Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,434
- 27,177
HakikaLakini hili la kukutana na Chadema katika maadhimisho ya BAWACHA hatutalisahau kirahisi.
Hatua ndio imeanza, Katiba inaundwa kikosi kazi na itakuja tu, usiwe na mawazo ya wahafidhina , kuwa na imani na Mama .Sumu ya haya maridhiano ni KATIBA MPYA maana hapo Chadema ndipo wataanza kununa. Dr Bagonza (Askofu wa KKKT), unasahau kuwa Katiba Mpya haiwezi kuandaliwa na wanaotamani madaraka bali wasiotaka madaraka. Hiyo haitakuwa katiba bali uozo. Yangu macho nasubiri siku hiyo itimie kama ya JK (ati nyie Wabunge hamtaki kuwa mawaziri!!!).
CHADEMA wamechukua hatua kwakuwa ACT ya ZITTO hawataki katiba wanataka tume huru.1. Tunatakiwa kufahamu kuwa nchi hii ni ya wote na sio ya CCM au CDM au chama kingine chochote.
2. maridhiano ni muhimu kwa ustawi wa Taifa ili tuondokane na ule utawala wa shetani!
3. Tutambue kuwa hata vitabu vitakatifu vinanena kuwa; haki uinua Taifa na dhuluma huangamiza taifa. (mfano mzuri angalieni utawala wa awamu ya 5 ulivyokuwa umeangamiza shetani)
Wewe nawe sawa na hao. Nitatoa mfano mmoja tu. Chadema inataka katiba ambayo matokeo ya urais yatapingwa mahakamani. Je Samia atakubali hilo? Chadema inataka katiba ambamo madaraka ya Rais yatapunguzwa, Je, Samia atakubali hilo?Hatua ndio imeanza, Katiba inaundwa kikosi kazi na itakuja tu, usiwe na mawazo ya wahafidhina , kuwa na imani na Mama .
Umesikia SAMIA hataki matokeo kupingwa? Uchaguzi ukiwa chini ya tume huru na ukiwa fair kwanini uogope Kesi?Wewe nawe sawa na hao. Nitatoa mfano mmoja tu. Chadema inataka katiba ambayo matokeo ya urais yatapingwa mahakamani. Je Samia atakubali hilo? Chadema inataka katiba ambamo madaraka ya Rais yatapunguzwa, Je, Samia atakubali hilo?
NINI KIFANYIKE?Wananchi watakula huo mkutano na maridhiano? Uchumi unaporomoka, watu hali ni mbaya, maji umeme mgao bidhaa bei juu bado mnashabikia huu upuuzi?
Akili yako mbovu, nani hajui kama kuna Tume Huru CCM haiwezi kufua dafu! Hii ni kawaida kwetu wanadamu, kitu ukiwa nacho unasema cha nini ingawa wasionacho wanasema tutakipata lini. Ndiyo maana nchi kama Zambia au Malawi kubadili uongozi ni rahisiUmesikia SAMIA hataki matokeo kupingwa? Uchaguzi ukiwa chini ya tume huru na ukiwa fair kwanini uogope Kesi?
Unafikir kila mtu atafungua kesi kisa tu hajashinda? Kesi za uchaguzi kuna pre -filling, kabla ya kuwa admitted lazma uonyeshe kuna ukiukwaji, tatizo lishe mbovu ya wabongo na elimu duni ya CCM kwa miaka 60 ndio maana hata wewe unayetaip hapa mambo mdogo kama haya hujui.
well saidAkili yako mbovu, nani hajui kama kuna Tume Huru CCM haiwezi kufua dafu! Hii ni kawaida kwetu wanadamu, kitu ukiwa nacho unasema cha nini ingawa wasionacho wanasema tutakipata lini. Ndiyo maana nchi kama Zambia au Malawi kubadili uongozi ni rahisi
Mambo si rahisi kama tunavyofikiria! Njia ya kufanya ni kuwa na sheria ambayo wote watakaohusika na uandaaji pamoja na kupitisha hiyo katiba mpya, wasigombee uongozi katika nchi hii kwa miaka 20 ijayo. Hapo tutapata katiba nyie Chadema muipendayo la sivyo msahau.well said
Wassira , Makongoro yaani ni viongozi zaidi ya miaka 50 na hawataki kuachia, ukisema katiba ije na vigezo vikali hawawezi kubali.Mambo si rahisi kama tunavyofikiria! Njia ya kufanya ni kuwa na sheria ambayo wote watakaohusika na uandaaji pamoja na kupitisha hiyo katiba mpya, wasigombee uongozi katika nchi hii kwa miaka 20 ijayo. Hapo tutapata katiba nyie Chadema muipendayo la sivyo msahau.
