Tusipotoshane, ajira ina nafuu na uhakika zaidi kuliko kujiajiri

Tuache kudanganyana alichosema ndugu kuhusu ajira kina ukweli ndani yake kwa asilimia kubwa sana ...kwa nchi maskini Kama tz kujiajiri risk kubwa Sana pia kutokana na circulation ya pesa ya Sasa kufanikiwa ni kwa extent ndogo Sana na hata ukifanikiwa itategemea vitu vingi Sana ..Kama kiwango Cha mtaji wako..maarifa na Aina ya biashara pamoja na bahati ...kumbuka Africa watu wenye vipato vya uhakika ni wachache Sana hivyo hii inaathiri purchasing power...hivyo hii inafanya mazingira ya kujiajiri kuwa magumu...tatizo la wabongo wanafiki na wazandiki Sana unakuta jitu linasema kujiajiri ni kuzuri wakati lenyewe limeajiriwa ..kwa zilizoendelea na zilizo na watu wengi walioajiriwa biashara ni rahisi lakini tusidanganyane kwanza biashara Africa hazina garantii hata uwekezaji ni mgumu Africa na ndio maana serikari inatoa tax holiday ya miaka mitatu for new investment kozi wanajua mazingira ya kupata faida ni magumu oneni matajiri wa kiarabu wanavyopigana vikumbo kununua timu za uingereza kozi wanajua ukiwekeza kupata faida ni rahisi lakini sio Africa mazingira ya biashara na kujiajiri ni magumu na hayana assurance tuacheni kudanganyana...strive mayisiwa tajiri wa zimbambwe aliwahi kusema serikari za kiafrica ziache kukimbia tatizo la ajira kwa kigezo Cha kujiajiri....inabidi ajira zitengenezwe kwa wingi ndio wengine wachache wajiajiri....pia Cha mwisho hata mindset za watu hawaamini kijana alijiajiri kutoboa unaonekana Kama unapoteza mda coz inajulikana mazingira ni magumu...Mimi mwenyewe nimemaliza chuo mwaka 2016 na nimejiajiri najua ugumu na changamoto zake ..
 
Mleta mada nitajie tajiri yeyote mkubwa nchini au duniani kote alietajirika kupitia mshahara

I could show ya how to juggle anything and make it double Weed, blow, real estate, liquor sto' wit' no trouble - Grand Hustle.
 
Acha kuongea yaani huku kwetu ambako mnapaita mwisho wa nchi kuna jamaa anauza vifaa vya ujenzi, kulingana na mimi ni fundi na tumezoeana sana huwa sometime naingia kwa duka lake naenda kumsaidia kuuza kama wateja wamembana aisee kwa hesabu ya haraka haraka huwa anakunja millioni 2 au 1.5 faida kwa kila siku. Harafu unasema kuajiriwa ni bora, haujui chochote mkuu
 
swala la kujiajiri au kuajiriwa ina tegemea na kichwa cha mtu kuna mwingine kuajiriwa ni utumwa na mwingine anaona ndio ame win maisha labda tujiulize swali hili ,majengo manzuri ,manzuri yaliyo mengi kwenye mkoa wako unaloishi sasa ni waajiriwa au walio jiajiri jibu atakalo toa ndio upande wenye mafanikio .
 
Namshukuru Mungu nimeshaachana na utumwa wa ajira. Nimewahi kufikia Hadi mshahara level ya mlion 2 na stahiki zingine ila nikaja kupiga chini na kupambana kivyangu mtaani.


Ninachojivunia Ni kutengeneza 100 au 200 kwa nguvu zangu .

Kwa mtu mvivu na asie risk taker ajira Ni kimbilio lake ila kwa aggressive Hustlers kitaa ndio kimbilio. Wadau mitaa Ina hela. Tafuta docho Zama. Umiza kicha. Hakuna shimo la hela utaambiwa kiurahisi.


I'm done
 
Kwa mtu mvivu na asie risk taker ajira Ni kimbilio lake
Lengo / Goal huwa ni kuingiza kipato: mtu aliejiajiri anaweza kufungua duka kila siku saa 12 na kufunga saa 3 usiku, akawa anapata kipato kilekile kama cha mwenzake anaefika kazini saa mbili kasoro na kutoka saa 10 na ana siku 150 kati ya 365 za kupumzika mwaka mzima.

Nimewahi kufikia Hadi mshahara level ya mlion 2 na stahiki zingine ila nikaja kupiga chini na kupambana kivyangu mtaani.
mkuu, nimepitia post zako za nyuma, ulipata chumba cha kulala ??

 
tuliza kichwa utajua kujiari na kuajiriwa kipi bora kuajiriwa ni utumwa hatari sana usiniambie
Utumwa upi?

Mtu kaajiriwa anapewa siku 28 kila mwaka kwenda likizo, anapewa siku 128 za likizo akiumwa na analipwa, anapewa wiki 2 akipata msiba na analipwa, anapewa siku 80 akijifungua na analipwa, huyo aliejiajiri vp?

