Tusipofanya sasa, Tutajuta Milele, ni lazima Wamasai waondoke Ngorongoro

Tusipofanya sasa, Tutajuta Milele, ni lazima Wamasai waondoke Ngorongoro

Upande wa pili mbuga ipi?? Taja hapa
Magharibi na kaskazini magharibi inapakana na Serengeti, kaskazini inapakana na Loliondo na inakwenda hadi Kenya na mashariki karatu na kusini mashariki Hifadhi ya Manyara
 
Amani iwe nanyi

Kama kichwa cha uzi kinavyosema, Kama Mtanzania ninayeipenda nchi yangu, ninayejali maendeleo ya Watanzania wote vizazi na vizazi, leo nasema kwa Sauti moja, Kama tunajali maendeleo ya Tanzania yetu, Ni lazima wamasai waondoke Ngorongoro ili lile eneo liendelee kuwa na wanyama wengi na kuvutia watalii ambao ni moja ya vyanzo vikuu vya mapato kwa Taifa letu

Kwa nini nasema haya?

1. Ngorongoro ni moja ya sehemu chache hapa Tanzania ambazo mtalii ana uhakika wa kuona wanyama walio kwenye hatari ya kupotea Duniani yaani Tembo, Faru, Simba, Nyati na Chui.

Nimefika ngorongoro kusema ukweli hadi Tour guides wanakwambia hivi karibuni imekuwa ngumu sana kuwaona baadhi ya hawa wanyama na sio tu hawa bali hata wanyama wengine ambao huko mwanzoni walikuwa ni wengi na wanaonekana kirahisi na kuvutia watalii wengi na kuongeza mapato mf pundamilia, pofu na wengineo. Hii ni kwa sababu wanadamu wameongezeka sana Ngorongoro na asili ya wanyama pori ni kuwa hawapendi kuchangamana na binadamu na shughuli za kibinadamu zikizidi huwa wanahama.

2. Kuna taarifa za uhakika kuwa Wanyama wanaohama Tanzania wanahamia upande wa pili yaani Kenya hivyo Kenya anafaidika kwa kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu Ngorongoro ambazo zinahamishia wanyama wetu Kenya. Hii ni hatari sana kwa uchumi wa Tanzania kwa sababu siku si nyingi, Watalii hawataona umuhimu wa kuja Ngorongoro na hivyo kwenda Kenya na kufanya nchi yetu kukosa Mapato.

3. Kuna taarifa za uhakika pia kuwa Wamasai waishio Ngorongoro hawana hata makabuli. Hivyo ikitokea mmasai amefariki anaachwa aliwe na fisi na mbweha. kibinadamu hii si sawa.

Napenda kumaliza kwa kusema imefika wakati sasa kwa maslahi mapana ya Tanzania, Wamasai wahamishwe Ngorongoro. Eneo hili ni nyeti na Tanzania nzima tunalitegemea kimapato. Likiangamia, Tanzania imeangamia. Ni wakati sasa Fedha zinazotengwa kuwalisha wamasai takribani bilioni 3-4 kwa mwaka zielekezwe sasa kuwajengea makazi ya kudumu wamasai hawa eneo jingine na kuwapatia teknolojia ya kufuga wanyama wachache tena kibiashara na kuachana na Maisha yale ya kijima

Naomba kuwasilisha!