Na hapo ndiyo mwisho wa ndoto za katiba mpyaWassira , Makongoro yaani ni viongozi zaidi ya miaka 50 na hawataki kuachia, ukisema katiba ije na vigezo vikali hawawezi kubali.
Hiyo ndo priority ya wanachi huku mchele kilo moja ukiwa umefika 4000Tafakuri ya Askofu Benson Kalikawe Bagonza
Rais Samia ameweka rekodi. Tutasahau barabara, madaraja, madarasa na teuzi anazofanya. Lakini hili la kukutana na Chadema katika maadhimisho ya BAWACHA hatutalisahau kirahisi.
Wapo walionuna pande zote mbili za CCM na Upinzani. Ni budi wawepo ili watukumbushe tulikotoka. Hata kuku wa pande mbili hizo hawakuruhusiwa kujamiiana. Leo twakumbatiana!
Mwaka jana 2022 nilihutubia Bawacha Kitaifa kule Iringa. Nilisema tunahitaji Tanzania mpya siyo CCM mpya wala Chadema mpya.
Niliporudi DSM nilikutana na kiongozi wa CCM kitaifa nikamwambia; “Awamu ya Tano imeimarisha upinzani kwa namna ambayo ni vigumu kuubomoa bali kuuruhusu ujibomoe.”
Sasa Rais Samia ameanzisha mchakato wa upinzani kujibomoa wenyewe, si kuruhusu Rais mwingine kama yule aje kuubomoa. Tumuunge mkono Rais Samia anapotumia hoja kuunganisha nchi kuliko kutumia fedha na mabomu kugawa nchi.
Napenda kushauri mambo 10:
1. Kila upande una wahafidhina (Zealots).
Kazi ya kiongozi si kuwapuuza wala kuwafukuza. Ni kujadiliana nao bila kupigana nao. Wakiondoka vyama vitalala.
2. Kufukuzana ni hulka ya viongozi madikteta na walevi wa madaraka.
Rais Samia na Mbowe wajiepushe na hulka hiyo.
3. Kuna mpito unakuja kitaifa.
Mbuzi atalala na chui zizi moja bila kuumizana. Bungeni, serikalini, na hata kwenye kamati. Tujifunze kuishi na hali tusiyoweza kuibadilisha.
4. Ukweli wa yaliyopita ni muhimu kuliko haki kwa yajayo.
Tujifunze kusamehe kosa lililo wazi. Hata marehemu akiacha madeni huwa yanalipwa na warithi.
5. Tusisahau tulipopitishwa.
Si CCM wote waliokubaliana na hali ile. Si wapinzani wote walioichukia hali ile. Ili tusirudi huko tuungane kusema NEVER and NEVER again.
6. Ili tusirudi huko, mifumo imara na taasisi imara ni muhimu kuliko super woman au super mwamba.
Hata kama hatuipendi; KATIBA MPYA ni hitaji la jana kuliko leo na wanaihitaji watawala kuliko watawaliwa.
7. Kiwango cha rushwa bado kiko juu na kinastawisha kiburi cha watawala dhidi ya wananchi.
Wenye fedha wanaanza kujiona juu ya sheria. Rushwa hii ikiingia ndani ya vyama, tutampata mwenye roho isiyo ya Samia na mbaya kuliko Bwana yuleee.
8. Jukumu la Rais ni kuongeza uhuru wa wananchi; si kuupunguza.
Watanzania tuunge mkono jitihada za Rais kuthamini na kuvumilia maoni tofauti. Rais hawezi kufa wala kuugua kwa kuambiwa asiyopenda kusikia.
9. Siku ya wanawake imefana, bado safari ya ukombozi wao ni ndefu.
Maadui wao ni wengi. Hata mwanamme anayekandamizwa na mkewe lakini anajifanya mbabe mbele ya wanaume wenzake asaidiwe na wanawake!
10. Wapinzani wa maridhiano ni wale walioshindwa ndani na nje ya vyama vyao.
Maridhiano yanawanyima uhalali. Lakini wapo wanaotaka maridhiano yaondoe tofauti za mtazamo na maoni tofauti. Hatutaki makasuku wa taifa. Tuheshimu tofauti bila kupigana.
Tumuunge mkono Rais Samia. Tumpinge kwa hoja. Tusisahau kirahisi tulikotoka.
na bado , subirini mwezi wa 6.Hiyo ndo priority ya wanachi huku mchele kilo moja ukiwa umefika 4000