Na Thadei Ole Mushi.
Diamond 💎 Platnumz ni Moja ya wasanii wanaowania Tuzo toka BET Awards kwenye kipengele Cha International ACT.
Kwenye category yake yupo na wasanii wengine wakubwa tu toka maeneo mbalimbali Duniani.
Wasanii wanaoshindania Tuzo hiyo na Diamond ni Aya Nakamura toka France, Burma Boy toka Nigeria, Emicida toka Brazil, Headie one Toka UK, Wizkid toka Nigeria, Young T toka UK na Youssoupha toka France.
Fuata link kuona washindani wa Diamond.
www.bet.com
Kwa jinsi walivyo na maeneo wanayotokea Diamond Platnumz ndiye Pekee anayetokea ukanda wa Africa Mashariki na Kati pamoja na Kusini mwa Africa. Kwa jinsi ilivyokaa Diamond angeliweza kushinda kama angelipata uungwaji mkono toka eneo analotokea.
Kilichotokea
Kwa sasa Kuna watanzania wanaoshinikiza BET kumwondoa Diamond kwenye kinyanganyiro Hicho kisa alishiriki kwenye Kampeni za 2021. Watanzania hawa wameanzisha Petition na wanasaini huko ili BET wamuondoe Diamond kwenye Award hizo. Link ifuatayo ni petition ya Watanzania kushinikiza Hilo.
BET - Disqualify Diamond Platnumz from BET AWARDS 2021 (for Best International Act)
www.change.org
Tunavyoongea watu 25,000 wameshasaini.
Huko nyuma Diamond aliwahi kuhojiwa kwa nn ameamua kuisapoti CCM akasema kuwa alifanya hivyo kwa kuwa yeye ni mwana CCM na hawezi kuacha kuiombea Kura.
Je kikatiba haukuwa haki Diamond kuwa na Itikadi ya Chama? Jibu ni Kuwa ana haki kabisa hivyo Hoja hii haina mashiko kabisa.
Hoja ya kwamba alishirikiana na Magufuli kama tukianza kuadhibu watu wote walioshirikiana na Magufuli Nani atakayebaki? Hata wapinzani wengine waliokuwa Serikalini kwa maana ya nafasi za kiutumishi kipindi Cha Awamu ya Tano walificha Kadi zao kabisa.
Hivi mlitaka Diamond ampinge JPM katika mazingira yaliyokuwepo angeponea wapi? Waliojaribu kufanya hivyo nini kiliwatokea?
Tusizime jitihada hizi za Naseeb.
Diamond katokea mbali Sana hadi kufikia hapo alipo. Ni mpambanaji haswa na amefanikiwa kuwabeba wenzake wengi tu. Naamini kama Kuna kijana wa kumsaidia afanikiwe basi ni Diamond kwa kuwa kila anapofanikiwa hushika wenzake mikono na kuwainua.
Nyuma yake wapo watu wengi Sana wananufaika na mafanikio yake. Tunaweza kuona kama tunamwadhibu yeye lakini wengi watakuwa wanaumia. Naamini kwa alipofikia hatakosa Pesa ya kula lakini Taifa linahitaji Sana mafanikio yake ili kwanza kulitangaza Taifa letu na kufungua Fursa nyingine za kiuchumi lakini Cha pili kutusaudia kuendelea kuajiri vijana wengine wanaomzunguka.
Hebu watanzania tufikirie tofauti. Tumsaidie afikie MALENGO makubwa zaidi.
Lakini Pia watanzania tusipende kushikiwa akili na watu eti Diamond nyimbo yake ya acha nikae kimya ulilenga kuwanyamazisha watu. Labda tuusikilize Tena na wabobezi wa fasihi wataelewa alichomaanisha Mondi.
Wenye petition hii waiondoe tusonge Mbele. Tusahau ya Nyuma tulijenge Taifa Letu.
Naomba kuwa Tofauti.
Ole Mushi
0712702602.