TEK
Senior Member
- Jul 13, 2015
- 184
- 35
Habari ndigu zangu! Mimi kila siku natamani sana kuona nchi yangu ikipiga hatua na kufika sehemu ambayo itakuwa ni suluhusho la maisha magumu tuliyonayo kisiasa, kihistoria na kiuchumi. Nchi hii inapitia vipindi vigumu sana hasa katika nyanja za siasa.
Siasa za nchi hii zinapitia maigizo mengi sana, kwa mfano miaka mitano ya utawala wa Dr. John Pombe Magufuli kulikuwa na maigizo mengi sana ambayo ilifika mudayakafanya wananchi tuishi kama wageni katika nchi yetu wenyewe. Ni kipindi hiki ndicho tulicho shuhudia watu wakijikana nafsi zao na kuuelekea ukweli wa uongo.
Ukweli wa uongo ni nini? Ni pale unapomuona mwanachama wa upinzani akipanda jukwaani na kutoa sifa zisizo na uhalisia kiasi kwamba ilileta utando kwenye macho ya wananchi wa kawaida hata wakashindwa kuelewa uhalisia uko wapi.
Tunahitaji Uhalisia yaani mtu asimame katika ukweli wake ndipo tutapata uongozi uliodhahiri. Mfano mwingine ndugu msomaji jaribu kukumbuka misimamo ya wanasiasa kuhusu COVID-19 kwa kipindi chote cha Magufuli. Utaona ni kuwa kumbe walikuwa wanaigiza tu kwasababu ya mazingira ya utawala uliokuwepo.
Watu wengi wanaishi maisha yasiyokuwa ya kwao ndiyo maana imekuwa na mzigo mzito kwa nchi yetu kuendelea kwasababu tunauongozi wa maigizo. Wako wanasiasa wengi wako mahali pasipopao na wanaishi maisha yasiyo kuwa ya kwao kwasababu ya hofu waliyonayo kutokana na mfumo wa utawala wa nchi yetu.
Huku mitaani ukiwa unaamini katika Chama cha Upinzani hasa CHADEMA unaonekana wewe ni haini, unaweza kuchukiwa na viongozi wako hadharani na wengine watakufuata binafsi kukwambia kuwa unahoja za msingi lakini achana nazo maana nchi hii haihitaji hizo hoja wewe jali kula ilimambo yaishe.
Tufanyaje sasa iliviongozi wetu wawe halisia? Mimi nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za nchi hii kiasi kwamba imefika muda hadi najiona kama naishi katika nchi ya watu wasiokuwa na mtazamo wa kweli kwa nchi yetu. Tanzania tunahitaji kujitawala, kuongozwa na kuwa na maamuzi yanayojali maslahi ya nchi yetu na huku tukifanya maamuzi ambayo yatailinda nchi dhidi ya utawala usiokuwa na muelekeo tunaoutaka, na hapo ndipo ninapopata jibu kubwa kuwa tunataka KATIBA MPYA!
Madhara ya utawa wasasa yamesababisha Watanzania wengi kuugua ugonjwa wa akili yaani tumekuwa watumwa wa utawala huu kiasi kwamba tunawaona wanasiasa wanaopingana na mfumo ulipo kama wanapoteza muda na kujiharibia sifa zao bure. Watu wengi nchini wanaumwa ugonjwa unaoitwa kwa Kiingereza MIND SLAVERY ugonjwa huu ni mbaya sana maana unaleta shida kwenye mitazamo ya watu kwa kuwaona wanaowaonea ni wema na wale waliogundua kuwa wanaonewa ni wabaya.
Ahsante!