Tusipofanya sasa, Tutajuta Milele, ni lazima Wamasai waondoke Ngorongoro

Amani iwe nanyi

Kama tunajali maendeleo ya Tanzania yetu, Ni lazima wamasai waondoke Ngorongoro ili lile eneo liendelee kuwa na wanyama wengi na kuvutia watalii ambao ni moja ya vyanzo vikuu vya mapato kwa Taifa letu
Naomba kuwasilisha!
Utalii unaweza kuwa chanzo kimojawapo na mapato lakini kinaweza kukizidi kile cha wananchi?
 
Wanyama wanaleta watalii wanaoleta fedha nyingi sana zinazonunua madawa hospitali, kujenga barabara na kulipa mishahara ya watanzania wenzangu
Kwa hiyo tuwafukuze wananchi kwenye mbuga ambako ndipo makazi yao ya asili! Kweli nchi yangu Tanzania, ila tunakoelekea sijui maana hata wakulima wanaweza kufukuzwa, maeneo wakapewa wafugaji ng'ombe
 
Duh kweli tz ni kichwa Cha mwenda wazimu.

1. Masai wanasababisha wanyama kuhamia upande wa Kenya

2. TSH 3 - 4 billions zinatumika kuwalea Masai ndani ya ngorongoro Kila mwaka

3. Masai Wana haribu mazingira

4. Masai hawana pa kuzikia

Yote haya, Bado Kuna wapuuzi wanataka Masai aendelee kuishi ngorongoro?

Waondolewe haraka sana
 
Tatizo tuna vigogo wanawatumia wamasai kufuga ngombe kwenye hifadhi
 
Mkuu tunahama sasa, mpaka jana tumejiandikisha wananchi wapatao 453 na bado kuna wengine wengi wanaendelea kujiorodhesha.
 

wenyewe wamesema hawaondoki , hizo taarifa zingine rudishen ela mliolipwa na maulid
 
Wamasai wasinyanyaswe wapewe fidia kama watakubali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…