Tusipochukua maamuzi magumu Taifa letu la Tanganyika litapotea kabisa

Tusipochukua maamuzi magumu Taifa letu la Tanganyika litapotea kabisa

Mkuu wasomi wengi walikuwa wanaenda kusoma nje kwa kupelekwa na Serikali ya Nyerere na wengi wao walikua wanaenda kusoma vyuo vya Russia, Israel na China, Uingereza, na kwa miaka hiyo ya 1975 ilikua rahisi kusafisha udara kwasababu idada yao ilikua ni chache na mifumo yao haikua haijajichimbia kwenda mbali, tofauni na sasa ambapo Magufuli alishindwa kwasababu wana mtandao wametapaka ndani na nje kwa wingi ili kuwasafisha Magufuli aliitajika kukaa madaraka zaidi ya miaka 10 na anayempokea kijiti awe wa mfumo wake. KingineMagufuli kilichokua kinampa tabu ni kutokana na jamii aliyotoka hawakua sehemu za vyombo vya Usalama ndiyo shida ilipoanzia. Kwa mfano Heche akiwa Rais ataweza kuumaliza mtandao kwa urahisi kutokana na jamii aliyotoka itamsaidia kupambana na wanamtandao na kuua kabisa.
Una uhakika Wakurya ndani ya Idara ni wengi? wakurya wapo JWTZ. Idara iimejaa watu mababila yasiyo na watu wengi ndani ya JWTZ.
 
Hii hoja yako ni mfu. Nani kakumbia wafanyakazi wa Idara wote lazima wale wasomi wa vyuo vikuu? Recritment ya Idara huwa inafanyika hadi kwenye ngazi za shule za Sekondary na mitaani pia. Hao wasomi wa ngazi za juu wanaohitaji siyo wengi kiasi cha kuhitaji kuwa na vyuo vikuu vingi. enzi za Nyerere hatukuwa na vyuo vikuu vingi wala hatukuwa na wasomi wengi wa vyuo vikuu lakini Idara yetu iliheshimika na ilitenda kwa weledi. Na hata baada kuivunja na kuiunda upya mwaka 1975 bado ilifanya kazi bora.
Usiwe unadandia gari kwa mbele
 
MAMBA HUWA ANA NGUVU AKIWEPO NDANI YA MAJI TU.

TAASISI zote za kiusalama duniani kote zina kitu kiitwacho INTEREPOLABILITY. Ambapo mafanikio ya kazi ya JASUSI X inategemea mafanikio ya kazi ya JASUSI Q, tena huenda hata hawafahamiani, wala hawaji kufahamiana. TAASISI haifanyi kazi ikitegemea MTU, bali watu ambao wakiwa wengi hutengeneza MFUMO ambao huwa unakuwa na lengo moja.

Wewe hata uwe JASON BOURNE, JAMES BOND au JACK RYAN usipokuwepo ndani ya MFUMO, huna utofauti wowote ule na MAMBA aliyepo nje ya MAJI. Ndiyo maana hata unapostaafu kuna baadhi ya SECURITY CLEARANCES unabaki nazo, kwasababu wewe umuhimu wako kwa MFUMO utaisha siku pale unapofariki tu.

Sasa wakitaka kukushughulikiwa, kwanza kabisa wanafanya REVOCATION OF SECURITY CLEARANCES, aidha kwa kukataza USIPEWE TAARIFA MUHIMU, au KUPANGARUA BAADHI YA IDARA kwa kuhamisha watu, kuwapa teuzi, kuziunganisha idara (Merger), kuiweka idara moja chini ya nyingine (Subordination) au kuua watu muhimu kwenye idara. Wakishakufumba macho hivi, aidha wanabana fedha zako au wanakuua.

Mataifa mengine, kama UCHINA na URUSI njia yao ni MOJA TU ambayo kwangu mimi naamini ITS THE MOST EFFECTIVE METHOD. Unawapa majasusi "The Scarlet Letter", ambayo itakuhakikishia A CLEAN SLATE, ya kuanza upya. Sema ndiyo hivyo hapa Afrika Mashariki aliyeweza kutoa The Scarlet Letter ni General Paul Kagame tu, ndiyo maana Rwanda mbali na ujinga wa UKABILA, mambo yanaenda.


