Tusipofanya sasa, Tutajuta Milele, ni lazima Wamasai waondoke Ngorongoro

Tusipofanya sasa, Tutajuta Milele, ni lazima Wamasai waondoke Ngorongoro

Sio sawa mkenya apone na Mtanzania aumie. Sio vizuri Kenya kuifanyia umafia Tanzania ili maslahi ya Tanzania yaharibike. Kwa nini Kenya wanataka kuharibu maslahi ya Tanzania kwa kupigia chapuo Ngorongoro kufa?
Ni chuki zako tu za kutokuwa na maarifa.....una asili ya uchawi....hayo unayosikia ni makaburu yaliyoko kenya toka kitambo.....usivyo na akili una mlenga ndg yako...ambaye nae ametegwa bila kujua... Huyo Baba nyerere amemkomboa kwa gharama kubwa!! Kupitia "front line state" hakika tutaanza na wewe!!
Inaonekana hata hujui pan Africanism ni nini!...OAU....AU. Ni zero...ndo maana unasumbua..wenzako wkt wako darasani wewe ulikuwa unaenda kuogelea ndo mnatusumbua humu. Haya ni ya drs la tatu huko......km unakumbua kale ka wimbo ka mchaka mchaka....Baba nyrr nipe bunduki mzinga nikakombo......... Unge nyamaza kimyaaa....
 
Amani iwe nanyi

Kama kichwa cha uzi kinavyosema, Kama Mtanzania ninayeipenda nchi yangu, ninayejali maendeleo ya Watanzania wote vizazi na vizazi, leo nasema kwa Sauti moja, Kama tunajali maendeleo ya Tanzania yetu, Ni lazima wamasai waondoke Ngorongoro ili lile eneo liendelee kuwa na wanyama wengi na kuvutia watalii ambao ni moja ya vyanzo vikuu vya mapato kwa Taifa letu

Kwa nini nasema haya?

1. Ngorongoro ni moja ya sehemu chache hapa Tanzania ambazo mtalii ana uhakika wa kuona wanyama walio kwenye hatari ya kupotea Duniani yaani Tembo, Faru, Simba, Nyati na Chui.

Nimefika ngorongoro kusema ukweli hadi Tour guides wanakwambia hivi karibuni imekuwa ngumu sana kuwaona baadhi ya hawa wanyama na sio tu hawa bali hata wanyama wengine ambao huko mwanzoni walikuwa ni wengi na wanaonekana kirahisi na kuvutia watalii wengi na kuongeza mapato mf pundamilia, pofu na wengineo. Hii ni kwa sababu wanadamu wameongezeka sana Ngorongoro na asili ya wanyama pori ni kuwa hawapendi kuchangamana na binadamu na shughuli za kibinadamu zikizidi huwa wanahama.

2. Kuna taarifa za uhakika kuwa Wanyama wanaohama Tanzania wanahamia upande wa pili yaani Kenya hivyo Kenya anafaidika kwa kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu Ngorongoro ambazo zinahamishia wanyama wetu Kenya. Hii ni hatari sana kwa uchumi wa Tanzania kwa sababu siku si nyingi, Watalii hawataona umuhimu wa kuja Ngorongoro na hivyo kwenda Kenya na kufanya nchi yetu kukosa Mapato.

3. Kuna taarifa za uhakika pia kuwa Wamasai waishio Ngorongoro hawana hata makabuli. Hivyo ikitokea mmasai amefariki anaachwa aliwe na fisi na mbweha. kibinadamu hii si sawa.

Napenda kumaliza kwa kusema imefika wakati sasa kwa maslahi mapana ya Tanzania, Wamasai wahamishwe Ngorongoro. Eneo hili ni nyeti na Tanzania nzima tunalitegemea kimapato. Likiangamia, Tanzania imeangamia. Ni wakati sasa Fedha zinazotengwa kuwalisha wamasai takribani bilioni 3-4 kwa mwaka zielekezwe sasa kuwajengea makazi ya kudumu wamasai hawa eneo jingine na kuwapatia teknolojia ya kufuga wanyama wachache tena kibiashara na kuachana na Maisha yale ya kijima

Naomba kuwasilisha!
 
kwa iyo unaona sawa Shughuli za kibinadamu kuzidi Ngorongoro na wanyama kuhamia Kenya kuondoka Tanzania?
Ondoeni Wawindaji na Mahoteli yanayoota kila kukicha, ondoeni watu ambao sio Wamasai Ngorongoro, baada ya hapo hizo shida zote hamtazisikia.
 
