Tusipochukua maamuzi magumu Taifa letu la Tanganyika litapotea kabisa

Hongera Sanaa kwa andiko zuri.
 
BOOKMARK THIS: Ndugu Humphrey Polepole na Ndugu Tundu Lissu hawapikiki chungu kimoja. Kuanzia KIFIKRA, KIITIKADI na KIMALENGO. Atakapotoka nje, Tundu Lissu ambaye anataka kuitoa CCM madarakani ndiyo tutafahamu kwamba kweli Ndugu Polepole anataka nini.

Mpaka sasa nitaendelea kumsikiliza, maana baadhi ya mambo anayoyasema yana ukweli nusu-nusu. MOST OF YOU ARE NOT READY FOR THIS DEBATE.
​
 
Taifa la Tanganyika ndio lipi? Kipi kinakuunganisha wewe na Mtanganyika mwenzako?
 
Kwa style hii itakuwa vigumu sana kuikomboa Tanganyika. Uvyama, ukabila, udini, huyu ni wa Lissu, huyu wa JPM.

Aliyofanya Mange, Maria Sarungi, Polepole huko nyuma yote inabidi yawekwe pembeni kwa sasa tuna adui mkubwa zaidi.

Hao watatu ndio wanatuhabarisha wanaofanya ufisadi, mauaji, utekaji, ndio wanaompigania Lissu atoke. Kwa sasa waungwe mkono.

Watanzania wote wanatakiwa kuwa wamoja wapigane kuondoa huu uongozi dhalimu wa sasa, baada ya hapo serikali ya mpito ikijumuisha wadau wote, watapanga jinsi ya kupata katiba mpya, Tume mpya ya uchaguzi, mahakama huru.

Wanamtandao wanawatawala Watanzania sababu siku zote wanawagawanya na kuwaweka kwenye makundi. Siasa safi, katiba mpya, tume huru, mahakama huru utaletwa na umoja wa Watanzania wote wakiwemo wana-CCM, vyama vya upinzani, wasio na vyama, viongozi wa dini na wadau wengine.

Polepole kajitolea kuwapigania Watanzania akijua wakati wowote wanaweza kumuua. Anasema uchafu wote uliopo ndani ya serikali, wahusika, jinsi unavyofanywa ndani ya CCM na serikalini na jinsi ya kusafisha CCM, serikali, nchi.

Kuwapinga hawa wanaharakati inasaidia kuimarisha hii serikali dhalimu ya sasa, kuwapa nguvu wanamtandao, mafisadi, wauwaji na watekaji. Haisadii harakati za ukombozi wa Tanganyika. Haisaidii Chadema, haimsaidii Lissu.

Polepole ni shujaa wa Taifa. Kumpinga ni kudhoofisha, kukwamisha, kurudisha nyuma juhudi za ukombozi wa nchi hii.
 
MAMBA HUWA ANA NGUVU AKIWEPO NDANI YA MAJI TU.

TAASISI zote za kiusalama duniani kote zina kitu kiitwacho INTEREPOLABILITY. Ambapo mafanikio ya kazi ya JASUSI X inategemea mafanikio ya kazi ya JASUSI Q, tena huenda hata hawafahamiani, wala hawaji kufahamiana. TAASISI haifanyi kazi ikitegemea MTU, bali watu ambao wakiwa wengi hutengeneza MFUMO ambao huwa unakuwa na lengo moja.

Wewe hata uwe JASON BOURNE, JAMES BOND au JACK RYAN usipokuwepo ndani ya MFUMO, huna utofauti wowote ule na MAMBA aliyepo nje ya MAJI. Ndiyo maana hata unapostaafu kuna baadhi ya SECURITY CLEARANCES unabaki nazo, kwasababu wewe umuhimu wako kwa MFUMO utaisha siku pale unapofariki tu.

Sasa wakitaka kukushughulikiwa, kwanza kabisa wanafanya REVOCATION OF SECURITY CLEARANCES, aidha kwa kukataza USIPEWE TAARIFA MUHIMU, au KUPANGARUA BAADHI YA IDARA kwa kuhamisha watu, kuwapa teuzi, kuziunganisha idara (Merger), kuiweka idara moja chini ya nyingine (Subordination) au kuua watu muhimu kwenye idara. Wakishakufumba macho hivi, aidha wanabana fedha zako au wanakuua.

