Tusimlaumu Makamu, bali tuulaumu uongozi wa juu hata kama haturuhusiwi kuongea ukweli

Dah pole mkuu, kumbe kipindi kile tuliumia wengi aisee.
Kwa sasa chama kipo kwenye mikono ya madalali wa siasa, hatuna jinsi tena ya kukirudisha katika dira yake.
 
Ninachokubaliana na mada hii ni jambo moja tu; kwamba ile CHADEMA iliyokuwepo nyakati za Magufuli, na hata enzi zile za akina Mihogo haipo tena.

Hapo hapo pia, ni wazi kwamba CCM iliyokuwepo chini ya Magufuli, na hata enzi za akina Mkapa, haipo tena wakati huu wa Samia.

Huu ndio ukweli usiopingika.

Lissu amekuja na kujionea mwenyewe uhalisia huo, na kujikuta kama anapwaya, hana sehemu anayofiti kisawasawa ndani ya CHADEMA mpya, ambayo ipo kwenye mjadala jinsi ya kuungana na CCM ya Samia, ili na wao wale bata.

Baada ya kuyasema hayo, sina hakika kama mleta mada yanampa ahueni sana katika anayoyasimamia yeye, kama kweli anayo.
 
Dah pole mkuu, kumbe kipindi kile tuliumia wengi aisee.
Kwa sasa chama kipo kwenye mikono ya madalali wa siasa, hatuna jinsi tena ya kukirudisha katika dira yake.
Niliumia sana kiasi kwamba tangu wakati huo nikaamua kuacha kujihusisha na chama chochote cha siasa.
Sifurahii chadema kufa, lakini ngoja hao madalali wavune walichopanda.
 
Niliumia sana kiasi kwamba tangu wakati huo nikaamua kuacha kujihusisha na chama chochote cha siasa.
Sifurahii chadema kufa, lakini ngoja hao madalali wavune walichopanda.
Kwa hakika siasa za Tanzania ni michosho sana. Mda mungine zinachosha akili na mwili. Bora ulivyoamua kukaa pembeni mkuu.
 
Ahueni ipo haswa kwa mambo mengi mazuri yaliofanywa na serikali ya hayati Magufuli na pia yanayofanywa sasa hivi na raisi Samia.
 
Chama cha democrasia mwenyekiti toka nazaliwa hadi leo na watoto wakubwa sijawahi sikia mwenyeketi tofauti na mbowe.hiyo democrasia gani sasa.wazungu wanasema charity begins at home.hiki ni chama cha ukoo wa kina mbowe ndio maana mbowe hatoki hapo ukijaribu utakiona chamoto
 
Bora na wewe umemueleza ukweli ndugu yangu. Hawa watu sijui wamelogwa kwa kutumia mzizi gani aisee. Wamekuwa wazito kuuona ukweli machoni mwao.
 
Msitafute sababu zisizo na mashiko kwa CHADEMA kukosa mvuto.
Mama Samia kazisambaratisha mbinu zote za wapinzani.
 
Msitafute sababu zisizo na mashiko kwa CHADEMA kukosa mvuto.
Mama Samia kazisambaratisha mbinu zote za wapinzani.
Dah yani ruhusa ya mikutano imevivua vyama vyetu nguo. Ni afadhali katazo lile lingeendelea tu hadi uchaguzi mkuu.
 
Nani anayefagilia Mbowe kukaa madarakani zaidi ya miaka 10 boss?
 
Niliumia sana kiasi kwamba tangu wakati huo nikaamua kuacha kujihusisha na chama chochote cha siasa.
Watu waliumia sana. Rafiki yangu Aweda Mikael tangu kipindi hicho hataki kusikia habari ya siasa.

Lakini kwa upande mwingine huwa namshukuru Mungu kwa yaliyotokea 2015. Tuliweza kutambua kuwa watu tuliowaamini kumbe nao ni laghai na pengine matapeli kuliko hao wa kijani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…