Tusimwadhibu Diamond Platnumz

Tutawakumbusha 2025 huu muda mnaopoteza kwa ishu za kijinga namna hii!

Badala ya muda huu mpiganie zile taasisimnazosemaga zinawanyima kura nyie mko busy na Mondi?

Kwa hiyo mondi akikosa hizo tuzo chadema inaenda ikulu?
 
wananchi gani ulitaka diamond asimame nao? kilichotokea Nigeria na bongo ni sawa? wananchi wenyewe maandamano wanakaa ndani hata chooni hawaendi unataka uwatetee kwa kipi? Hao kina davido walipata nguvu sababu wananchi almost wote walitoka barabarani kupiga udhalimu ule. Ni chuki tu kwa jamaa hamna lolote wao wenyewe ni keyboard warrior hawatoki leo mtu maarufu kama yeye mnataka aweke maisha rehani.
 
Ingetosha tu hata kuandika ujumbe mfupi kwa page zake, lakini he never did that, luunga wananchi mkono sio lazima muingie barabarani
 
Acha huo uduanzi wako kuidhalilisha Tanzania ilimradi umtetee diamond.
Tanzania hatujafikia katika huo umasikini wa kutupwa,na hata top 20 ya umasikini hatupo... report ya global finance hii hapa
 
Kiongozi muovu kwa mujibu wa nani?

Chadema ni wajimga sana aisee!

Yani unataka kila mtu afuate uanchokiamini wewe?

Yani viongozi wote kasoro Mbowe tu wamefanya mondi ndio agenda yao kuu! Alafu mnataka 2025 mshinde uchaguzi?
Kiongozi muovu kwa mujibu wa matendo yake. Cdm kiko kwenye operation zake na huku mitandaoni sio ofisi za cdm ww bendera fuata upepo. Ni wapi cdm wameongelea mambo ya Diamond kama chama? Au hujui lolote unarukia tu kila neno ukilisikia unalikimbilia?
 
Kiongozi muovu kwa mujibu wa matendo yake. Cdm kiko kwenye operation zake na huku mitandaoni sio ofisi za cdm ww bendera fuata upepo. Ni wapi cdm wameongelea mambo ya Diamond kama chama? Au hujui lolote unarukia tu kila neno ukilisikia unalikimbilia?
Unapoona Msigwa, Lema, Lisu na top leaders wengine wa chadema wameingia ulingoni kupambana na Diamond unategemea nini? Unautengaje msimamo wa Lisu na chadema?
 
Unapoona Msigwa, Lema, Lisu na top leaders wengine wa chadema wameingia ulingoni kupambana na Diamond unategemea nini? Unautengaje msimamo wa Lisu na chadema?

Kuna kikao chochote rasmi cha chama kimekaa kumjadili Diamond? Hao uliowataja leo wakisema ni washabiki wa simba au Yanga utasema ni msimamo wa cdm kushangilia hizo timu. Nakwambia ww ni bendera fuata upepo huamini.
 
Jamani mbona yeye amemkataa baba yake hamkupiga kelele leo nayeye hawamki acheni avune

 
Kuna kikao chochote rasmi cha chama kimekaa kumjadili Diamond? Hao uliowataja leo wakisema ni washabiki wa simba au Yanga utasema ni msimamo wa cdm kushangilia hizo timu. Nakwambia ww ni bendera fuata upepo huamini.
Na ndio hapo sasa kama ishu ni kutetea haki Mbona simba na yanga zote wadhamini wao ni wana ccm ila sijawahi kuona hao viongozi wako wakisusia kushabikia Simaba au Yanga?

Yani timu nzima ya viongozi wa juu wa chadema eti wanashambulia huku na huko kisa diamond?
 

Nikikuambia ww ni bendera fuata upepo naomba unielewe. Ulikuwa unasema ni cdm, nikakuambia hakuna popote cdm kama chama wamemjadili Diamond, sasa hivi unasema ni viongozi. Mbona Bananga na Prof J wamesema watampigia kura Diamond hujasema ni maagizo ya Cdm?

Hao viongozi wa simba walijihusisha moja kwa moja na siasa za dhalimu? Huyo Mo si ndio jiwe alimuagiza muovu mwingine bashite amteke? Acha kuwa bendera fuata upepo man, Diamond alijiweka kimbelembele kwenye siasa za dhalimu, acha sasa aonyeshwe siku nyingine asijihusishe na siasa za kiongozi muovu.
 
Hawawezi kukuelewa hao, njoo tujadili vizuri hili swala inbobo
 
Hayo mambo yake na mabeberu yanatuhusu nini sisi "wanyonge"?
 
Hawa kina Maria Sarungi wanasema alikuwa Dikteta sijui nini hivi nchi nyongine yeye angekuwa salama? Hebu acheni kukumbatia wazungu!
 
Alichokichagia hakikuishia pale, ndiyo kimemfikisha hapa. Hivyo kama alihofia kupoteza kipinde kile basi alishapata fungu lake, fungu hili la sasa siyo lake, ajubali kukaa pembeni na aheshimu maoni ya watu kama walivyoheshimu ya kwake kipindi kile

Jaiwezekani awe Ndumilakuwili ale huku na huku. Kusema angewezaje kipindi kile kusimamia haki mbona kuna waliosimamia?
Akina Prof Jay mbona walikubali kupoteza? Roma alikubali kupoteza hadi akatekwa na kuteswa sana lakini aligoma kupiga magoti akalazimika hadi kuikimbia familia? Kwani hao hawana historia za kutokea pagumu? Hao hawakua na kitu cha kupoteza?
Acheni utetezi dhaifu usio na mashiko
 
Siasa ni maisha, siyo burudani, Diamond ni mshirika wa Mwendazake, jazi ya ke ya burudani na umaarufu wake vinamfunga na kumlazimisha kuwa makini sana na upande anaochagua kuuegemea katika siasa. Afadhali angesema yeye alilipwa kama msanii, lakini alikiri alifanya bure sababu ya mapenzi yake na anavyomkubali Mwenda zake.
Hakuna anayemtuhumu kwa U-CCM wake, bali kwa kufungamana na mwenda zake kiasa cha kujitenga na watu pia wasanii wenzake.
Hili la hizi awards ni mwanzo atapigwa pin kila pembe ili iwe fundisho kwa wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…