Mataifa mengine, kama UCHINA na URUSI njia yao ni MOJA TU ambayo kwangu mimi naamini ITS THE MOST EFFECTIVE METHOD. Unawapa majasusi "The Scarlet Letter", ambayo itakuhakikishia A CLEAN SLATE, ya kuanza upya. Sema ndiyo hivyo hapa Afrika Mashariki aliyeweza kutoa The Scarlet Letter ni General Paul Kagame tu, ndiyo maana Rwanda mbali na ujinga wa UKABILA, mambo yanaenda.


====================================================
Kule Rumi ya Kale (Ancient Rome) vyombo vya usalama vilikuwa vina adhabu iitwayo DECIMATION, ambapo wanajeshi walikuwa wanagawiwa katika vikosi vya MAKUMI, MAMIA na MAELFU. Tatizo likitokea kwenye kikosi moja unamchukua kiongozi wao unamuambia awaambie wenzake wale tisa wamuue wa kumi. Au wale tisini wawau wale kumia. Au mia tisa wawaue wale mia.

Hili lilileta heshima mno kwa majeshi ya Warumi ambapo wakubwa wa vikosi walifahamu fika kabisa, tukileta uzembe tutaambiwa tuue wenzetu wa kikosi kimoja ambao bahati mbaya sana walikuwa ni watoto wao, wakwe wao au ndugu zao. Hata MONGOLS jeshi lao lilikuwa na nidhamu kwasababu ya adhabu ya DECIMATION.

Ukiisha ingia kwenye vyombo ya usalama ni lazima uwe na nidhamu. Nchi ambayo maafisa wake hawana nidhani huwa haidumu muda mrefu. Hawa watu huwa wanapewa mafunzo, wanafahamu siri na kudekezwa kama mayai kwa mishahara na marupurupu. Wanapoharibika na tamaa, hakuna njia ya kuwarudisha kwenye mstari zaidi ya kuwapeleka mapema ahera.

TANZANIA ilipofika, ili kuokoa nchi ni lazima TUCHUKUE MAAMUZI MAGUMU bila kuonesha hata CHEMBE YA HURUMA, wala SONI. WEWE ambaye umesomeshwa kwa hela za walipa kodi, ukawa hadi Balozi, watoto wako wako International Schools halafu ukasaliti kiapo chako, ulitegemea kitokee nini ??? A Bullet at the back of your head or A Noose around your neck.
​
 
Ngoja tuone inaendeleaje
 
Ni wazi nayosoma hapa yameandikwa na kijana wa zamani haswa. Gen Z kutumia alama kama mkato, nukta n.k ni jambo gumu sana kwao.

Tatizo letu ni mfumo mbovu na muendelezo wa utamaduni wa hovyo wa kuogopa kuulizana na kuchukuliana hatua. Hali ambayo imechangia hata watu wenye nia ya kweli wanaoingia serikalini kupoteza utashi na nia yao.

Sehemu kadhaa umeeleza kuwa hatuitaki mijadala fulani na hii ni kwa sababu ya muendelezo wa baadhi ya tabia tulizokuzwa nazo. Kama tuliruhusu sheria muhimu kama za idara ya usalama wa taifa kupitishwa bila kujadiliwa kwa kina niwazi bado kama taifa hatuyajui maslahi yetu wala hatuyahitaji. Ni wazi hatujui tunataka nini na tutakipataje.
 
Umefafanua vizuri sana...

Kila mtu amejua tatizo ni wanamtandao...

Lakini mwisho unamlalamikia mtu anayepambana na wana mtandao...

Badae unajaribu kuwagombanisha polepole na lissu, ambao wanaweza wasiwe chama kimoja ila wote ni maadui wa samia na mtandao...

Na badae tena unajaribu kufanya ramli, kwamba mmoja akitoka jela hawatoelewana...

Kipi ni kipi brother...

Kitu unachokosea, kuna namna humfahamu Lissu...

Lissu ni mweupe wa roho na yuko tayari kushirikiana na yeyote kupambana na adui...

Lissu sio mbowe, mbowe anatabia za chuki...

Lissu anaweza kufanya kazi na yeyote ili mradi ameonesha nia njema...

Humfahamu polepole...

Polepole amenyooka sana na ni rahisi kufanya kazi na watu walionyooka kama lissu...

Ndio maana alipewa ugali na kikwete ila hakuendana nae, amekuja kuendana na magufuli...