====================================================
Kule Rumi ya Kale (Ancient Rome) vyombo vya usalama vilikuwa vina adhabu iitwayo DECIMATION, ambapo wanajeshi walikuwa wanagawiwa katika vikosi vya MAKUMI, MAMIA na MAELFU. Tatizo likitokea kwenye kikosi moja unamchukua kiongozi wao unamuambia awaambie wenzake wale tisa wamuue wa kumi. Au wale tisini wawau wale kumia. Au mia tisa wawaue wale mia.

Hili lilileta heshima mno kwa majeshi ya Warumi ambapo wakubwa wa vikosi walifahamu fika kabisa, tukileta uzembe tutaambiwa tuue wenzetu wa kikosi kimoja ambao bahati mbaya sana walikuwa ni watoto wao, wakwe wao au ndugu zao. Hata MONGOLS jeshi lao lilikuwa na nidhamu kwasababu ya adhabu ya DECIMATION.

Ukiisha ingia kwenye vyombo ya usalama ni lazima uwe na nidhamu. Nchi ambayo maafisa wake hawana nidhani huwa haidumu muda mrefu. Hawa watu huwa wanapewa mafunzo, wanafahamu siri na kudekezwa kama mayai kwa mishahara na marupurupu. Wanapoharibika na tamaa, hakuna njia ya kuwarudisha kwenye mstari zaidi ya kuwapeleka mapema ahera.

TANZANIA ilipofika, ili kuokoa nchi ni lazima TUCHUKUE MAAMUZI MAGUMU bila kuonesha hata CHEMBE YA HURUMA, wala SONI. WEWE ambaye umesomeshwa kwa hela za walipa kodi, ukawa hadi Balozi, watoto wako wako International Schools halafu ukasaliti kiapo chako, ulitegemea kitokee nini ??? A Bullet at the back of your head or A Noose around your neck.
​
Hichi ndicho wanacho ogopa ccm
 
Dawa ya kutovunja katiba ni ndogo sana.

Kuondoa kinga ya kushtakiwa kwa Viongozi wote wa Kisiasa na kuweka makosa ya kukiuka katiba kuwa makosa ya Jinai.

Alafu vyeo vyote vikuu vya kiutendaji unaviwekea ulinzi wa Kikatiba. Wanateuliwa ila hawawezi kutenguliwa.

Mbona simple sana
Naunga mkono
 
Yaan kwa idadi ya wanaharakati waliokufa kutupambania na hakuna action yoyote tumechukua,itoshe tu kusema...sisi tukishiba chakula inatosha.
🤣🤣🤣🤣🤣 Tatizo letu sisi Wanyonge hatuna umoja afu ni Waoga vibaya sana!
 
Una uhakika Wakurya ndani ya Idara ni wengi? wakurya wapo JWTZ. Idara iimejaa watu mababila yasiyo na watu wengi ndani ya JWTZ.
Sasa ni rahisi kuwavumua na kuingiza kwa temporarily kuliko kuanza kuajili wapya kwa mara moja
 
Mkuu MALCOM LUMUMBA

Hongera kwa andiko murua lenye nyama nzuri zilizoshiba kweli.

Hili kwangu ndo andiko bora kabisa la mwaka huu pamoja na kutofautiana na wewe sehemu chache.

Kuhusu watu wanaoipigania kweli Tanganyika unakosea sana kuwaondoa Mange Kimambi na Maria Sarungi.

Hawa wanawake nimewafuatilia kwa muda mrefu sana na kusema kweli wamekuwa wanaonesha consistence kwenye kile wanachokipigania.

Shida ni Watanzania kuendekeza ujinga na Watawala kuwaliisha Watanzania Ujinga.

Nakubaliana na wewe kuhusu Mabadiliko ya Sheria ya TISS ya mwaka 2023 kuwa msumali wa mwisho kuiangamiza Taasisi hii ambayo ilishaanza kujifia baada ya Kikwete kui compromise vibaya sana kisiasa na kundii lake.

Sheria ya TISS haijafanya kosa la kumuondoa KMK na Waziri tu. Wamefanya kosa kubwa zaidi kwa kuweka kisheria Mkuu wa Idara kwa Upande wa Zanzibar kuwa lazima awe Mzanzibari wakati suala la Ulinzi na Usalama Kikatiba ni suala la Muungano.

