Tusimung'unye maneno, barabara ya Kusini ilijengwa chini ya viwango!

Hiyo njia ya kuzunguka Tunduru,Songea,Njombe hadi Makambako hata wakati ndio ilikuwa suluhisho wakati wa masika,ila ilikuwa inachukua hadi siku tano kufika Dar,sababu Masasi Songea kulikuwa hamna lami,halafu magari yenyewe enzi zile ilikuwa Layland CD hazikuwa na mwendo mzuri kwenye milima.
Yah ila kwasasa ni same same day
 
Kumfukuzisha kazi RM Lindi ni kukosa BUSARA kwa Bashungwa, hajui au hataki kujua historia ya ujenzi wa hii barabara, hii barabara inafanana kabisa na Ile ya Dodoma -iringa na Bagamoyo-Msata! Naamini wakubwa watanielewa
Bora hata Ile ya bagamoyo msata kuliko Dodoma iringa au hiyo ya kusini.
 
Barabara sio kwamba iko chini ya kiwango ile barabara ilijengwa bila kuzingatia hali halisi ya ardhi ilivyo ,ardhi ile ukiangalia sehemu kubwa kuanzia Rufiji mpaka karibu na Kilwa sehemu kubwa iko kwenye mikondo ya mito,kwahiyo kiwango cha unyevunyevu ni kikubwa sana ,ndio maana ile barabara mara kwa mara ina mashimo kila wakati kwa ajili ya kutitia...
Huko kutozingatiwa kwa hali halisi ya ardhi ndio chini ya kiwango kwenyewe.
 
Ni ngumu kuishinda nguvu ya maji...

Ndio maana hata nchi kubwa zinapata shida kama zetu
nchi kubwa ndio zikoje mkuu zina mabawa au?
ivi kweli hata wewe huwezi kufikiria au akili zako kama za niki wa pili aliesema baada ya Mungu ni mzungu halafu yeye niki wa pili, lowest bidder kutokea milima ya uchina anawezaje kujenga barabara ya kuweza kupambana na nguvu ya maji.
 
huyo pm mwenyewe KWAO Kuna gari moja tu hadi leo na njia mbovu vile vile
Hivi huyo PM si mzaliwa na ni mwenyeji wa Kusini.. Kwanini hataki kuchonga na Bashungwa ili hii barabara ya Kusini ijengwe upya..
Maana nimechunguza hii barabara kutoka Kusini mwa Jiji la Dar yaan Mbagala Rangi3-kokoto-Vikindu-kisemvule-Mkuranga hadi kufika Masasi(Wilaya iliyochangamka zaidi katika Mikoa ya Kusini) barabara inatia huruma sana dadeq
 
Huu ndio wakati wa serikali kuamka na kufikiri kwa kina.
kila leo masikini Bashungwa yuko barabarani kukagua uozo uliofanywa na watanguizi wake.
Failure in design na viwango hafifu vya barabara zetu sasa zinatucost.
Rushwa imechangia kwa kiasi kikubwa.Pili upeo mdogo, wewe ni msimamizi unamsimamia mkandarasi,unamwita SIr hata akivurunda,hii inferiority complex inatugharimu.
Wataliani ni mafundi wazuri hasa wa madaraja wanaposimamiwa na mtu anayejitambua kama Mwingereza.Lakini Wataliano hao hao wakisimamiwa na akina Boramimi bin Mangungu ni shida,hakuna daraja au mtoto wa daraja.
 
View attachment 2983070
View attachment 2983106

Kwa wale mliopitia habari za barabara ya Dar es salm, Kibiti, Lindi Mtwara hivi karibuni, sasa tunajionea madudu ya kale.
Barabara hii imejengwa chini ya viwango.
Na tukumbuke waziri aliyehusika na barabara hii kwa kupewa misifa mingi isiyo stahili.

Barabara ina katika kila leo kwa mvua ambazo ilistahili kuhimili.
Kiwango cha ujenzi wa barabara hii huwezi kabisa kulinganisha na kiwango cha kwa mfano Iringa akambako.
Wakandarasi ni wale wale -wachina.

Serikali ijionee sasa na msimamo wake usioendelevu- ati anapewa kazi-LOWEST BIDDER!
Ujinga huu sasa unasababisha usumbufu kwa maelfu ya wananchi, ukiacha ajali zinazosababisha vifo kutokana na barabara kutokidhi viwango.

Tunavuna tulichopanda kwa misifa isiyostahili.

NB INAHITAJIKA TECHNICAL REVIEW/AUDIT
Sasa hivi kunahitajika kuwepo a Technical Review au Audit ya ujenzi wa barabara hii. Nina uhakika madudu mengi tu yatagundulika.
Ni shida
 
Kawaida tu, expansion joint hizo 🤣
 
Rushwa imechangia kwa kiasi kikubwa.Pili upeo mdogo, wewe ni msimamizi unamsimamia mkandarasi,unamwita SIr hata akivurunda,hii inferiority complex inatugharimu.
Wataliani ni mafundi wazuri hasa wa madaraja wanaposimamiwa na mtu anayejitambua kama Mwingereza.Lakini Wataliano hao hao wakisimamiwa na akina Boramimi bin Mangungu ni shida,hakuna daraja au mtoto wa daraja.
Hili lina ukweli ndani yake.
Usimamizi wa wahandisi wetu nchini tunaufahamu.
Wengi wanakuwa compromised(kununuiwa) na vihela wanavyopewa na wachina.
Hili tuamini tusiamini lipo.
 
