Tusipochukua maamuzi magumu Taifa letu la Tanganyika litapotea kabisa

Indeed, Lissu is damn smart. Damn Smart and a Principled Man.

ILA MASWALI MUHIMU NI HAYA :
a. Je, Acacia walikuwa wamesajiliwa hapa nchini ???

b. Je, Acacia walikuwa wanalipa kodi stahiki hapa nchini ???

c. Je, Acacia walikuwa hawaibi madini kinyume na utaratibu uliowekwa ???

d. Je, Lissu kutishia kwamba tutashitakiwa MIGA alikuwa sahihi kisheria ???



Nimeweka The MIGA TREATY 1985( As Amended in 2010) napo bado unabisha tu ???

=================================================================
Mheshimiwa Tundu Antipasi Lissu mwaka 2015 na CHADEMA walishawahi kufanya makosa makubwa mno ambayo kama yangefanikiwa yangeigharimu vibaya sana hii nchi. Marehemu ndugu Edward Ngoyai Lowassa, alikuwa MWANAMTANDAO MWANDAMIZI aliyehusika kuifikisha nchi yetu hapa ilipo leo.

Mwaka 2008, CHADEMA walituaminisha kwamba Ndugu Edward Ngoyai Lowassa ni FISADI MKUBWA. Ilipofika mwaka 2015, wakaanza kumsafisha na kumpa dhamana ya kupeperusha BENDERA YA CHADEMA kugombea URAISI. Kipindi kile Lowassa alikuwa akishirikiana na ROSTAM AZIZ, Apson Mwang'onda na mamia ya matajiri. Unadhani Mheshimiwa Lissu alikuwa sahihi katika hili ???

Kama hakuwa sahihi hapa, basi ni BINADAMU ambaye ni FALLIBLE kama sisi wengine. Hivyo ni lazima kwanza tufahamu kwamba tunafanya kazi ni binadamu, hivyo tuweke MIFUMO IMARA na KULAZIMISHA UWAJIBIKAJI na KUTII KANUNI, kwa kila mtu ndiyo twende mbele kama nchi. Bila hapo ni kujilisha upepo tu.
​
 
Kwa nini hakuwahi kupeleka mikataba ya madini kujadiliwa bungeni??
Mkuu my point actually.

Kwa nn wanajeshi wa Marekani hawakuwakamata wale mabaharia waliodaiwa ni wauza ngada?

Kwa nn wakawaua pale baharini?
 
Kuhusu Lowassa nadhani alifafanua kwamba kwanza walijua fika asingeshinda na hata kama angeshinda asingetangazwa.

Pili ambalo ndilo lengo kuu lilikuwa kujizolea idadi kubwa ya wabunge ili kwenda kuchochea mabadiliko ya msingi huko Bungeni.

Simtetei TAL. Niko tu kwenye hoja.
 
Kama unakubali Lissu ni damn smart na very well principled man basi hoja yangu inaishia hapo.

Kuhusu MIGA ninachofahamu ali i quote kumaanisha hatua zilizokuwa zinachukuliwa na Serikali kuhusu sekta za madini zilikuwa zinaliweka Taifa kwenye hatari ya kushtakiwa.

Najua unajua lile kama onyo lake lilikuja kutimia maana baada ya kufutwa kwa retention licences Serikali imeshtakiwa kwenye makesi mengi sana ambayo tumelipa ma trilioni ya fedha. Fedha za walipakodi masikini wa nchi hii.

Kesi zingine zikapelekea hadi ndege zetu kuzuiwa na kukamatwa. Najua hili pia unalijua
 
Kwa nini aliua kwa mabavu upinzani bungeni??
Upinzani upo toka 1992 ulifanikiwa nini kuzuia wahuni na uhuni wao kwenye mali za umma?
Kikwete aliwapa sana nguvu wapinzani ndani na nje ya bunge lakini yaliibuka makashifa mazito ya RICHMOND, ESCROW, n.k.
Katiba mpya maoni ya wananchi kwenye rasimu ya katiba mpya chini ya Warioba na wenzie ilivurugwa upinzani ukiwa na uhuru mkubwa kufanya siasa.
 
