Tusipotatua matatizo ya msingi itakuwa kila baada ya uchaguzi tunafanya maridhiano

Tusipotatua matatizo ya msingi itakuwa kila baada ya uchaguzi tunafanya maridhiano

Tusipokuwa makini itakuwa kila baada ya uchaguzi tunafanya maridhiano
Mfano mwaka huu 2026 tupo kwenye maridhiano na itakuwa hivyo hivyo mwaka 2031 tutafanya tena maridhiano na itakuwa mwaka 2036 tunafanya maridhiano sababu hatutaki kuadress mambo ya msingi
View attachment 3641314
Hiyo sio shida kwa CCM, kwanza ni kama mkakati wa kuendelea kubaki madarakani.
 
Sahivi mambo mengi yamesimama kwa sababu kuna uncertainity
Sahihi kabisa. Kuna mambo yanapaswa kushughulikiwa once for all. Tuanze na kura ya maoni juu ya Muungano (uwepo au usiwepo), kama ukiwepo, uwe wa muundo gani. Baada ya hapo tutajua tunaenda kutunga katiba mpya ya Tanganyika au ya JMT (ya muundo fulani). Haya mawili yakishashughulikiwa, yatatatua sana changamoto kubwa ya kisiasa tuliyonayo.
 
4. MASHARTI NA MUDA MAALUMU KUTOKA COMMONWEALTH CMAG(The Ultimatum)

Kutokana na mapendekezo ya Mjumbe Maalum, CMAG imetoa maelekezo yenye ukomo wa muda (Time-bound actions) kwa Tanzania:

Ndani ya Siku 30: Kutatua suala la kushikiliwa kwa Tundu Lissu kupitia njia za kisiasa au kisheria, na kuwaachia wengine wote wanaoshikiliwa kwa kutumia haki zao kwa amani.

Ndani ya Siku 60: Kurejesha upatikanaji kamili wa mitandao ya kijamii na kuacha vitisho dhidi ya vyombo vya habari na watetezi wa uhuru wa kujieleza.

Ndani ya Siku 90: Kuitisha jukwaa shirikishi na la kuaminika la vyama vya siasa (likiongozwa na mwezeshaji huru) kujadili mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi, ushindani wa kisiasa, wafungwa, na uwajibikaji.

Bila Kuchelewa: Kuanza uchunguzi huru wa makosa ya jinai uliopendekezwa na Tume ya Uchunguzi, pamoja na fidia kwa wahanga.

MWISHO WA UBAYA NI AIBU
 
Back
Top Bottom