The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 4,249
- 11,592
Hiyo ndugu MALCOM LUMUMBA imeniacha solemba...Mwaka 1975, baada ya IDARA kufanya mauaji makubwa na kuonea raia wake kule kanda ya ziwa, Mzee Nyerere alichukua maamuzi magumu mno. Alifukuza kazi MAAFISA USALAMA kuanzia wakurugenzi waandamizi, WAZIRI OFISI YA RAISI na WAZIRI WA MAMBO YA NDANI, hadi POLISI.
Mzee Nyerere kurudisha heshima alivunja kabisa IDARA, na kuteua MKURUGENZI msomi DR. Laurent GAMA aiongoze. Tofauti na ule utaratibu wa zamani wa kujaza TANU YOUTH LEAGUE ambao wengi walionekana kuwa THUGGISH and SADDISTIC, kina Dr. Gama waliaenda kufanya En Masse Recruitment mashuleni na vyuo vikuu.
Rucruitment ya 1975, ndiyo ilileta watu kama Membe, Mizengo na wengine ambao binafsi nawafahamu walioenda kupata mafunzo ya kinidhamu nje ya nchi. Walau IDARA iliendeshwa kiheshima, hasahasa baada ya kuona Mzee Emilio Mzena na Mzee Peter Siyovelwa ambao waligeuza IDARA kama mali yao binafsi wametimuliwa. Huyu Siyovelwa siku maafisa wameitwa Ikulu kwenye kikao aliinuka na kuanza kumtolea Mzee Nyerere maneno ya kashfa akimnyooshea kidole na kumwambia "Wewe Julius unahisi hii nchi ni yako peke yako"
Huyu Peter Siyovelwa alikuwa kama mungu-mtu. Ukimuona kwa nje-nje hivi unaweza ukasema ni mtu mwenye bashasha lakini ni moja kati ya watu waliochochea ugomvi baina ya Mzee Nyerere na Mzee Kambona. Ilifika hadi kipindui pale Iringa wakiteua WAKUU WA MIKOA wanawake alikuwa anapiga simu kwa Raisi au Waziri Mkuu, akisema hataki. A Megalomaniac Per Excellance.
SASA WATU AINA HII, ambao wanadhani wanaweza kutoa uhai wa binadamu mwenzao bila kuwajibika ndiyo wamejazana CCM, TISS, TPDF na PT. Wengine hujiita ni WAZALENDO. Ila ukweli ni kwamba MWANADAMU asipowekewa mipaka ndiyo kinatokea kile kilichotokea mwaka 2017 kwa Tundu Lissu.
BOOKMARK THIS: Siku Tundu Lissu anatolewa nje, Amin Amin nawaambia, tutafahamu madhambi mengi ya Ndugu Humphrey Polepole ambayo aliwahi kuyafanya. Pia sidhani kama atakuwa na uwezo wa kujibu hoja za Lissu. Wakati hili linatokea, WATANGANYIKA wengi watakuwa washachagua upande kati ya Lissu au Polepole. SUBIRI UONE
Ndo kusema kuwa Tundu Lissu anayajua mengi ya Humphrey Polepole kuliko anavyijijua yeye Polepole, au siyo..?
Haya bhana. Hopefully kuwa, Tundu Lissu Jumatatu tarehe 8/9/2025 mahakama itamrudishia haki ya uhuru wake ili tuione hii battle...