The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,709
Hakuna ubishi. Samia Suluhu Hassan ni mmojawapo wa watawala wanaochukiwa ndani ya nje. Japo anao machawa wake wanaomtetea na kuwaona wanaomchukia kama wasaliti na wenye makosa kwa sababu wazijuazo ambazo nyingi ni za kibinafsi, ukweli usemwe tu.
Samia anachukiwa. Naye analijua hilo. Ukisikia matamshi yake yasiyo ya busara, unaliona hili dhahiri. Badala ya kutafuta sababu ya kuchukiwa kwake, Samia anajitahidi kuchukia kuchukiwa bila kwenda kwenye kiini cha kuchukiwa kwake.
Kabla ya tarehe 29 Oktoba, 2025 allipoamuru polisi na jeshi kuua waandamanaji, Samia alikuwa hachukiwi wala kujulikana kama sasa. Je, jibu ni kujibu mapigo tena kijinga au kuliendea tatizo na kulitafutia ufumbuzi? Je, anao uwezo wa kufanya hivyo hasa tukijikumbusha utawala wake ulivyogeuka aibu kwa taifa? Je, Watanzania wahanga tufanye nini?