Ingawa practically Wakuu wa TISS upande wa Zanzibar wamekuwa Wazanzibar ila lile kutokuwepo Kisheria liliweza kuzuia subbotage ya Rais wa JMT inayoweza kufanywa kupitia Idara kutokea Zanzibar maana kwa kuwa Sheria haikuwa inasema chochote inngewezekana mtu yeyote kuwa Mkkuu wa Idara kwa kule na kuepusha ssabbotage kwa Tanganyika.

Nchi hii kuna mambo mengi sana yalifanywa kisheria ila kwa nia mbaya. Kuwafanya Mawaziri kuendelea kuwa Mawaziri hata baada ya Bunge kuvunjwa ni moja ya Mambo ambayo yalifanywa kimkakati sana ili kuiondoa Nchi kwenye usimamizi wa mifumo na kiuweka mikononi ya Wanasiasa.

Sio hivyo tu. Hata Mhimilii wa Mahakama kuwekewa chini ya Ma DC na RC kinidhamu kwa Mahakimu ni moja ya Mambo yaliyofanywa kimkakati kabisa na kusababisha kuuaa mifumo imara iliyotengenezwa kulisimamia hili Taifa.
Mange hana consistency mkuu!
 
Mange hana consistency mkuu!
Kati ya wanawake Watanzania 10 wanaojielewa vizuri hapa duniani Mange anaweza kuwa No. 1 au 2

Ni sisi tu Watanzania tunamwangusha ila yupo vizuri sana kwenye kusimamia Haki na Utawala Bora.
 
UTANGULIZI:
Habari ndugu MTANGANYIKA, leo ni mambo mengi kweli ya kusema ambayo yanatatiza sana moyo wangu. Nimejaribu kuandika wiki kadhaa lakini naishia kufuta kila nikimaliza kuyaaandika. Mengine nikiyasema hadharani yanaweza kuwaumiza sana moyo na mkaishia kukata tu, tamaa. Ila itoshe kusema kwamba TANGANYIKA ISHAUZWA.

1.TANGANYIKA KUTETEWA NA WANAHARAKATI WALIOWAHI KUTUHUJUMU:
Ndugu Humphrey Polepole na pamoja na wanaharakati wengine wa mtandaoni kama Mange Kimambi na Maria Sarungi, watu ambao kwa nyakati tofauti waliwahi kuwa wanufaika wa mfumo na hata kutumika kuhujumu wananchi. Mtu pekee ambaye amekuwa akisema ukweli siku zote ni kaka yangu Evarist Chahali (He has been very Consistent and Objective).

Miundombinu mingi ambayo Samia anaitumia kututesa WATANGANYIKA, ilitengenezwa na Raisi John Pombe Magufuli. Humphrey Polepole na Dr.Bashiru Ali Kakurwa walikuwa ni wahandisi wakuu wa kisera. Ilifika kipindi hadi Dr. Bashiru alitamka wazi kwamba CCM inaweza kuvunja katiba ili kubaki madarakani kwasababu ndiyo imeshika dola.

Hawa wengine kama Maria Sarungi, na Mange Kimambi tunafahamu kwamba madai mengi yalianza kama maslahi binafsi. Hasahasa Binti Sarungi ugomvi wake mkubwa na JPM chanzo ni mambo ya kifamilia ambapo yeye kama munfaika wa mfumo alikutwa na SHOCK-THERAPY ya JPM. Alikuwa na mwenzake Fatma Binti Karume, ambaye mlimbatiza jina na kumwita Shangazi, lakini awamu hii rangi zake naye mshaziona.

Mange Kimambi, ni mamluki. Alishawahi kuwa upande wa CCM, baadaye dhidi ya Lowassa, baadaye upande wa Lowassa dhidi ya Magufuli. Baadaye kushangilia msimba wa Magufuli na kumnadi Samia, na saa hizi yuko dhidi ya Samia. WATANGANYIKA hatufahamu kesho atakuwa dhidi ya nani.

Hii dhambi naona inatafuna wengi mno hadi maafisa usalama ambao binafsi nawafahamu waliwahi kuwa mstari wa mbele kutetea kila ujinga unaofanywa na dola, ambapo mamia ya WATANGANYIKA walipoteza uhai, kuumizwa, kufungwa au kufilisiwa. Hata humu JF wengi nawafahamu, naona kabisa mwelekeo wao ni watu aliyepagawa na pepo au kapata wazimu.