Alieajiriwa anaweza kuingia kazini saa mbili na kutoka saa 10 kasoro,waliojiajiri wengi tunawaona wanaingia alfajiri na kutoka usiku, hapo vp??

Alieajiriwa anaweza akawa anaenda kazini jumatatu hadi ijumaa tu, siku za weekend anafanya shughuli nyingine, pia sikukuu za serikali na dini zipatazo siku 20 haendi, kwa wengi waliojiajiri bado wanaendaga hata kukiwa na sikukuu hizi na mbaya zaidi wengi hawanaga weekend na ikiwepo basi ni j2 tu, utumwa uko wap?

Motivational speakers wamewatia sumu kali mno aisee.....

Mtu una ajira yako huna haja ya kusota ili kupata faida yako ya kwanza ama kurudisha mtaji ama kuwaza hasara,,,,Unaingia kazini mshahara unalamba vizuri kabisa, unajiongeza unaingia kundi la pili.
 
ninakueleza haya kwasababu niliajiriwa na kuacha na sasa mm ni mtu huru. ilikua inanirazimu kuamuka saa kumi na moja nijiandae ili angalau saa moja niwe kazini kutokana na usumbufu wa foleni za dar ilikua kila siku kuanzia saa mbili mpaka saa moja nipo kazini kwani kulingana na kazi yangu wakati mwingine kazi haikuisha uibebe kuifanyia nyumbani ili siku inayofuata uwe umekamilisha nikajikuta niko busy siku saba zote kuwaza kazi ya mwajiri unaweza kuona upo huru barabarani ukaona upo bichi ila akiri yote inawaza jumatatu unaanzia wapi kazi ya boss na unaikamilishaje kiporo kiufupi sikuweza kua na mda hata wa kufikiri juu ya mpangilio wa pesa au nifanye nn hivo maisha yangu ikawa ni mshahara mshahara na mm nilijikuta baada ya miaka minne sijafanya investiment ya namna yoyote zaidi ya suti na shati jeupe kuonekana ninanawili kumbe kiumbo tu moyo ni sonona tupu. baas nikaamua kuacha hata bila maandaliz mazuri nikazama kitaa nimepigika kwa kipindi cha miez sita nikiwa nimebana sana yaan ninamanisha hata kula ilibid nihesabu tofauti na nilipokua nineajiriwa nilikua nikuamuka saa kumi nipo barabarani nikasema acha nipigike kwani nimependa mm kwasasa nipo kitaa mwaka wa pili sasa ila sina nia ya kujisifu nipo kwangu bunju A maweni nyumba imekamilika ninamke na mtoto ninabiashara ambapo mm nimelala vijana wanakuja kuchukua maelezo nikiwa kitandani ninaweza lala mpaka saa tatu nikaamuka nikaanza kupitia vimiradi vyangu wewe tulia utajua utamu wa kujiajiri. ninakubaliana na ww kwamba kuna mateso mwanzoni ila si kama ya kushikiwa akili na mtu yaani ufokewe uambiwe fanya hili kama mtoto mdogo mh siwez kabisa kurudi kuajiriwa
 
Kumbe ww mtoa mada akili hauna, uwezi copy uzi wa mtu akiulizia vitu vingne kwa ajili ya uzi wako, what if alikua anamtafutia mdogo wake hiko chumba au even ni yeye? Ina mnyima nn kutoa maoni kwenye uzi wako.

Pathetic.
 
watumwa mpo wengi katika nchi hii
 
Mimi binafsi mara mia nilipwe mshahara kama ni biashara ntafanya investment. make yale maswala ya biashara kuniendea vibaya miezi mitatu kwa sababu zilizonje ya uwezo wangu sitaki.
 
Naona uyo jamaaa ajakosea kulingana namazo yake but akikua atajua pia anaye sema kujiajil unaweza kuangukia pua anasaau kunawangap wanafukuzwa kazi pia anayesema mshahara wa milion 3 nibora kuliko kijilipa lakitano ajajua lakitano inaweza kufika milion 5 kwa mwezi lakini milion 3 itafika milion 3.5kama boss ataamua
 
B
oss tofautisha ajira siasa na biashara
 
Nimeshaajiriwa na kujiajiri!
Mara zote nikirudi kujiajiri, coz ajira nilitumia napangilia mambo yangu, kama source ya Ku boost mtaji wangu!

Namshukuru Mungu niko kujiajiri, nalima, nafuga, nakusanya mazao, Nina mambo mengi yanayozungusha pesa!

Sijawahi kujua kwanini masomo ya biashara, Commerce, booking, accounts, hayafundishwi kuanzia darasa la 5, sayansi inafundishwa tokea darasa la kwanza. Concept Tu za biashara!

Hili litasaidia mpaka magepu ya ajira, mtu anaajiriwa miaka 5-10 baadaye anajiajiri, wengine wanachukua nafasi yake wanaajiriwa, hivyo hivyo!
 
Fac
t
 
Mishahara imeongezwa...mama anaupiga mwingi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…