View attachment 2983070
View attachment 2983106

Kwa wale mliopitia habari za barabara ya Dar es salm, Kibiti, Lindi Mtwara hivi karibuni, sasa tunajionea madudu ya kale.
Barabara hii imejengwa chini ya viwango.
Na tukumbuke waziri aliyehusika na barabara hii kwa kupewa misifa mingi isiyo stahili.

Barabara ina katika kila leo kwa mvua ambazo ilistahili kuhimili.
Kiwango cha ujenzi wa barabara hii huwezi kabisa kulinganisha na kiwango cha kwa mfano Iringa akambako.
Wakandarasi ni wale wale -wachina.

Serikali ijionee sasa na msimamo wake usioendelevu- ati anapewa kazi-LOWEST BIDDER!
Ujinga huu sasa unasababisha usumbufu kwa maelfu ya wananchi, ukiacha ajali zinazosababisha vifo kutokana na barabara kutokidhi viwango.

Tunavuna tulichopanda kwa misifa isiyostahili.

NB INAHITAJIKA TECHNICAL REVIEW/AUDIT
Sasa hivi kunahitajika kuwepo a Technical Review au Audit ya ujenzi wa barabara hii. Nina uhakika madudu mengi tu yatagundulika.
Unaogopa hata kutaja ni waziri gani, tuajuwa vipi; kama waziri huyo huyo kasimamia ujenzi eneo jingine ambalo barabara ni imara tuendelee kusema ni waziri ndiye mhusika?

Nakubaliana na mawazo yako, lakini tabia ya unafiki kufichaficha mambo hata yasiyokuwa na lazima kufichwa haipendezi.
Huyo waziri alikuwa nani, Kawambwa, Magufuli, au rafiki yako sasa m-Pemba ambaye ulimwandikia mada nzima humu JF ukimlalamikia; lakini wakati huu unamwaga sifa kedekede!
 
Barabara sio kwamba iko chini ya kiwango ile barabara ilijengwa bila kuzingatia hali halisi ya ardhi ilivyo ,ardhi ile ukiangalia sehemu kubwa kuanzia Rufiji mpaka karibu na Kilwa sehemu kubwa iko kwenye mikondo ya mito,kwahiyo kiwango cha unyevunyevu ni kikubwa sana ,ndio maana ile barabara mara kwa mara ina mashimo kila wakati kwa ajili ya kutitia...
Huko kuto zingatia hali halisi ya ardhi ndo chini ya kiwango kwenyewe
 
Barabara sio kwamba iko chini ya kiwango ile barabara ilijengwa bila kuzingatia hali halisi ya ardhi ilivyo ,ardhi ile ukiangalia sehemu kubwa kuanzia Rufiji mpaka karibu na Kilwa sehemu kubwa iko kwenye mikondo ya mito,kwahiyo kiwango cha unyevunyevu ni kikubwa sana ,ndio maana ile barabara mara kwa mara ina mashimo kila wakati kwa ajili ya kutitia...
Uko sahihi kabisa
 
U
nchi kubwa ndio zikoje mkuu zina mabawa au?
ivi kweli hata wewe huwezi kufikiria au akili zako kama za niki wa pili aliesema baada ya Mungu ni mzungu halafu yeye niki wa pili, lowest bidder kutokea milima ya uchina anawezaje kujenga barabara ya kuweza kupambana na nguvu ya maji.
Unashauri kazi wapewe watu kutoka nchi gani ili tutunge sheria wachina wasiombe kazi ? Unaujuzi na sheria za manunuzi au unafikiri kazi zinagawiwa bila kushindanishwa kwa ushindani wa wazi
 
Kwa ambao hawajawahi kupita hii njia wanaweza kuona utani...il ukweli hii njia kuanzia Mbagala rang 3 pale kokoto mpaka Mtwara hakuna kitu pia kutoka mnazi mmoja mpaka masasi takataka kabisa. Kuanzia masasi kuelekea Songea ndo wamejitahidi.

Zamani kidogo Muhoro-Somanga ndo palikua na mkeka angalau na ni kwasababu ulikua mpya ila baada ya muda viraka vikaanza.

Njia ya Kusini ngumu kukaa na kusoma uzi ukiwa ndani ya gari maana haijatulia hata kidogo,,wenzao wa Iringa atleast wana mkeka safi kuanzia pale Ruaha mpaka makambako.
Halafu hapo mnazi mmoja hadi Masasi ni pa zamani mno na ubovu wake
Sasa kama hadi Muhoro -Somanga pameharibika ,si upuuzi maana pamejengwa juzi tu
 
Back
Top Bottom