NB: nyinyi ndio mlimtengeneza shetani ndani ya magufuli...

kipindi magufuli anaanza kazi alikua na nia njema ya kushirikiana na kila mtu...

baadae mkaanza kutumika na mtandao, pamoja na usomi wenu...

kipindi cha magufuli ndio tuliona wasomi wa jf wakipinga miradi ya bwawa la mwalimu na sgr kwa kutumia sababu za watu wa ulaya na marekani...

eti pollution...

miradi ya daraja la busisi ikapingwa na wasomi wetu kwasababu za kikabila...

wengine tukajiuliza mwanza sio tanzania? mbona miradi mingi inaenda dar, arusha, pwani na dom watu hawalalamiki?

kwa jinsi watu wa mwanza walivyokua wanahangaika kuvuka pale ferry halafu msomi mmoja anakuja kukwambia daraja limejengwa kikabila, unashangaa!

kumbe ndugu zetu mnatumika mda huo, akili mmeweka kwenye mfuko...

yaani anaibuka msomi mmoja anakwambia mradi wa bwawa la mwalimu ndani ya mbuga utasababisha uchafuzi mkubwa wa mazingira na dunia haitakua mahali salama...

unajiuliza huyu ni msomi kweli? kumbe mwenzako ameweka akili mfukoni, anatumika...

baada ya magufuli kuwagundua...

akaanza kutocheka na mtu...

mkajikuta mmemgeuza magufuli, na ikabaki historia...
 
Utofauti mkubwa uliopo baina yangu na wewe, ni ule uliokuwepo baina ya CICERO na MARK ANTHONY. Cicero aliamini katika Rumi kama Jamhuri ambayo inaongozwa kwa katiba, taratibu na bunge. Mark Anthony akiwa mfuasi mkubwa wa Julius Ceaser aliamini katika mtu, siyo katiba, taratibu na bunge, kwamba mtu maadamu ni Benevolent Dictator basi aachwe afanye chochote kile bila kuangalia madhara kwa vizazi vijavyo.

Jean Monnet aliwahi kusema hivi "For things to work, we need people" but "For things to last we need institutions". Mzee John Pombe Magufuli alipofanya mazuri nilimsifia, na alipokosea nilimsema waziwazi. Kwenye suala zima la MAKINIKIA na STIEGLER's GORGE mpaka siku ya kufa kwangu nikasema kwamba Mzee JPM alipatia sana na historia itamtetea.

Ila hili la kuamini kwamba alipatia kila kitu, na kwamba baadhi ya tabia zake za kidikteta zilianza punde baada ya kuwa Raisi na kuonewa na WANAMTANDAO limenishangaza sana. Ni kweli MTANDAO ulimhujumu Raisi Magufuli, Ni kweli MTANDAO ulimfanyia vibaya, lakini tabia zake nyingi alitoka nazo chini. Hivi kilichomtuma Raisi Magufuli na watu wake kumshambulia Lissu kilikuwa ni MTANDAO au hulka binafsi ??? Vipi kuhusu Ben Saanane, do you think he deserved that ???

Kuhusu Lissu, binafsi nazifahamu hulka zake tokea Ilboru na hawa waliosoma naye Magroup ya WhatsApp huzungumza mengi. Binafsi kuna tabia zake huwa sizikubali kabisa, tena nachelea kusema kwamba kama akiwa Raisi kwa katiba kama hii, yeye naye lazima atateleza tu. SISI NI BINADAMU, we are not GOD who is beyond reproach.

UNAAMINI WANASIASA ??? Good for you, kila la kheri.
​
 
Wazo zuri.
 
Umenena vema.
Kuna vitu JPM alikosea na vingine alifanya vema.
Lissu ana tabia fulani zinazo shabihiana na za JPM mojawapo kutodhibiti kauli zake. Na udikteta kwa mbali.
Anaamini yeye ni bora kuliko mtu yeyote kwenye kufikiri au kufanya maamuzi.
Wote JPM na Lissu wana tabia ya kupenda sifa.
Lissu ni mzuri sana kwenye mambo ya sheria lakini namuona siyo kiongozi mzuri sana.
Lissu ana tabia moja nzuri sana ya kusimamia hoja zake au itikadi fulani.
Kwa nje nje tu namuona Lissu siyo mtu wa rushwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…