Tusipokuwa makini na watu kuwajibika, basi AFCON 2027 inaweza kuwa bonge la failure badala ya fahari

Tusipokuwa makini na watu kuwajibika, basi AFCON 2027 inaweza kuwa bonge la failure badala ya fahari

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Suala la kuwa mwenyeji wa AFCON 2027 kwa Tanzania, Kenya na Uganda ulitangazwa kama ushindi wa kihistoria kwa Afrika Mashariki. Lakini kadri siku zinavyosonga, ndivyo uhalisia unavyozidi kuwa mchungu.
images - 2026-02-07T185701.697.jpeg

Ila nimeshangazwa sana na taarifa na habari za Tanzania kuomba msaada wa taifa la China mwaka huu wa 2026 ili kuboresha miundombinu ya AFCON 2027. Yaani hii ni ishara ya wazi ya udhaifu mkubwa katika maandalizi na tumeona kuwa kuna watu wana masihara mengi. Ombi hili halionyeshi ushirikiano wa kimkakati, bali linaibua swali gumu: tulikuwa tayari kweli tulipoomba kuwa waandaaji?

Soma Pia: Tanzania yaomba msaada China miundombinu ya AFCON 2027
images - 2026-02-07T185911.262.jpeg

Miundombinu ya usafiri bado iko katika hali isiyoridhisha. Barabara nyingi Dar es Salaam, Arusha pamoja na Zanzibar ni mbovu, hazipitiki kirahisi hasa mvua inaponyesha, na hazistahimili msongamano unaotarajiwa wakati wa mashindano. Huduma za usafiri wa anga ni chache, ghali na zisizo na uhakika, hali inayohatarisha mtiririko wa mashabiki na timu kati ya nchi hizi tatu.
images - 2026-02-07T185719.904.jpeg

Viwanja vya michezo navyo vina shaka kubwa haina haja ya kusifia hata kidogo. Baadhi yake huharibika kirahisi wakati wa mvua, mifumo ya mifereji ya maji ni mibovu sana, na matengenezo hufanyika mara chache badala ya kuwa endelevu. Na baadhi bado havijakamilika hata kwa 60% 😃 Vituko kabsa.
africa-cup-of-nations.webp

Kuomba msaada 2026 kwa mashindano ya 2027 ni kukiri wazi kuwa maandalizi ni dhaifu sana, ni sawa na kwenda kukata tiketi ya basi dakika 1 kabla ya basi kuondoka.
images - 2026-02-07T185838.673.jpeg

Tusipokuwa makini na watu kuwajibika, basi AFCON 2027 inaweza kuwa bonge la failure badala ya fahari.
 
Anjella kairuki kasema usiikashifu serikali wala usiwakosoe viongozi waliochaguliwa na wananchi,utakamatwa na mafwele kijana.tulia fuatilia Simba na yanga zinavyogawa dozi ligi kuu😅😅
 
Back
Top Bottom