Kila alichokisema Lissu kilitimia
 
Hujajibu swali,
Kwa nini aliua kwa nguvu upinzani nchini?
Tanzania imefaidikaje kwa upinzani kuuwawa na jiwe?
 
Hujajibu swali,
Kwa nini aliua kwa nguvu upinzani nchini?
Kwasababu uliondoka kwenye misingi ya kupigania taifa.
Unafikiri kutekeleza agenda ya kupinga ufisadi na kumpokea Lowassa 2015 kisha kumpa kugombea uraisi CDM walikuwa sahihi?
Umewaona waliompokea Lowassa na kuibuka kwa CHAUMA?
 
Kwasababu uliondoka kwenye misingi ya kupigania taifa.
Unafikiri kutekeleza agenda ya kupinga ufisadi na kumpokea Lowassa 2015 kisha kumpa kugombea uraisi CDM walikuwa sahihi?
Umewaona waliompokea Lowassa na kuibuka kwa CHAUMA?
Kwa nini aliwapokea tena Rostam na Lowassa??
 
Tatizo hata hii Katiba mbovu bado wanavunja.
Naamini hata tukipata mpya wataivunja pia. Kuna kitu lazima kifanyike kuzuia watu wasivunje katiba. Kisha tuunde katiba mpya.
Mi naamni mahakama ingekuwa kama TLS yaani viongozi wake watokane na wanasheria na si teuzi za wanasiasa, bunge likawa na wagombea binafsi wasitokane na vyama tu. Tungefika mbali sana
 
Inakuwaje rahisi wakati wahuni na wanamtandao ndo wameshika mpini?
Ukileta ubishi na ujuaji unatekwa na kutulizwa chap
 
Pia kuna mahojiano yake yapo hadi YouTube Lissu amekiri kuwa walifanya kosa kumkubali Lowassa.

Kama unavyosema. Hatumtetei Lissu ili kumtetea tu ila kusema ukweli he is a rare gem kwenye kizazi chetu sisi Watanzania kilichojaa utapeli na unafiki.

Lissu ni mkweli sana na mara nyingi hata anapokosea anakuwaga tayari kuwajibika kwa kusema kuwa mahali fulani nilikosea au tulikosea.
 

..asante kwa kutoa ufafanuzi mzuri kuhusu MIGA.

..sidhani kama kuna mwanaJF alijitolea kuelezea suala hili kwa kirefu kama ulivyofanya.

..Majibu yako yanafafanua kilekile nilichokieleza.

..MIGA jukumu lao ni kulinda wawekezaji dhidi ya hatua mbalimbali ikiwemo UTAIFISHAJI ktk nchi walikowekeza.

..Je, Magufuli hakutishia kutaifisha mali za Acacia?

..Kama ni kweli basi Tundu Lissu alikuwa sahihi kusema Tanzania inaweza kushitakiwa MIGA.


NB:

..Hakukuwa na ulazima wa ku-publish ripoti za UONGO.

..Sio sahihi kukusanya the best brains in the country kuhusu masuala ya madini, fedha, na kodi, halafu ukawaamrisha watengeneze madai BOGUS.

..wale Maprofesa walitakiwa waandae ripoti na ushahidi ambao tukiupeleka popote duniani Tanzania itashinda.

..Accacia walikwenda mahakamani kwasababu walikuwa wanajiamini watashinda.

..actually moja ya madai yao ilikuwa mazungumzo hayasongi mbele, yamekwama.

..kesi iliondolewa baada ya minority shareholders kupewa cha kwao na Barrick kuendelea na mazungumzo na serikali.
 
Hii ni muhimu sana ili kuiponya nchi na kurejesha upya uzalendo kwa wananchi
 
Hii ACCOUNT nimegundua ni ya CHAHALI.

Sioni HOJA ya msingi hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…