Tusipokubaliana na mtazamo wa Godbless Lema, CCM itaendelea kutawala na katiba ya Sitta itapita

Tusipokubaliana na mtazamo wa Godbless Lema, CCM itaendelea kutawala na katiba ya Sitta itapita

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Posts
2,973
Reaction score
3,904
Kwa miaka 4 sasa tangu Godbless Lema awe Mbunge wa Arusha, nimekuwa nikivutiwa na hotuba zake, nikimfuatilia na kumjifunza kwa karibu.

Baada ya kumfuatilia nimegundua sababu moja kubwa ya Arusha mjini chini ya Godbless Lema kuwa ngome ya Chadema isiyotikisika na ambayo hata ccm wanajua kuwa hawawezi kushinda mwaka 2015.
CCM wanaweza kufikiri kurudisha jimbo lo lote la Chadema lakini siyo Arusha mjini --- Wanajua Lema atashinda Arusha mjini kwa kishindo 2015.

Dalili za ukweli huo ni kuwa chaguzi zote za marudio za madiwani Arusha mjini Chadema ilishinda kwa kishindo pamoja na ccm kukamia kutaka kushinda. Swali la msingi ninalotaka tulijadili ni kwa nini imekuwa hivyo Arusha mjini?
kwa maoni yangu Sababu kubwa ni moja, Godbless Lema amejua tatizo la watanzania na linalochelewesha mabadiliko ni Woga. Agenda kubwa ya Lema Arusha Mjini tangu mwaka 2010 ambayo imefanikiwa sana ni agenda yake ya kudumu ya kuwapa wanaArusha ujasiri. Lema haamini kama mtu mwoga anaweza kuleta mabadiliko. Hilo jambo utaliona kwenye hoja zake Bungeni, kwenye vikao na kwenye hotuba zake kwa wananchi----- anasisitiza kuacha woga na kuwa na ujasiri.

Godbless Lema anaamini kuwa:
Kumwambia mtu mtanzania mwoga Chagua Chadema ni kazi ya hasara kwa kuwa atachagua Chadema na kura zitaibwa huku watu 20,000 watashindwa kulidna kura zao na kutawanywa na polisi 2 kwa sababu ya woga tu na ccm itashinda kwa wizi.

Lema ana amini kuwa unaweza kutumia mil 500 kuzunguka Tanzania nzima kuhubiri ubaya wa ccm halafu Waziri moja wa ccm ataita vyombo vya habari na kuwatisha watanzania kuwa ukichagua chadema nchi itaingia vitani na watu wote kwa uwoga wao wataichagua ccm hata kama dhamira zao hazitaki ccm.

kwa hiyo, kwa mtazamo wa Kamanda Godbless Lema mahubiri yo yote yasiyokuwa ya kuwabadilisha watanzania kuwa wajasiri na kuacha woga ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

Na kwa bahati mbaya sana, ccm wameshajua kuwa watanzania wengi (ukiacha Arusha mjini) ni waoga sana na wanautumia uwoga huo wa watanzania kama mtaji wao, Na ndo maana;

mwaka 1995 waliwaonesha watanzania mauaji ya kimbali ya Burundi na watanzania wakatishika sana,

mwaka 2005, cuf ilipokuwa tatizo siku moja kabla ya siku uchaguzi IGP aliibuka na majambia ya CUF na kuwatisha watanzania - na wakatishika.

Mwaka 2010 walipoona Chadema ya Dr Slaa imekuwa tatizo kubwa zaidi wakaja na vitisho kigogo wa JWTZ na swahiba wa Kikwete,
Adulrahamani Shimbo akawatisha watanzania siku chache kabla ya siku ya Uchaguzi. Dr Slaa alipohoji kama Shimbo alitoa kauli kwa niaba JWTZ au ni kauli yake, hawakumjibu, lakini tayari wameshawatisha wapiga kura na kupunguza kura za wapinzani.
Mwaka 2015 kwa hali ilivyo tutake tusitake, lazima kutakwa na mradi wa kuwatisha watanzania.

Sijawahi kumsikiliza LEMA akitoa hotuba yo yote mahali po pote bila kutaja neno woga. Na amekuwa na kauli mbiu kadhaa zinazozungumzia ubaya wa woga kama vile, Hakuna dhambi kubwa kama dhambi ya woga....... Heri vita ya kutafuta haki kuliko amani inayopumbaza na kuhalilisha utu wa mwanadamu ........ Wakati wa mapambano ukiona wameniua,usilie, kanyaga maiti yangu, songa mbele pigania haki.

