Tusimung'unye maneno, barabara ya Kusini ilijengwa chini ya viwango!

Inasikitisha sana namna tunavyoshindwa kusimamia miradi muhimu ya miundombinu kwa manufaa yetu wenyewe
 
Kwenye hii Barabara kipande Cha kuanzia ikwiriri Hadi somanga ndo kipande korofi mno , sasa kuna mambo mengi
1. Hiki kipande kina mito mingi mno maana ndo sehemu matawi ya mto rufiji yanaenda baharini hivyo maji yakua yameathiri sana
2 baada ya kujengwa hiki kipande lami yake ilikua na muonekano mweupe hivi , nadhani kokoto zilizotumika sio za lugoba, huenda zimetumika zile ya ubuyo ambayo ambazo water absorption zake hua ni kubwa kwa sababu ni porous kwa hiyo asphalt mix design huenda haikua efficient
3 Hii Barabara imekamilika miaka zaidi ya 15 iliyopita, huenda lifespan yake imeshaisha ukizingatia Barabara zetu nyingi design lifespan ni miaka 10 tu
4 Usanifu wa hii Barabara haukuconsider sudden load ya dangote factory, malori ya cement nayo yamechangia uchakavu wa hii Barabara to some extent, coz imagine dangone ana fleet kama 600 hivi , jumlisha na watu watu wengine hii Barabara lazima iharibike tu hasa kama Usanifu haukuzingatia huo mzigo ambao kimsingi haukuwepo kabisaaa

Ifanyike impact analysis kwa hiki kipande Cha km 60, kijengwe upya kwa kuzingatia new design assumptions
Let's be constructive na tuiache kunyooshana vidole hasa kwa hizi mvua A mwaka huu ambazo zipo juu ya kiwango Cha kawaida.
 
Mkuu mada ikiwa juu ya uwezo wako kudadavua, we sepa tu uelekeo wa chit-chat!
 
Mkuu mada ikiwa juu ya uwezo wako kudadavua, we sepa tu uelekeo wa chit-chat!
Hakuna lolote la mada kuwa juu. Sijaanza kukusoma leo, na wala hakuna jipya katika uliyo andika katika mada hiyo unaloweza kudai lipo juu ya uwezo wa wengine kulitambua.
Nimekupa ushauri, bila shaka umekuingia akilini vya kutosha.
 
Hakuna lolote la mada kuwa juu. Sijaanza kukusoma leo, na wala hakuna jipya katika uliyo andika katika mada hiyo unaloweza kudai lipo juu ya uwezo wa wengine kulitambua.
Nimekupa ushauri, bila shaka umekuingia akilini vya kutosha.
Mkuu usilazimishe kulumbana na akili kubwa.
Kubali tu ukomo wako wa kufikiri.
 
Sasa Mbona wanasema baada ya Masaa 72 pawe pametengenezwa? Tunaziba maji ya Mto kwa Mawe? Halafu mto unarudi ulipotoka?
 
Respect mkuu kwa kujadili mambo ya kimsingi kabisa kihandisi.
Hii barabara yoote DSM TO MTWARA, hasa Ikwiriri -Somanga, iko katika failure mode.

Serikali kupitia wizara husika itake note hydrological facts kutokana na mvua za mwaka huu.
 
Hata ya Bagamoyo ilijengwa chini ya kiwango na Waziri Husika alikuja kuichukulia hatua na Riasi na Kawambwa wanawabagamoyo walikuwepo
 
Ile ya makambako benki ya dunia wamekopesha wanajua shaba ya Zambia na mizigo ya Malawi itawalipa
 
Bila shaka ilijengwa na wale jamaa wa Kharafi.
Lakini ni Bora watu wakusini wamesahau yale mateso ya nangurukuru, somanga nk.

Kipindi cha masika na mvua Mtwara kulikuwa hakuendeki, option ya Meli ilikuwa 2days.

Hizi barabara shida ni umasikini wetu lakini kuwapa wachina plus kupenda urahisi na rushwa tunabaki na majanga
 
Halafu hapo mnazi mmoja hadi Masasi ni pa zamani mno na ubovu wake
Sasa kama hadi Muhoro -Somanga pameharibika ,si upuuzi maana pamejengwa juzi tu
Lami ya masasi ya zaman sana ila Muhoro hapajakaa sana viraka kama vyote
 
Hata ya Bagamoyo ilijengwa chini ya kiwango na Waziri Husika alikuja kuichukulia hatua na Riasi na Kawambwa wanawabagamoyo walikuwepo
Barabara ya Bagamoyo ipi haswa, Msata-Bagamoyo au Bagamoyo-Tegeta?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…