Wanyama wanaleta watalii wanaoleta fedha nyingi sana zinazonunua madawa hospitali, kujenga barabara na kulipa mishahara ya watanzania wenzangu
Unique feature ya Ngorongoro ni mchanganyiko wa Wanyapori na Binadamu. Na Ndio maana likaitwa eneo la Hifadhi. Wamasai wamekuwa Wahifadhi wa Wanyamapori KWA sababu wao HAWAWINDI WALA KUUWA WANYAMAPORI, it has been so for decades, ila KWA sasa kuna "Wamasai Waarabu na Wazungu" Ndio wanaowinda na kufukuza Wanyama kutokana na uwindaji wao na Mahoteli yao huko porini. Masai ni sehemu ya Utalii KWA Ngorongoro. Nao wanachangia pato la Taifa KWA Watalii kutoka maelfu ya Kilomita kuja kuona Binadamu anaishi na wanyamapori, lakini pia alietunza utamaduni wake KWA karne na karne.

#AcheniHila
 
Haya yatakuwa mapandikizi ya Kenya yanayotaka Ngorongoro ife ili yakamate soko la utalii Afrika Mashariki
Ngorongoro imepakana na Manyara na Serengeti. Ili ife, inabidi uziue zote hizi pamoja na Masai Mara ya Kenya nayo itakufa. So, hamna Hoja yoyote ya kuwaondoa watu Ngorongoro. Mkitaka waondoeni Waarabu na Mahoteli yote Ngorongoro.
 
Na mm nakazia watoke tu maana hamna namna nyingine watokeeeee...period...watu wanafanya mipango ya kwenda kuishi Mars sisi tunawatetea wamasai wazendelee.kuishi na wanyama pori...maajabu Haya

Hiyo hela ya kuwalisha wanaowatetea Kuna jinsi wanakulaga ganchi hapo haiwezekani kutumia hela nyingi kiasi hicho kwa watu ambao wanaaribu hifadhi yetu hyo hela itumike kuwaandalia makazi mapya waiache hifadhi yetu.

Hatuwataki Tena wamasai ngorongoro waondoleweeee.
Huna Hoja yoyote ya kuwaondoa. Zaidi sana nauona ushabiki maandazi tu kwako. Wameishi na Wanyama KWA milenia zaidi ya 7, leo Ndio unashangaa wao kuishi na wanyamapori? Hiyo ni Akili kweli? Huoni hiyo ndiyo uniqueness yao na hivyo wanapaswa kulindwa?

Ngorongoro ni ya wanangorongoro. Na KWA nini hii Hoja inakuja sasa? Kwamba Ndio Wamasai wameingia sasa hivi Ngorongoro?

Ondoeni kila mtu Ngorongoro wabaki Wanyama tu, asiwepo Mwarabu mwindaji wala mwenye Hoteli ndani ya Hifadhi.
 
Unajua milenia 1 ni miaka mingapi? Au unaropoka tu hapa?
 
Ngorongoro imepakana na Manyara na Serengeti. Ili ife, inabidi uziue zote hizi pamoja na Masai Mara ya Kenya nayo itakufa. So, hamna Hoja yoyote ya kuwaondoa watu Ngorongoro. Mkitaka waondoeni Waarabu na Mahoteli yote Ngorongoro.
Kuna mwarabu gani Ngorongoro? Nani kakwambia Wamasai tu ndo wanatolewa Ngorongoro? Hadi mamlaka wameamrishwa kuondoa ofisi zao ndani ya hifadhi
 
Ondoeni Wawindaji na Mahoteli yanayoota kila kukicha, ondoeni watu ambao sio Wamasai Ngorongoro, baada ya hapo hizo shida zote hamtazisikia.
Hakuna kinachobaki Ngorongoro zaidi ya wanyama kwa ajiri ya hifadhi tu
 
Huna Hoja yoyote ya kuwaondoa. Zaidi sana nauona ushabiki maandazi tu kwako. Wameishi na Wanyama KWA milenia zaidi ya 7, leo Ndio unashangaa wao kuishi na wanyamapori? Hiyo ni Akili kweli? Huoni hiyo ndiyo uniqueness yao na hivyo wanapaswa kulindwa?

Ngorongoro ni ya wanangorongoro. Na KWA nini hii Hoja inakuja sasa? Kwamba Ndio Wamasai wameingia sasa hivi Ngorongoro?

Ondoeni kila mtu Ngorongoro wabaki Wanyama tu, asiwepo Mwarabu mwindaji wala mwenye Hoteli ndani ya Hifadhi.
Ongera kwa kujaza server
 
Back
Top Bottom