Hii ndo siri ya mafanikio ya Chadema Arusha -- wana Arusha hawana uwoga na vitisho vya aina yo yote wala kifo.
Je,ni wabunge na viongozi wangapi wa Chadema wanahubiri ubaya wa woga na kuwatia ujasiri wapiga kura wao??

Binafsi na naamini kuwa mabomu ya Arusha ni mradi wa watawala kuwatisha wana Arusha waachane na Lema na Chadema yake --- wameshidwa vibaya. Wamekufa watu wengi na baada ya vifo hivyo chadema ikashinda kwa kishindo kwenye chaguzi zilizofuata. Wengi hawajui kuwa mabomu yale yangekuwa mahali pengine (siyo Arusha ya Godbless Lema) Chadema ingeshidwa vibaya sana kwa sababu hofu na woga.

Na ifahamike, kila baada ya matukio mashushu wanajazwa mitaani na kuhusisha kila aina ya vurugu hizo na Godbless au Chadema kwa ujumla wake.

Kwa bahati nzuri sana Godbless Lema ameshawajaza ujasiri wana Arusha kiasi kwamba hawaogopi tena kifo kutokana kauli mbiu tajwa hapo juu na nyingine nyingi.

Ni kwa sababu hiyo basi,
Binafsi nimeongoka nimeongoka na nimeamini kuwa tatizo kubwa la watanzania ambalo lazima litatuliwe kwanza kabla ya mengine ni tatizo la Uwoga, mgombea nafasi yo yote wa upinzania asipolitatua tatizo hili kwanza katika eneo lake, anajiandaa kushindwa.

Pili, uchaguzi wa Serikali za mtaa ukianza nachukua likizo nitakwenda kuwajaza ujasiri wana Mbulu hadi wawe kama Arusha mjini.
Huu ndo mwarobaini wa kuiondoa ccm mwaka 2015 kwa sababu hakuna mtanzania asiyejua ubaya wa ccm, tatizo lao ni woga.

Tatu, narudia tena, tusipowajaza watanzania ujasiri mithili ya Godbless Lema hata katiba ya Chenge na Sita italetwa mtaani na watanzania watatishwa na itapita. Wakiweza kuwatisha wabunge, watashindwaje kuwatisha wanachi wa kawaida? Au kama wana ujasiri wa kuiba kura za wabunge kwa kutumia wapambe wa Bunge, watashidwaje kuiba kura za wananchi mtaani kwa kutumia polisi na JWTZ.
Tuondoe kwanza uwoga wa watanzania KWANZA ndipo tufikirie katiba mpya na mradi wa kuiondoa ccm 2015, vinginevyo.............
Nawasilisha.
MICHALE AWEDA.
 
Umeongea sahihi kabisa,hembu ona walimu wanakatwa mishahara eti wajenge maabara,jee kikwete na baraza lake la mawaziri watakatwa hizo pesa pia?Wanajua waalimu ni dhaifu waoga ndio maana wanawachezea hivyo!Ingekua nchi zilizoendelea rais angekua hana kazi muda huu
 
uko sahihi nadhani ni wakati mzuri wa cdm waunde cheo kiitwe "mhamasishaaji mkuu taifa" hata kama hakipo kwenye katiba yao kinaweza kutengenezwa kwa malengo maalum kwa muda kuelekekea uchaguzi 2015 kiwe na wajumbe nganagri nchi nzima, iili tuachane na siasa legelege
 
Ujasiri ni Muhimu lakini pia..Kabla ya yote wapinzani kama wana nia ya dhati ya kuletea ukombuzi wa kweli kwa njia ya Amani inawabidi kuzingatia:
Ujasiri wa Kulinda kura.Kusimamia kutangazwa mshindi na Mwisho kabisa kura za wapinzani tayari sikuzote zimekuwa zikitosha hivyo basi; swala la muhimu na nyeti zaidi ni kusoma Mbinu na Wizi wa CCM. Nawashauri wapinzani wajikite katika kusoma mbinu za kuibiwa kura na kuporwa ushindi vinginevyo kila mwaka watakuwa wasindikizaji tu ka mzee wangu Duvotwa.
Jikiteni kusoma wizi na ngiliba zote za ccm, na huo ndio mpango mzima.
 
