Tusipotoshane, ajira ina nafuu na uhakika zaidi kuliko kujiajiri

Tusipotoshane, ajira ina nafuu na uhakika zaidi kuliko kujiajiri

Kujiajiri vs Kuajiriwa
Wale ma ceo wanaopokea mil 60 kwa mwenzi plus allowances za kutosha sijui wanasemaje ktk hili
 
Ajira kitu ingine, imagine huyo mkuu wa wilaya aliwai kuimba ''nakataa kuwa mtumwa najituma'' leo hii anatumwa kama kawaida tu, duh!
 
Kwanza kabisa naomba tuyaelewe haya makundi matatu

KUNDI LA KWANZA - ALIEJIAJIRI / SELF EMPLOYED
View attachment 2008017View attachment 2008020

Huyu biashara inamuhitaji ili iende, yeye ndie ngvu kazi kuu ya kuieiendesha biashara kwa bidii yake na hata akiajiri bado yeye inabidi ahusike kwa level ya juu sana ili biashara iende, Wengi wao inabidi aende dukani kila siku alfajiri mpaka usiku, kutembeza bidhaa mitaani (machinga), fundi cherehani, n.k kundi hili mara nyingi asipoenda ofisini hakuna pesa inaingia hapo, akiumwa hakuna malipo, n.k Kundi hili kusema kweli hakuna uhuru, mtu ukiwa kundi hili usije kujichanganya hata siku moja kujifananisha na watu wa kundi la pili, wenzetu wengi wa nchi zilizoendelea kwenye maarifa, mtu akiingia hili kundi anasota miaka hata mitano ili aingie kundi la pili, cha ajabu huku Tanzania ni kama vile watu wa hili kundi wamridhika kuwepo hili kundi ama hawanana mikakati ya kuingia kundi la pili, wengi nimewajua tangu nipo shule ya msingi bado wapo pale pale, nahisi ni kukosa maarifa kwa kudhani kwamba wapo kundi moja na kundi la pili.


KUNDI LA PILI - MMILIKI WA BIASHARA / BUSINESS OWNER
View attachment 2008018View attachment 2008019


Hawa sifa yao kuu ni kwamba wameajiri watu wengine wawasaidie kuzalisha pesa, hawafanyi kazi ili wapate pesa kama kundi la kwanza na la tatu,
pesa ndio inawafanyia kazi ..Yeye anaweza akanunua kiwanja akapageuza kuwa car wash, vijana wanakuja kuosha magari, ikifika jioni anakuja kuchukua mgao wake. Anaweza akawa ni Mo au Bakhresa ikifika asubuhi watu wanawahi kwenda kwenye viwanda vyao kufanya kazi ili kuwatengenezea pesa na wao kulipwa mishahara,

hata kwa upande wa wasanii, Diamond yupo kundi la pili, kaajiri mameneja, wasanii, n.k ana magari ya kufahari kama rolls royce toleo la mwaka huu, escallade toleo la mwaka jana, yani hata v8 yake inakuwa ya kawaida akizipana gari zake, wenzake wengi wapo kundi la kwanza wanatembelea toyota za mwaka 2014 zilizotumika sana nchini Japan.


KUNDI LA TATU- ALIEAJIRIWA (EMPLOYED)

View attachment 2009001View attachment 2008023

hili kundi lina nafuu kuzidi kundi la kwanza hasa wakiwa wanapata kipato sawa
  • kazi anayoifanya haifanyi peke yake huwa wanasaidiana na wengine kwa hio mzigo haujamuelemea​
  • Mshahara wake atalipwa hata akiumwa ama kuwa na sababu maalum ya kutofika kazini​
  • anaweza kuingia kazini saa 2 na kutoka saa 10 / 11 jioni na kupata muda wa kukaa na watoto kama mzazi.​
  • anapumzika siku za weekend zipatazo 104 , sherehe za kidini na sherehe za kiserikali siku 20, kkizo ya mwezi siku 30, n.k​
  • Kipatoo ambacho ni mshahara atakipata kwa uhakika bila longo longo, pia kuna posho​
  • Anapata status kwenye jamii mfano baba flani ni mwanajeshi, injinia, muhasibu, dokta, hakimu, n.k. ukipata tatizo flani anaweza kutumia nafasi yake kukusaidia.​
  • anaweza kuingia kundi la pili bila kupitia taabu za kundi la kwanza maana tayari ana mshahara na anapata mkopo bila longo longo unaoweza kuwa mtaji na ukagharamia mfanyakazi wa kumtengenezea fedha​

TUREJEE KWENYE MAADA.....

Huwa nashangaa sana mtu wa kundi la kwanza anaeshinda dukani masaa zaidi ya 12, anapigwa na jua mchana akitembeza bidhaa, n.k na faida yenyewe haizidi hata elf 30 kwa siku, Sijui ni wapi anautoa ujasiri wa kumdharau mtu wa kundi la tatu kwa kauli kama "ajira ni utumwa" hapo ikumbukwe yeye na mwenzake wanaingiza kipato sawa lakini mwenzake anafanyia kazi zake ofisini kwenye kiyoyozi, umeme ukikatika generator inawashwa, anafana kazi mpaka saa 10 tu jioni, ana siku siku 150 kati ya 365 za kupumzika kila mwaka, akiumwa bado anapata analipwa, kuna posho za ziada, anaweza kufungua biashara na kuajiri wasimamizi, n.k,

Kauli nyingine ya kijinga ya kujifariji ni kuuliza swali "nitajie tajiri yeyote mkubwa nchini alietajirika kupitia mshahara?" Hapa mtu anauliza hili swali kwa maksudi kabisa ili kujifariji huku akijidanganya kwamba yupo kundi moja na kina bakhresa waliopo kundi la pili, anasahau kabisa kwamba watu wa kundi la pili ni Business owners (wamiliki wa biashara) wanaoajiri watu wawatafutie pesa, hata wakiuchapa usingizi mpaka saa nne pesa inaingia tu.