WATANGANYIKA, ili kuepukana na kadhia hii ya kubebwa na kila aina ya upepo wa kimaslahi wa watu ni lazima WASOMI wajifunze kusimamia kitu kinachoitwa KANUNI (Principles). Hata pale ambapo mwanasiasa unayempenda anakosea, wewe inabidi uufunde moyo wako kusimamia KANUNI.

RAI YANGU KWA WATANGANYIKA, hasa WANAUSALAMA: Kwenye BIBLIA, Daudi alikuwa ni mtenda dhambi mkubwa kama sisi tu, lakini tunaambiwa ni moja kati ya watu walipata kibali kikubwa sana kwa MUNGU. MUNGU alisema wazi kabisa kwamba anampenda Daudi kwasababu MOYO WAKE HAUNA HILA. Daudi alikuwa ni mtu mwenye kusimamia KANUNI.

Mfalme Sauli alikuwa anamuwinda amuue Daudi. Mara mbili Daudi alipata nafasi ya kumuua kabisa Sauli, kwa mambo aliyomtendea lakini Daudi alisimamia KANUNI. Alikataa kumuua na kusema HUYU NI MPAKWA MAFUTA WA MUNGU, atamalizana na MUNGU wake.

Daudi alikuwa ni KIONGOZI MKARIMU (Equittable). Kuna sehemu kwenye BIBLIA ilitokea vita, na baadhi ya askari wake walichoka wakashindwa kwenda vitani. Waliporudi na kupata ushindi mkubwa na mali nyingi, kuna baadhi ya askari wakasema hawa ambao hawakwenda na sisi vitani wasipewe chochote kile. Daudi aliwakemea na kusema aliyekwenda vitani, na aliyebaki kulinda mji wote watapata mali sawa. Akimaanisha kwamba kila mtu ana umuhimu ndani ya jamii.

Daudi alikuwa ni KIONGOZI MUUNGWA. Alikosea mno kwa kuiba mke wa mtu na kumpa mimba, huku akimuua mume wake. Baadaye alipofutwa na nabii Nathani kuambiwa ukweli, wala hakutafuta vijisababu, bali alikuwa mpole na kwenda kuomba msamaha mbele ya taifa zima. Hakusema kwamba yeye alikuwa na nia njema, ila alisema wazi kwamba amekosea.

SASA BASI: wale ambao mliwahi kuwakosea WATANGANYIKA, na kusababisha vifo, misiba, umasikinui na majeraha ombeni TOBA KWA MUNGU, OMBENI TOBA KWA WATANGANYIKA, lakini kubwa zaidi TOBA YA KWELI huambatana na mabadiliko ya moyo. Jaribuni kukaa kwenye viatu vya watu kama Wazazi wa Ben Saanane, Familia ya Gwanda, Familia ya Soka, Familia ya Akwilina na wengine kisha mtafahamu kwamba WENGI HAMKUISHI VIAPO VYENU.
​
2. UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU YA USALAMA WA TAIFA ILIVYOANZA
Idara za usalama duniani kote huongozwa na kitu kiitwacho COMPARTMENTALIZATION. Wanausalama wa chumba namba SABA hawatakiwi kufahamu kinachoendelea chumba namba MBILI. Wameenda mbali kabisa kwamba wanausalama wa chumba namba KUMI, hawatakiwi kuwafahamu wanausalama wa chuma namba NANE. Lengo zima ni kulinda usiri na weledi wa taasisi.

Baada ya MTANDAO kujipenyeza ndani ya CHAMA na SERIKALI, walivuruga utendaji kazi mzima wa taasisi za kiusalama hapa nchini. Taasisi kuu za kiusalama hapa nchini ziko tatu (PT, TISS na TPDF-The Cerberus of the State), hazikuwa zinafanya kazi kama inavyotakiwa.

Mwaka 2015, JPM amekuwa Raisi na kukuta wakubwa wengi ndani ya taasisi ni wale wa miaka kuanzia 1992, vijana wengi ni wale wa kuanzia 1996 na wapya wengi ni wale wa Jakaya. SHIDA YA TAASISI ZA KIUSALAMA, ni kwamba huwa mnaapishwa wote siku moja, na mnastaafu wote siku moja au mwaka mmoja, kama mtatofautiana basi ni miaka isiyozidi mitano.