Hahahahahaaaaaaa! Naona machadema yanajifariji. Mkuu aweda, unatafuta Uben Saanane nini?
 
uko sahihi nadhani ni wakati mzuri wa cdm waunde cheo kiitwe "mhamasishaaji mkuu taifa" hata kama hakipo kwenye katiba yao kinaweza kutengenezwa kwa malengo maalum kwa muda kuelekekea uchaguzi 2015 kiwe na wajumbe nganagri nchi nzima, iili tuachane na siasa legelege
Lema mwisho wake ni 2015
 
Ni heri vita inayotafuta haki na usawa kuliko amani inayopumbuza-Godlesss Lema.

A very wise saying by wise person.

Hutaki unaacha!
Kama polisi tu wanawafanya muingie kwenye mazizi ya kitimoto, hiyo vita mtapigana na nani?
 
Kwa aya ya mwanzo tu' kichefuchefu! Unavutiwa na matusi yake kwa raisi? Halima Mdee Vs Esta Bulaya, Wewe Vs Lema now. Timizeni zile ndoto za ndoa za jinsia moja anazozitetea Lema.
Kajifungue kwanza
 
Kwa aya ya mwanzo tu' kichefuchefu! Unavutiwa na matusi yake kwa raisi? Halima Mdee Vs Esta Bulaya, Wewe Vs Lema now. Timizeni zile ndoto za ndoa za jinsia moja anazozitetea Lema.

Kama kichef chef Lamba ndim usitapike....
 
TUSIPOKUBALIANA NA MTAZAMO WA LEMA,KATIBA MPYA HAMNA
Lema haamini k
Mkuu Shemeji Mikael Aweda kwanza asante kwa hii!, pili inaelekea uliedit na kusave huku umeikata hii thread, edit tena urudishe yale yaliyokatika!.

Mwisho, nadhani hii thread ni mingoni mwa threads zile zile za watu kuwaabudu watu!, kusifiana ushujaa, huku mkiliangamiza taifa!. Mimi nilikuwepo Arusha wakati wa kampeni za Mhe. Lema, mwenyewe anajua kilichomfanya ashinde, na mimi pia nakijua, na wala sio huo ujasiri maandazi unaousifia humu!. Mhe. Lema ni "populist kind of a leader!", Arachuga ni mji wa machalii, hivyo kadri unavyofanya fujo, ndivyo unavyozidi kupendwa!, na hata ingetokea Osama akafanya ziara AR, Watu wangefunika mbaya viwanja vya Unga LTD!.

Sifa kuu ya Arusha ni jiji la kitalii, linalotegemea uchumi wa kitalii, kwenye utalii amani na utulivu ni muhimu kuliko kuondoa uoga!. Wananchi wa Arusha, wanataka maendeleo na sio maandamano!, hawatakula huko kuondoa uoga!.

Kwa msio jua, ushindi wa Lema Arusha Mjini, ni sawa na Ushindi wa Nasari kule Arumeru, chanzo za shindi zote hizo mbili ni "vita vya panzi" CCM kwa CCM!.

CCM wakiweka nyumba yao sawa, Arusha na Arumeru, 2015 kazi ipo!.

Kwa maoni yangu, 2015, Chadema sio tuu inahitaji viongozi populist kama Lema type, Sugu type etc ili kuvuna kura za vijana ma jobless na wamachinga, pia inahitaji watu able wenye "brain power!" ya kuweza kushika dola na kuunda serikali!. Kuna viongozi wa Chadema they are the best kwenye kuhamasisha maandamano, kuchochea fujo na vurugu!, halafu they do nothing kuhamasisha maendeleo!. Watu wananaka maendeleo na sio maandamano!.

Pasco
 
Ccm haitatoka madarakani kwa kuibembeleza kamwe! Ni liwalo na liwe, ccm hutumia polis na vyombo vya dola vingine kupambana na upinzani. Jukumu la upinzani kwa sasa ni kutoa elimu ya uraia kwa watanzania na kuiandaa jamii kwa mabadiliko.
 
Pasco
Bravo!! Wewe ni mtu makini sana pasco. Hili liaweda pamoja na elimu yake kubwa limebaki hivyo hivyo lilivyoanza chuo, ie ametoka kama alivyoingia
 
Last edited by a moderator:
Ccm haitatoka madarakani kwa kuibembeleza kamwe! Ni liwalo na liwe, ccm hutumia polis na vyombo vya dola vingine kupambana na upinzani. Jukumu la upinzani kwa sasa ni kutoa elimu ya uraia kwa watanzania na kuiandaa jamii kwa mabadiliko.
Ccm ina baraka za haki kutoka kwa mungu.mtahangaika sana
 
Back
Top Bottom