Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu wana JF wenzangu,
Ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze kwenye mada husika hapo juu.
Wana JF wenzangu, siku mbili tatu zilizopita tumeshuhudia lawama, kejeli na vijembe kutoka kwa watu mbali mbali wakimlaumu makamu mwenyekiti wa Chadema mh Lisu kwa kukimbia mapambano mapema na kukiacha chama kikiwa hakina muelekeo wa maana kisiasa. Watu wengi wameonekana kumlaumu makamu huyo bila kujua hasa chanzo halisi na cha kweli kilichomkimbiza m'beleji huyo alieingia nchini wiki tatu tu zilizopita baada ya kukaa Ubelgiji kwa zaidi ya miaka miwili kwa kile kinachofahamika na watu wengi wenye akili kwamba alikimbia aibu ya kushindwa vibaya katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Ndugu Lisu alipotangaza kuja au alipoingia nchini chawa wengi walionekana kuwa na matumaini nae na kufikiri kwamba makamu huyo anakuja kukijenga tena chama ambacho kinaonekana kimeyumba haswa baada ya kuwa na shutuma kwamba mwenyekiti wa chama hicho taifa amelamba asali na kukiuwa chama kiaina, hali inayopelekea wananchi wengi wakose imani nacho.
Sasa inashangaza makamu huyo baada ya kuingia amefanya mikutano yake miwili mitatu bila kupata support ya aina yoyote kutoka kwa wale aliowatarajia. Lakini ukiachana na hayo ya kususwa katika mikutano hapo chini naorodhesha mambo makubwa yaliomfanya makamu huyo aingie mitini na kukitelekeza chama hicho.
1) Kitendo cha mwenyekiti wa chama kuvuta mpunga na kukikodisha chama hicho kwa Lowasa bado kipo katika akili ya makamu huyu japo kwa sasa hawezi ongea kwa sababu na yeye alimegewa fungu na kujikuta anameza matapishi yake mwenyewe.
2)Kitendo cha mwenyekiti kulamba asali na kuvuta ruzuku za wale covid 19 kimya kimya kupitia account ya uchochoroni pia kimemfanya makamu achukie kwani msimamo wa chama na wa mwenyekiti wa chama ni vitu viwili tofauti.
3) Katibu mkuu wa sasa hana muelekeo, ushawishi na uthubutu kama ule aliokuwa nao yule wanaemwita Dr Mihogo.
4) Chama kukosa muelekeo maana toka ruhusa ya mikutano ianze ni viongozi wachache tu wa chama hicho ndo wamejishirikisha na mikutano ila wengine wanaonekana kuwa busy na mambo yao ya kuwaingizia kipato chao kwa ajili yao na familia zao.
Hakuna mtu mwenye akili angekubali kuja kusimama juani kutwa nzima kusikiliza sera za kupigwa bunduki nk huku watoto nyumbani wakiwa hawajui watakula nini. Wakati huo huyo aliekusimamisha juani watoto wake wako Marekani wanakula bata na tayari wana uraia wa nchi hiyo.
Sababu zilizomkimbiza Lisu ni nyingi ila hizo ni baadhi tu. Siku akitoka chamani au kuachana na siasa atakuwa na mengi ya kuongea. Maana jamaa huwa ni mtu wa visasi kwahiyo naamini na haya yaliomchukiza na kumkimbiza kuna siku atayaongea tu. Let's wait time will tell.
J2 njema.