Nimeacha kusoma hutuba yako baada tu ya kusoma mistari michache. Nadhani ndugu zetu hamna taarifa zote za suali la kuondoshwa kwa kwa masai. Kutoka katika taarifa mbali mbali za vyombo vya habari vya nje ya nchi ni kuwa sehemu hiyo serikali imeliuza eneo hilo kwa kampuni yenye makao makuu yake UAE ili kuifanya sehemu hiyo kutumka kwa trophy kwa watalii!!!!!! Kwa maana nyengine itakuwa ni sehemu ambayo watu watatoka nchi zao za mbali kuja Tanzania kuuwa wanyama wetu na kujichukulia ngozi, vichwa na pembe na kuvipeleka kwao. Sio kuwa itakuwa sehemu ya watalii kuja kuona wanyama ambao hawana nchini kwao na ambao ni fahari kubwa ketu kuwa nao, la! Serikali inaruhusu wanyama wetu wawe wanauliwa sio kwa sababu yeyote ile bali ni kwa mchezo tu. Kwa ufupi serikali imeamua kuweka mbele pesa na iko tayari kupoteza treasure ya taifa. South africa wanajuta kuruhusu mchezo huu na sijui kwa nini tanzania tunaona kuwa hii idea nzuri!!!!!!
 
Magharibi na kaskazini magharibi inapakana na Serengeti, kaskazini inapakana na Loliondo na inakwenda hadi Kenya na mashariki karatu na kusini mashariki Hifadhi ya Manyara
Sasa wanahama kwenda Serengeti au Kenya? kupitia Loliond!!?? Fafanua ili ujibiwe sasa
 
Nimeacha kusoma hutuba yako baada tu ya kusoma mistari michache. Nadhani ndugu zetu hamna taarifa zote za suali la kuondoshwa kwa kwa masai. Kutoka katika taarifa mbali mbali za vyombo vya habari vya nje ya nchi ni kuwa sehemu hiyo serikali imeliuza eneo hilo kwa kampuni yenye makao makuu yake UAE ili kuifanya sehemu hiyo kutumka kwa trophy kwa watalii!!!!!! Kwa maana nyengine itakuwa ni sehemu ambayo watu watatoka nchi zao za mbali kuja Tanzania kuuwa wanyama wetu na kujichukulia ngozi, vichwa na pembe na kuvipeleka kwao. Sio kuwa itakuwa sehemu ya watalii kuja kuona wanyama ambao hawana nchini kwao na ambao ni fahari kubwa ketu kuwa nao, la! Serikali inaruhusu wanyama wetu wawe wanauliwa sio kwa sababu yeyote ile bali ni kwa mchezo tu. Kwa ufupi serikali imeamua kuweka mbele pesa na iko tayari kupoteza treasure ya taifa. South africa wanajuta kuruhusu mchezo huu na sijui kwa nini tanzania tunaona kuwa hii idea nzuri!!!!!!
Hizo habari zilizoandaliwa na wakenya wenye mission ya kuhakikisha Ngorongoro inakufa hazina mashiko
 
siyo rahisi rahisi kama unavyo fikiria, kwenye sheria ya kuwa ruhusu kuishi apo walipo mkoloni alishindilia kabisa na kuwapa haki kubwa wamasaai, bahati mbaya wengi humu ni vijana wadogo wa mlio miaka 20s & 30's, sisi 'waze' tunajua ugumu uliopo ………..!
Hii sio nchi ya Mkoloni...amka wewe!
 
Hizo habari zilizoandaliwa na wakenya wenye mission ya kuhakikisha Ngorongoro inakufa hazina mashiko
Nope my friend. Taarifa zangu nimesoma kupita BBC world news na al jazeera news. Zote zimenukuu exactly nilichosema kampuni inayoitwa OBC (orttelo Business Corporation) ndio wanakodi/wananua hiyo sehemu kwa lengo la kuanzisha trophy hunting business!
 
Hivi kiuhalisia hamna sehemu nyingine ya kuishi zaidi ya kuishi pamoja na wanyama huko Ngorongoro?
 
Kama wewe ni mkenya kubali tu kuwa Tanzania imeamka. Lazima Ngorongoro tuilinde na maslahi ya Tanzania tuyalinde ili utalii uzidi kutuingizia fedha
Mimi wa hapahapa, Ila siendi kama zuzu ilimradi watu wana interest zao niunge mkono....
 
