wao huchachawa mno waonapoona mpira ukichezwa ndani ya 18 zao.

Hatuko mbali, tunajongea. Habari ndiyo hiyo.
 
Majina mazito mazito haya ni kielelezo kamili cha wapigania haki wenye kutukuka. Nini kisimame mbele ya watu kama hao kuzuia haki kutamalaki?

Nini thamani ya maisha ya awaye yote kama ukosefu wa haki ndiyo unaozidi kuota mizizi?

Nini kimetupata watanzania sisi leo kutokuwa na kizazi cha waungwana firebrand kama hawa katika jamii yetu?

Harakati huongozwa, haziwezi kuja (spontaneous) kama mvua.

Kadamnasi lisililokuwa na viongozi thabiti ni sawa na kundi la kondoo bila Mchungaji.

Mengine tuyaonayo ni yatokanayo tu.
Agenda ya Dunia imebadilika. Hao uliowataja walikuwa Pan-Africanists ambao malengo yao yalikuwa kuikomboa Afrika baada ya post WWWII. Na walifanikiwa hilo kuanzia 1957 wakati Ghana ikipata uhuru hadi 1994 wakati South Africa ya Mandela ikiondoa Serikali ya kibaguzi na kuleta utawala wa kidemokrasia.

Mpambano wa sasa hivi ni against NWO ambao unachezwa kimkakati zaidi kuhakikisha kuwa Afrika inakuwa mshirika mkubwa wa uchumi wa Dunia na siyo mpeleka Mali ghafi. Hapahitaji kupayuka bali pnahitaji best brains katika investments, legal issues, negotiations skills etc
 
Umeyasoma vyema majina niliyoyataja yote mkuu? Tafadhali yarejee.

Kumbuka Julius Malema ni kijana angali kupoa.
 
Julius Malema hatokuja kupewa nafasi ya kutawala SA. Hata wazawa wanaogopa kuwa atafuata nyayo za Robert Mugabe. No matter kuwa Walowezi wa Zimbabwe walipaswa kuwa achia ardhi yenye rutuba wenyeji ambao ni weupe kisha Serikali ya UK kuwalipa fidia Walowezi, lakini namna ambayo Mugabe aliitumia kuyachukua mashamba na kuyagawa kwa rafiki zake wapigania uhuru, ndiyo iliyoharibu uchumi wa Zimbabwe.
 
Kupewa kutawala na kupigania haki ni mambo mawili tofauti.

Ninakazia: wako wapi kina Shivji, Ulimwengu, Odinga, Kakoko, Mkenda, Bazigiza, Matiko Matare na wenzao wa zama zile, leo?

Wako wapi kina Sarungi? Wako wapi kina Kimaro?

Eeh Mola wetu, ukisikie kilio chetu.
 
Unapokuwa na mwanasiasa anayejiita wa upinzani anadai awamu hii hatakuwa akipinga chochote, hapo ni sawa na hatuna mpinzani, watanzania ni lazima tuamke, kuendelea kuwasubiri wakina Lissu na Mbowe kila siku wakati wameshaongea sana siku za nyuma, ni kuwaonea.
 
Bila kina Tutu, Mtikila, Malema, Maalim Seif na firebrand wa namna hiyo watanzania walio amka ni kama kundi la nyumbu tu.
 
Kupewa kutawala na kupigania haki ni mambo mawili tofauti.

Ninakazia: wako wapi kina Shivji, Ulimwengu, Odinga, Kakoko, Mkenda, Bazigiza, Matiko Matare na wenzao wa zama za leo?

Wako wapi kina Sarungi? Wako wapi kina Kimaro?

Eeh Mola wetu, ukisikie kilio chetu.
Bazigiza alikufa, Matiko Matare naye alikufa na Harun Kimaro alikimbikia Zimbabwe na kufanya kazi za uganga wa kienyeji.

Ukitaka FRUSTRATION just kuwa Anti Government
 
Majina mazito mazito haya ni kielelezo kamili cha wapigania haki wenye kutukuka. Nini kisimame mbele ya watu kama hao kuzuia haki kutamalaki?

View attachment 2330437

Nini thamani ya maisha ya awaye yote kama ukosefu wa haki ndiyo unaozidi kuota mizizi?

Nini kimetupata watanzania sisi leo kutokuwa na kizazi cha waungwana firebrand kama hawa katika jamii yetu?

View attachment 2330438

Harakati huongozwa, haziwezi kuja (spontaneous) kama mvua.

Kadamnasi lisililokuwa na viongozi thabiti ni sawa na kundi la kondoo bila Mchungaji.

Mengine tuyaonayo ni yatokanayo tu.
Kataa kuwa chini ya sheria bali taka kuwa chini ya haki tu
Mtua apendaye kuwa chini ya sheria usema kuvunja sheria ni kosa bali aliye chini ya haki uvunja sheria kwa ajili ya haki na huyo ndiyo mzalendo wa kweli mtu ambaye yupo tayari kuvunja sheria kwa ajili ya HAKI.
Kwa kuwa kuvunja sheria kwa ajili ya haki ndiyo haki yenyewe hiyo.
 
Bazigiza alikufa, Matiko Matare naye alikufa na Harun Kimaro alikimbikia Zimbabwe na kufanya kazi za uganga wa kienyeji.

Ukitaka FRUSTRATION just kuwa Anti Government
Kuvunjika kwa koleo hakujawahi kuwa mwisho wa uhunzi.

Kufa siyo mwisho wa kuwapo duniani. Walikufa kina Tutu, Mtikila, Mandela na wengine. Lakini tungali tukiuliza walipo.

Hata kina Kimaro na Sarungi kimwili walishakufa. Harakati zao zilikufa pia?

Yuko wapi Prof. Chachage?

"Wanamapinduzi hawafi. Hata wakifa mizimu yao huendeleza mapambano." -- Fidel Castro.

Habari ndiyo hiyo.
 
Bazigiza alikufa, Matiko Matare naye alikufa na Harun Kimaro alikimbikia Zimbabwe na kufanya kazi za uganga wa kienyeji.

Ukitaka FRUSTRATION just kuwa Anti Government
Ndio frustration ila je watu waogope na waendelee kuumizwa na haki zao za msingi kugandamizwa bila kuongea ama kuyasema hayo kisa frustrations.

#MaendeleoHayanaChama
 
Walamba asali na chawa wao wangependa mno tuogope.

Habari mbaya kwao ni kuwa - hatutapoa.
 
Simba vs Yanga
Betting online
Mzuka shinda mahela
Pombe
Casino
Bongoflava
Vijana wa ovyo tu ndio tuliobakia hao wa kupigania haki kwishaa kabisa.

Wasiwasi wangu ni kuwa haya ni yatokanayo kwa kukosa uongozi usiopoa kama wa akina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema, Tutu na wa namna hiyo.

Wako wapi kina Prof. Chachage na kina Prof. Sharif?

Ndipo ulipo msingi wa hoja: Tusilaumiane - mengine ni yatokanayo.

Kundi la vijana hao bila uongozi thabiti halina tofauti na genge la nyumbu tu.
 
Back
Top Bottom