Uchaguzi 2020 Tusimuache Lissu atuahidi yasiyowezekana

Hiyo millioni 50 imezaa zahanati na umeme wa REA kila kijiji..kumbuka kujiungia umeme ilikuwa 170,000 na sasa ni elf 27 tu..upewe nini?
Zahanati na umeme vinatoa mikopo kama ahadi ilivyesema juu ya milioni 50?au na wewe ndo walewale pelekwapelekwa
 
Ungeacha jazba ujenge hoja,urais si uongozi ndani ya Chadema kwamba kila lopolopo apewe.Tafakari
KAMA ULIMWAMINI CHIZI,LAGHAI NA MWIZI ( hata rambi rambi,tr.1.5) UTASHINDWAJE KUMWAMINI MSEMA KWELI?
 
Ccm hawajajenga ofisi katika Tanzania hii labda kama ni ktk nchi nyingine.

Ndivyo Kanu kule Kenya walijidanganya kuwa zile ofisi zilikuwa ni zao lkn siku walipotolewa madarakani hawakuamini macho yao.

Hivyo nyie jidanganyeni tu hivyo kuwa mna ofisi. No situation lasts for ever.
 
Mungu amekupa akili na maarifa kama una elimu sio lazima uajiriwe kuna shughuli nyingi za kufanya mpaka vijijini kwa nini usiw mbunifu kazi ni nyingi tena zinavipato zaidi ya ajira .
 
Hoja inahusu utekelezaji wa ahadi za lisu ususa swala la bima usilete habari za magufuli au membe au hashimu rugwe au lipumba elewa hoja acha ubishi
Mkuu hivi bima ya afya kwa watanzania ambao si kwamba wanaishi hospital na elimu bure kwa mtazamo wako kipi chenye gharama nafuu?
 
Mungu amekupa akili na maarifa kama una elimu sio lazima uajiriwe kuna shughuli nyingi za kufanya mpaka vijijini kwa nini usiw mbunifu kazi ni nyingi tena zinavipato zaidi ya ajira .
Mkuu elimu ndo inatakiwa iwe maarifa si maarifa ya kupewa na Magu.Magu yupo kwenye ajira maisha yake yote amejitutumua tu kuanzisha Ranchi baada ya kuwa rais na still anatumia resources za serikali kuendesha biashara zake binafsi ,angekuwa na maarifa angetegemea kuajiriwa ili aendeshe maisha yake,?
 
Kuna mgombea alisema anataka kuigeuza Tz iwe kama Ulaya,vip hapo.maana nadhani hiyo ndio ndoto kubwa isiyotekelezeka kuliko zote alizoota.
 
Lissu alikuaga mbunge lakini jimboni kwake sio ata pa kuongea kwa sauti ni mjini lakini hio aibu basi tu
Kwani Lissu anakusanya kodi?. Si hata kodi zilizokuwa zinakusanywa na halmashauri zimechukuliwa na serikali kuu, unatarajia afanye nini? Huyu mbunge aliyepo sasa hivi ameshafanya maajabu gani hadi sasa? Umeshatembelea majimbo mengine yaliyo chini ya ccm hapo mkoani Singida na kuona maendeleo yake?
 
Nafikiri amepotosha Makusudi kwa sababu ni mwanaFisiemu...

Katika suala la afya na bima, Lissu anazungumzia upatikanaji wa huduma za afya pamoja na unafuu wa gharama za matibabu....i.e. Accessibility and Affordability

Lissu hajasema kutakuwa na bima ya bure, isipokuwa anasema huduma z afya nchini zinaweza kuboreshwa kwa kila Mwananchi kuwa na bima ya afya iliyo nafuu....kwamba uchangiaji Utakuwa nafuu, atakayeweza kulipia huo unafuu ndo atafaidika...hoja kubwa hapa ni dhamira, bima ya afya isiwe exclusive kwa kundi flan tu...Kama Magustinho naye anataka aoneshe dhamira, yeye atafanya nini? Serikali yake itaendelea tu kukwanyua hela za NHIF na mifuko ya hifadhi ya Jamii kujenga madaraja?

La pili Lissu anakemea mfumo wa kibaguzi katika utaratibu wa sasa wa huduma za matibabu kwa bima ya NHIF...Lissu analalamika kuwa Serikali imekopa mabilioni ya fedha kutoka NHIF kiasi kwamba taasisi hiyo inaamua kuwadhulumu Wanachama wake kwa kuwanyima kupata huduma za matibabu kwa Kisingizio cha kiwango cha mchango wa mwanachama; kama mchango wako ni chini ya 600,000/- kwa mwaka hutibiwi, utaishia kuandikiwa panadol tu

Kingine Serikali haiwasilishi kwa NHIF makato ya Mishahara ya Wafanyakazi wake kwa ajili ya bima ya afya...wanakata hela halaf zinaliwa juu-kwa-juu

Kwa hiyo Lissu anakemea mambo Haya ni Lazima aungwe mkono!
 
Denmark wanatia bima kwa kila raia na hata wageni. Ukishapata working au permanent residence na raia wao wote unpewa kitambulisho Cha ukazi/uraia na yenyewe ni bima. Unaenda hospital yeyote kumuona Dr. Ni hurry, vipimo vyote ni bure, upasuaji wa Aina yeyote Ile bure. Unalipia dawa tu. Na dawa hiyo Ina subsidy (ruzuku) ukinunua dawa za DKK1000 utalipa 100% kuanzia 1001-2000 unalipia 75% , zaidi ya 2001-3000 unakupa 50% ukinunua dawa 3001-4000 unalipia 25% above 4001 ni free.

Pamoja na yote hizo bima zao hazifanyi coverage kwa meno na miwani.

Pia watoto wote below 12 Yrs bure kila kitu na wazee wote above 65yrs bure kila kitu.

Fanya research yako Tena Bob mushi
 
KWANI VYAMA VINGINE VILIWAHI KUJIJENGA OFISI?
 
Tuanze na yule aliyetuahidi Mill. 50 kila kijiji.
 
Contradiction; Unaandika kuwa Lisu anasema kila mtanzania kumiliki bima ya Afya; wewe mwenyewe unajiongezea eti BIMA BURE
 
Lissu anatoa ahadi zinazotekelezeka sio zile za milion 50 kila kijiji au laptop kila mwalimu.

Mlet mada ni mpumbavu. Hiyo Marekani aliyotaja hajui kuwa kati ya makampuni tajiri ni yale yanayotoa bima za afya! Hajui fedha za bima huwekezwa kwenye mabenki na kuzaa. Hakui kuwa waougua na kuhitaji matibabu ni sehemu ndogo sana ya watoa michango na ni pesa ndogo sana kutoka pesa ya jumla. Mleta mada hajui kuwa watoa michango nyuma ya pazia ni watu wanaofanya kila bidii ili wasiugue - hivo kufanya michango yao kuhudumia wachache tu!!

Ahadi anazotoa Lissu zinatekelezeka! Kama atashinda au kushindwa, hili ni jambo lingine.
 


Kazi ya mbunge ni kuwasemea wananchi bungeni matatizo waliyo nayo: toka lissu ameingia kua mbunge sjawahi ona akishuhulikia miradi yoyote na wananchi wake, yeye kazi yake ni kuropoka always
 
Hakuna mahali Lissu amesema atatoa Bima ya Afya bure. Amesema atatoa Bima ya Afya kwa kila Mtanzania lakini hajasema atatoa bure

Sent from my vivo 1904 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…