Mimi wa hapahapa, Ila siendi kama zuzu ilimradi watu wana interest zao niunge mkono....
Sasa kama wa hapahapa tetra maslahi ya Tanzania. Hadi wabunge wa Chadema waliopo Bungeni na waliostaafu kina Salome Makamba, Esther Matiko, Mchungaji Msingwa wamesimama na maslahi ya Tanzania pamoja na wabunge WAZALENDO wa CCM wewe kwa nini usisimamie maslahi ya Tanzania?
 
1. UKOLONI;
Kama ilikuwa serikali ya kikoloni, now serikali ya kiafrika mliyoipa mamlaka wenyewe haina hadhi ya kufanya mabadiriko?

2. NEGOTIATE NA MABABU;
Serikali inaendelea kufanya majadiliano hata sasa kuwa nininkifanyike je kuna kosa?

3. IDADI NDOGO, ARIDH;
Eneo lote la aridhi JMT lipo chini kiongozi mkuu wa nchi, ambaye ana mamlaka kufanya mabadiriko na kulinganisha ukubwa wa nchi na mapoli yaliyopo kwingine nje na ngorongoro unadhani aridhi imekwisha na lazima nyie mbaki pale, endapo kuna matumizi mengine?.
1. UKOLONI
Serikali ya sasa ina hadhi ya kufanya mabadiliko kama ambavyo serikali ya kikoloni ilikuwa nayo. Lakini swali ni je,
a. Je, maslahi ya wakazi wa pale yanazingatiwa?
b. Ardhi mbadala yenye hali ya hewa au tabia ya nchi kama pale iko wapi? Serikali ya kikoloni iliwahamishia eneo ambalo halikuwa tofauti na Serengeti hasa kwa shughuli yao ya ufugaji au uchungi wa mifugo kama msemavyo kwa kejeli.
c. Ni mabadiliko gani hayo ambayo mnasema serikali ya sasa ina haki ya kufanya? Serikali ya sasa inataka kufanya nini pale? Je, inataka kubadilisha kuwa national park? Mswada uko wapi?
Watanganyika msidangayike kirahisi.
2. NEGOTIATION
Serikali hii haikufuata utaratibu wa kawaida wa serikali inapotaka kuchukua eneo. Serikali imekuja kujump in baada ya NCAA kuwatumia vyombo uchwara vya habari kuwadhalilisha na kuwatweza utu wa wakazi wa eneo lile.
Ilishindikana nini kufuata utaratibu wa kawaida wa kubadilisha matumizi ya ardhi katika vijiji au miji?
3. ARDHI NDOGO
Inaonekana wewe unaangalia hii nchi kwa macho ukiwa kwenye basi au ndege au gari yako binafsi. Niambie wilaya ambapo kuna ardhi tu imekaa inayoweza kuaccomodate wakazi takriban laki moja watakaondolewa pale NCA.
Na isitoshe watu wanaondolewa na watu wanaohitaji ardhi kubwa kwa ajili ya kilimo na ufugaji.
Sisi hatujazoea kuishi kwenye viwanja vya 20 kwa 20 babu.
Hatujazoea kulima bustani.
Hatujazoea kukaa kwenye joto kama la Vigwaza Pale.
Wamaasai wa Ngorongoro ni tofauti sana na Wamaasai wa mikoa ya Pwani kama Tanga, Moro na Pwani.
Na sisi hatujazoea kukaa koo zetu mbali mbali.
Niambie kijiji gani kiko tayari kupokea idadi yote hiyo ya watu?
Nimesikia wanasema watawapeleka Kitwai kule Simanjiro. Kitwai ni mahali padogo sana kwetu na pia ina hali ya hewa tusioikubali. Bora tufe kuliko kwenda Kitwai.
Wengine wanasema Kilindi; Sisi tunaishi kijamaa. Yaani ng'ombe hawana mipaka ya ardhi kati ya kitongoji kimoja na kingine. Huko Kilindi, watu wanaishi kwa mipaka.
Mkitupeleka Kilindi, mnaenda kuchochea migogoro isiyoisha.
 
Back
Top Bottom