Ndani ya TAASISI, huwa kuna IDARA MBALI-MBALI, kwasababu ni mwiko kuweka mayai yote ndani ya kapu moja(All Eggs in One Basket), maana yakivunjika inakula kwako. Afisa anapoenda kufanya oparesheni kubwa, ni lazima ajaze fomu na afanye utaratibu maalumu kwenda kuomba vifaa vya kufanyia kazi kutoka kwa watu wa IDARA NYINGINE, ambao wanavitunza.

Mfano, unatafuta kuua magaidi. Unafanya utaratibu wa kwenda kwenye IDARA yenye watu wenye mafunzo maalumu ya kijeshi, ambao hao watatakiwa kwenda kuomba silaha maalumu za kufanyia oparesheni kutoka kwenye IDARA nyingine inayotunza silaha. Kuna silaha kama SUMU (Chemical Weapons) huwa zinatunzwa kwenye ghala maalumu chini ya IDARA maalum SURVEILLANCE DEVICES, nazo zinakuwa chini ya watu wa IDARA nyingine.

Sasa operesheni inafanyika kwa kuunganisha idara hata zaidi ya tatu ndani ya TAASISI ya usalama. Mara nyingine tatizo likiwa kubwa sana hata PT, TPDF, MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS na MINISTRY OF FINANCE huhusishwa. Katika hili sasa ndipo MTANDAO walikuwa mbele ya Raisi JPM hatua tano zaidi. Kila akiratibu jambo kwa siri, taarifa zinavuja kutoka IDARA moja kwenda nyingine mwishowe zinafika kwa MTANDAO.

Leo umetuma watu kuchukua SUMU, watu wa ile IDARA kwa akili ya haraka wanajiongeza kwamba, kama SUMU inachukuliwa basi ni lazima kuna POLITICAL ASSASSINATION, hivyo taarifa zinavuja kwamba kuna Dangerous Substance imetoka maabara, na imebebwa na watu wa IDARA fulani hivyo wafuatilieni mwanzo mwisho. AU kuna watu wanafuatiliwa na IDARA ya IT, simu zao zimeingiziwa PERGASUS, taarifa zinatoka tu.

Mzee JPM kazidiwa ujanja, SULUHISHO NI NINI ??? Unda TASKFORCE na fanya En-Masse Recruitment, wape vijana mafunzo (Voda-Fasta) halafu waingizwe mitaani. Anza mdogo-mdogo kuchomoa baadhi ya maofisa ndani ya TAASISI, ambao una uhakika walipenyezwa na watu, lakini zuia Rectruitment nyingine isifanyike bila wewe kujua. Hapa ndipo wakazaliwa WATU WASIOJULIKANA.

Kweli TASK-FORCES, zinasaidia USIRI. Tatizo ni kwamba hazifanyi kazi kwa kufuata sheria. Maana ndani ya TAASISI, kila oparesheni inayofanyika ni lazima itakuwa AUDITED tu. Operesheni nyingi na fedha zake ni lazima zipitishwe na utawala wa kiraia (Civilian Administration) ili kuhakikisha TAASISI hazifanyi mambo ya ajabu kama kutaka kupindua nchi, au kutumika na watu binafsi kufanya hujuma.

Hata kipindi cha JK, taarifa zilikuwa zinavuja kwasababu ya huu mlolongo nwa KIIDARA ambao uko kisheria. Mambo mengi yalikuwa yanamulikwa, ndiyo maana kuna mipaka hata yeye na UFISADI wake alikuwa anaogopa kuivuka. Mzee JPM, kaanzisha TASK-FORCE, zina watu lakini wengi siyo PROFESSIONAL and SEASONED-VETERANS. Tatizo ni kwamba ukiwataka PROFESSIONALS unakuja kuambiwa wengi wanafahamiana, au wengi walienda mafunzo kambi moja, au wengi walifanyiwa mafunzo na kuingizwa kwenye taasisi na WANAMTANDAO waliowahi kuwepo ndani TAASISI.