Kuponda ajira ni utumwa kwa mtu aliejiajiri ni sawa na "sizitaki mbichi hizi", nimeshushudia ajira zikitangazwa, hao waliojiajiri wanazishambulia sio mchezo, mtu anafunga duka lake kapata safari ya kwenda dar kufanya interview,

Kuna vijana wadogo wengi tu wameajiriwa, wanakunja mshahara zaidi ya milioni 2 kila mwezi na wamepiga hatua ya ziada kufungua biashara zao za kuajiri wenzao (kuwa business owners), kujenga wakiwa bado vijana wadogo, n.k Niambie vijana wangapi wa kundi la kwanza wanakuwa wamefika hizo level?

Jiulize kwanini hata wazazi wengi ambao wapo kundi la kwanza wanapigana kufa kupoma kuwapeleka watoto kusoma na kuwaambia wasome ili wapate ajira ?? kwanini wasiwaambie wasome ili wawe kama wao ??
Umeandika vema sana.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Huu mjadala wa kujiajiri na kuajiriwa ni muhimu kujadiliwa kwa upana wake, maana Kuna sintofahamu nyingi hapo ambazo hupelekea baadhi ya watumishi wa serikali kuacha kazi na mwishowe kuanza kuishi kwa kutapatapa.
 
Huu mjadala wa kujiajiri na kuajiriwa ni muhimu kujadiliwa kwa upana wake, maana Kuna sintofahamu nyingi hapo ambazo hupelekea baadhi ya watumishi wa serikali kuacha kazi na mwishowe kuanza kuishi kwa kutapatapa.
Ni naona ajira ufanye huku unaokusanywa kama hauna mtaji kabisa na uwe na uwezo wa saving na malengo ya mda mfupi na mrefu .hii ni poa sana at least uanze business ukiwa bado inakupatia la mshahara ilisimama poa unaacha kazi mazima
 
Huu mjadala wa kujiajiri na kuajiriwa ni muhimu kujadiliwa kwa upana wake, maana Kuna sintofahamu nyingi hapo ambazo hupelekea baadhi ya watumishi wa serikali kuacha kazi na mwishowe kuanza kuishi kwa kutapatapa.
Usiache ajira ili kufanya biashara

Acha ajira, biashara ikianza kukulipa vizuri na kwa uhakika kuliko ajira yako.

Tatizo watu wengi hawana financial education, nashangaa sana mtu anamaliza mpaka chuo hajawahi kusoma vitabu muhimu kama rich dad poor dad au rich man in babylon, hivi vitabu ni muhimu sana kuvisoma kama unaweza kusoma.

Mtu anaacha ajira kisa kawasikiliza motivation speakers waliokariri quotes, motivational speaker anahubiri uache ajira sasa wewe jichanganye humo bila kuongezea akili yako, ndio utajua hujui.
 
Unasema?! Hivi nyie watu mnaishi wapi? Tokeni ndani ya maboksi hayo. Mshahara wa 6m kila mwezi ni hela ya kubeza biashara? Be serious man! Nilitaka nipite kimya ila uzalendo umenishinda.
Yani laki 2 per day eti ndio anatishika. Lol sina biashara lakin najua hio hela ni ndogo sana kwa wenye maduka makubwa ya jumla
 
Kila upande una faida na hasara pia,

1 (a) aliyeajiriwa anaweza kuwa na mikopo mingi ambayo hajaifanyia cha maana zaidi ya starehe
(b) aliyejiajiri atahakikisha mkopo unafanya kazi ya jinsi alivyopanga

2 (a) aliyeajiriwa kipato chake kina uwezo wa kumtosheleza endapo ana nidhamu ya fedha
(b) aliyejiajiri kipato chake inabidi awe na bajeti kali ili kumuwezesha kutekeleza majukumu mengine nje ya mahitaji ya kila siku

NB: Ajira hazipo ndio maana kujiajiri kunaonekana kunafaa, mtu akiwa na kianzio tu anaingia kupambana badala ya kusubiri ajira ambazo zina mamilion ya wahitaji wanaosubiri kuajiriwa
 
Kuna tofauti kubwa kati ya mfanyabiashara na mjasiriamali, mfanyabiashara anaweza kuacha biashara akatamani kuajiriwa; lakini mjasiriamali hana mtazamo wa kuajiriwa kamwe, yuko tayari hata zaidi ya miaka 10 apate hasara, lakini atimize kile anachokiamini. Wajasiriamali huwa ni 'greatest thinkers'. Mafanikio mnayoyaona hapa duniani ni kwa sababu ya wajasiriamali. Kwa mtazamo wako wewe, huna 'element' za ujasiriamali. Pia, ujasiriamali 'is not for every one'.
 
Back
Top Bottom