1. UKOLONI;
Kama ilikuwa serikali ya kikoloni, now serikali ya kiafrika mliyoipa mamlaka wenyewe haina hadhi ya kufanya mabadiriko?
2. NEGOTIATE NA MABABU;
Serikali inaendelea kufanya majadiliano hata sasa kuwa nininkifanyike je kuna kosa?
3. IDADI NDOGO, ARIDH;
Eneo lote la aridhi JMT lipo chini kiongozi mkuu wa nchi, ambaye ana mamlaka kufanya mabadiriko na kulinganisha ukubwa wa nchi na mapoli yaliyopo kwingine nje na ngorongoro unadhani aridhi imekwisha na lazima nyie mbaki pale, endapo kuna matumizi mengine?.
1. UKOLONI
Serikali ya sasa ina hadhi ya kufanya mabadiliko kama ambavyo serikali ya kikoloni ilikuwa nayo. Lakini swali ni je,
a. Je, maslahi ya wakazi wa pale yanazingatiwa?
b. Ardhi mbadala yenye hali ya hewa au tabia ya nchi kama pale iko wapi? Serikali ya kikoloni iliwahamishia eneo ambalo halikuwa tofauti na Serengeti hasa kwa shughuli yao ya ufugaji au uchungi wa mifugo kama msemavyo kwa kejeli.
c. Ni mabadiliko gani hayo ambayo mnasema serikali ya sasa ina haki ya kufanya? Serikali ya sasa inataka kufanya nini pale? Je, inataka kubadilisha kuwa national park? Mswada uko wapi?
Watanganyika msidangayike kirahisi.
2. NEGOTIATION
Serikali hii haikufuata utaratibu wa kawaida wa serikali inapotaka kuchukua eneo. Serikali imekuja kujump in baada ya NCAA kuwatumia vyombo uchwara vya habari kuwadhalilisha na kuwatweza utu wa wakazi wa eneo lile.
Ilishindikana nini kufuata utaratibu wa kawaida wa kubadilisha matumizi ya ardhi katika vijiji au miji?
3. ARDHI NDOGO
Inaonekana wewe unaangalia hii nchi kwa macho ukiwa kwenye basi au ndege au gari yako binafsi. Niambie wilaya ambapo kuna ardhi tu imekaa inayoweza kuaccomodate wakazi takriban laki moja watakaondolewa pale NCA.
Na isitoshe watu wanaondolewa na watu wanaohitaji ardhi kubwa kwa ajili ya kilimo na ufugaji.
Sisi hatujazoea kuishi kwenye viwanja vya 20 kwa 20 babu.
Hatujazoea kulima bustani.
Hatujazoea kukaa kwenye joto kama la Vigwaza Pale.
Wamaasai wa Ngorongoro ni tofauti sana na Wamaasai wa mikoa ya Pwani kama Tanga, Moro na Pwani.
Na sisi hatujazoea kukaa koo zetu mbali mbali.
Niambie kijiji gani kiko tayari kupokea idadi yote hiyo ya watu?
Nimesikia wanasema watawapeleka Kitwai kule Simanjiro. Kitwai ni mahali padogo sana kwetu na pia ina hali ya hewa tusioikubali. Bora tufe kuliko kwenda Kitwai.
Wengine wanasema Kilindi; Sisi tunaishi kijamaa. Yaani ng'ombe hawana mipaka ya ardhi kati ya kitongoji kimoja na kingine. Huko Kilindi, watu wanaishi kwa mipaka.
Mkitupeleka Kilindi, mnaenda kuchochea migogoro isiyoisha.