MATOKEO ni NINI ??? Oparesheni nyingi zinaanza kufanywa kiholela kwasababu kwanza kabisa hazina wataalamu ambao wengi wangeweza kuuliza maswali, kutoa ushauri wa kitaalamu, au hata kukataa kufanya mambo ya ajabu. Lakini pili, kwasababu hakuna sheria inayounda TASK-FORCE wala kuzisimamia kila kitu kinakuwa ni halali. Wengi wataua watu, watateka na kutesa watu bila hata sababu zisizo za msingi.

Chanzo chote cha haya ni MTANDAO ambao umevuruga nchi na kujipenyeza kila sehemu na kumsababishia Mzee JPM awe na hofu muda wote (Paranoia). JPM alikosea na kiukweli mbali na kufanyiwa hujuma, huyu Mzee wetu alikuwa ni mtu mwenye tabia ngumu tangu uwaziri. Tunaweza kusema kuna baadhi ya maadui aliwatengeneza bila ulazima wowote ule. Angekua ni mtu mwenye kutuliza kichwa, sidhani kama MTANDAO wangemshinda.

Kiufupi, alichokifanya Mzee JPM na TASK-FORCE zake, hakina utofauti sana na kile ambacho Marehemu Mzee Jiang Zemin wa Uchina alikifanya mwaka 1999 kwa kuanzisha OFFICE 610, ambapo alishawishi CHAMA CHA KIKOMUNISTI kwamba waruhusu ianzishwe ili kupambana na makundi hatari kama The Falun Gong, nje kabisa ya mfumo wa Guaonbu (THE MINISTY OF STATE SECURITY).

Katika hili alifanikiwa mno, sema tatizo ni kwamba OFFICE 610, ilianza kutumika vibaya na MTANDAO wa Jiang Zemin a.k.a The Shanghai Clique ambao ulikuwa umejaa watoto wa vigogo (Princelings) kama Bo Xilai ambao walitumia OFFICE 610 kupata Uraisi, hadi mwaka 2012 kudiriki kutaka kumzuia Raisi Xi Jinping asiapishwe kwa kusambaza vikosi vya majasusi zaidi ya 15000 na askari zaidi ya 80,000 waliopo Tibet na Xi Njian wakisingizia kufanya mazoezi.

Hivyo TASK-FORCE zinasaidia, lakini bila usimamizi mzuri chini ya watu aina ya Bashite na Mafwele zinaweza kuvuruga kabisa mchakata wa kiutawala ndani ya nchi hasahasa pale zinapokuwa tayari kubwa na zenye askari wengi na rasilimali nyingi. Tulipofika, haitakiwi TAASISI yoyote ya kiusalama kufanya jambo kubwa bila usimamizi wa kisiasa (Civilian Oversight).

Bahati mbaya sana sasa, Raisi Samia kaingia Ikulu na amegundua kwamba kuanzisha FORCE-WITHIN A FORCE a.k.a TASK FORCE zina manufaa mengi kisiasa hasahasa pale unapotaka mambo yake yaende haraka, bila usimamizi wowote ule wa kisheria (Legal Scrutiny) na ushahidi (Incriminating Evidence). Mbali na NIDA+CCM+NEC kuwa na hatihati ya kumnufaisha Raisi Samia, hiyo mifumo ya FORCE-WITHIN A FORCE a.k.a TASK FORCE ambao ulianzishwa na Mzee JPM kupambana na MTANDAO, leo hii unatumiwa na MTANDAO kupambana na WATANGANYIKA.

RAI YANGU: Watanzania tusikubali TAASISI za kiusalama zitumike kisiasa bila kuwawajibisha viongozi wanaofanya hivyo. Lazima tufuate KANUNI, ili kuzuia madhira kama haya yanayolikumba hili taifa letu. Leo hii kuna baadhi ya wafanyabiashara wanaweza wakakuchukia tu, na wakaamua kupiga simu moja tu kwa hawa watu wa TASK-FORCE na tusikuone tena mtaani.

Pia mara nyingine unaweza ukalaumu Polisi, Maafisi na Wanajeshi kwamba kwanini mnafanya mambo kinyemelea na kihuni bila weledi wowote ule, bila kufahamu ukweli ni kwamba ndani ya taasisi zao kuna vikosi maalumu (TASK-FORCES) zinazofanya kazi za wanasiasa bila kuwa CIVILIAN AUDITED, tena vimejaa maofisa ambao hawana ujuzi wala uzoefu mkubwa.
​
Salute mkuu wewe ndo great thinker wa ukweli
 
Back
Top Bottom